Siku hizi imekuwa ni rahisi kuandika mtandaoni. Status za WhatsApp, Facebook na maeneo mengine.
Kitu hiki kinawafanya watu waandike jumbe fupi Ila nzuri ambazo huwa zinapotea baada ya muda.
Kwa mfano, mtu anaandika status ya WhatsApp, lakini inapotea baada ya saa 24. Ule ujumbe wake mzuri alioandika unapotea na hauonekani Tena. Na wengi wanaoandika kwenye status huwa hawatunzi kumbukumbu za kile walichoandika. Kwa hiyo baada ya mwaka akitaka kurejea alichoandika mwaka mmoja uliopita. Kinakuwa hakipo! Halafu eti ninasema baada ya mwaka. Mwaka wote huo.
Hata baada ya saa 24. Ebu fikiria jumbe nzuri ngapi zinapotea tu kama upepo kila siku. Jumbe ambazo watu wanaweka WhatsApp na bado hazimnufaishi mtu yeyote.
Kama wewe ni mpenzi wa kuandika kwenye status za WhatsApp Basi leo Kuna kitu nataka nikwambie.
Unaonaje badala ya kuandika jumbe zako hizo nzuri na kuziweka WhatsApp tu Ambapo zinapotea baada ya saa 24 ukiziweka sehemu Ambapo hazipotei Kama kwenye blogu. Unaweza hata kutengeneza blogu ya bure mtandaoni. Ukawa unaziweka huko kwa ajili ya kumbukumbu ya baadaye.
Unaonaje badala ya kuandika status fupi za WhatsApp ukiandika makala ndefu ya kuweka kwenye blogu, halafu ukatoa kipande tu cha kuweka status Kama kawaida yako.
Unaonaje ukiendeleza jumbe zako fupi na kuzifanyia KUWA kitabu?
Siyo kwamba huwezi kuandika kitabu. Unaweza vizuri tu, Mimi nina hakika ukijumuisha status zako zote ambazo umekuwa unaandika whatsap kwa miaka sasa, utakuwa umeshaandika kitabu kikubwa. Sasa kwa nini usiamue kuanzia hapa kuandika kitabu chako.
Nina uhakika Kati ya wote watakaosoma ujumbe huu, wengi wataupuuzia, mmoja ataufanyia kazi na baada ya mwaka atatoa kitabu chake. Na nitamwandika hapa jamvini. Sasa kwa nini mmoja huyo asiwe wewe?
Ebu chukua HATUA.
Najua utakuwa unakwama kwa kujiuliza, nawezaje kuanza kuandika kitabu? Jibu ni rahisi sana. Hakikisha unapata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA (Hardcopy) na kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU (softcopy). Kuvipata hivi Vitabu wasiliana nami kwa 0755848391
Hivi vitakupa mwongozo wote unaouhitaji.
Kila la kheri.
2 responses to “Kama Wewe Ni Mpenzi wa Kuandika kwenye Status Za WhatsApp Basi Leo Kuna kitu Nataka Nikwambie.”
Ujumbe mzuri sana na funzo kwa waandishi wote🙏🏿
Hakika.