JINSI YA KUJUA THAMANI YA MUDA WAKO


Tuna rasilimali nyingi ambazo tunaweza kutumia kwenye maisha yetu ya kila siku.

Rasilimali hizo ni kama

  • Ardhi
  • Madini
  • Maji
  • Fedha
  • Muda ……

Kati ya hizo rasilimali zote, muda ndio rasilimali ambayo ukiipoteza huwezi kuipata. Hivyo, unahitaji kuweza kuitumia vizuri rasilimali hii ya kipekee.

Na leo nataka nikwambie namna ambavyo unaweza kujua thamani ya muda wako. Kujua thamani kutakusaidia zaidi kuwekeza nguvu zako kwenye kufanya kazi na majukumu ambayo ni ya muhimu, huku ukiachana na majukumu ambayo siyo ya muhimu

Ili tujue thamani ya muda wako, kwanza unapaswa kujua kiasi gani unataka kuingiza kwa mwaka mmoja ujao. Je, unataka kuingiza kiasi gani kwa mwaka mmoja ujao? Ebu kwa mfano tuseme kwamba una mpango wa kuingiza milionoi 100. (Hiki kitu tukiite A)

Kitu cha pili cha kujiuliza ni muda kiasi gani ambao uko tayari kufanya kazi kwa wiki? Kama kwa siku unafanya kazi kwa saa 15 na kwa wiki unafanya kazi kwa siku sita. maana yake kwa wiki unafanya kazi kwa saa 90 (Hiki kitu tukiite B).

Na kitu cha tatu ambacho tunataka tujue ni je, kwa mwaka utakuwa tayari kufanya kazi kwa wiki ngapi? Kwa kawaida mwaka una wiki 52. Sasa ni wiki ngapi utakuwa tayari kufanya kazi ukiondoa wiki za mapumziko. Kama unapumzika kwa mwezi mzima kwa mwaka, maana yake unafanya kazi kwa wiki 48 tu kwa mwaka (hiki kitu tukiite C).

Sasa kifuatacho, ngoja tuone thamani ya muda wako kwa kutumia vipengele hivyo hapo juu. Kujua thamani ya muda wako utachukua.

Thamani ya muda ni sawa= (A÷B÷C)

Kwa hiyo kama una mpango wa kuingiza milioni 100 kwa mwaka na kufanya kazi kwa saa 90 kwa wiki kwa wiki 48. Hivyo,

Thamani ya muda wako= (100,000,000÷90÷48)=23,146

Kwa hiyo wewe thamani ya muda wako ni sawa na 23,148. Ukifanya kazi yoyote ambayo ni ya chini ya hivyo viwango, basi unakuwa umejishusha.

Kama ulikuwa hujawahi kupima thamani ya muda wako, Ebu fanya hivyo siku ya leo. Utajifunza vitu vingi na kikkubwa zaidi ni kwenye utunzaji mzuri wa muda wako. Rafiki yangu, tunza muda wako vizuri kulingana na viwango vyako vya fedha ambavyo unatakiwa kulipwa kwa saa.

Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA pamoj anakitabu na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO nashauri sana usome vitabu hivi.

Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

Fanya hivyo sasa hivi.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X