Kitu Kimoja Cha Kufanya Unapokutana Na Watu


Unaendeleaje rafiki yangu mpendwa. Siku ya leo ningependa tujadili kitu kimoja cha kufanya unapokutana na watu. Kitu hiki ni kubadili maisha yao na Kuyafanya kuwa bora zaidi kuliko ulivyowakuta.

Yaani, kuwainua na kuwafanya wajisikie vizuri ZAIDI Kuliko pale walipokuwa hawajakutana na wewe.

Hii Ni moja sifa ya viongozi na watu wote WALIOFANIKIWA.

Kwa hiyo kila ukikutana na mtu, angalia ni kitu gani unaweza  kufanya kumwacha bora zaidi ya vile ulivyokuta mwanzoni?

Kuwa sehemu ya kusambaza upendo,  na furaha. Kuwa mtu wa kuhamasisha watu. Kuwa mtu wa kuwaacha watu Bora ZAIDI ya vile ulivyokuta. Hivi ndivyo viongozi wote wakubwa wanavyofanya.

Ukikutana nao unapata hamasa ya kwenda kufanya kazi kwa ubora ZAIDI.

Siyo kwamba wanakukatisha tamaa.
Siyo kwamba wanakufanya ujisikie wa chini Kuliko wao. Bali wanakuwa nyuma yako kuhakikisha kwamba wanakusuma uende mbele zaidi.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X