Huu Ndio Ulevi Pekee Ambao Unapaswa Kuwa Nao


Rafiki yangu mpendwa, najua umekuwa unasikia kuwa ulevi ni noma! Ulevi ni hatari. Mimi mwenyewe siyo kwamba napinga hili. Hapana, nakubaliana nalo kwa asilimia zote, ukweli ni wamba ulevi ni hatari kwa afya yako.

Watu wanajiiingiza kwenye aina mbalimbali za ulevi. Kuna ambao wanaingia kwenye ulevi wa pombe, wengine madawa ya kulevya, wengine mitandao ya kijamii na hata wengine umalaya.

Sasa siku ya leo napenda nikwambie aina mpya ya ulevi ambao unapaswa kujihusisha nao. Na ulevi huu ni ulevi wa kufanya kazi kwa bidii.

Hii ndi aina pekee ya ulevi ambayo inaweza kukusogeza mbele na kukufanya wewe uweze kufika mbali maishani mwako. Hakuna aina nyingine ya ulevi ambayo inaweza kukuletea maendeleo tofauti na aina hii tu ya ulevi. Kwa hiyo, kama unataka kufanya makubwa rafiki yangu, zama kwenye ulevi wa kufanya kazi kwa  bidii.

Hii ndio aina pekee ya ulevi ambayo ninaweza kukushauri ujihusishe nayo rafiki yangu. aina pekee ya ulevi ambayo inaweza kukuletea maendeleo.

Achana na ulevi mwingine wowote ulioo nao.

Kila la kheri.

Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA nashauri sana usome kitabu hiki.

Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

Fanya hivyo sasa hivi.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X