Kitu kimoja kitakachokusukuma wewe kuweza kufanya makubwa


Habari ya upande wa huko rafki yangu wa ukweli, siku ya leo ningependa kukwambia kitu kimoja ambacho kitakusukuma wewe kuweza kufanya makubwa. na kitu hiki siyo kingine bali ni upendo. Upendo unapaswa kukusukuma wewe kufanya kitu kwenye maisha yako. Bila upendo sidhani kama kuna kitu cha maana ambacho utafanya hapa duniani.

Upendo wa kazi

Upendo wa kazi ndio unapaswa kukusukuma wewe katika kufanya kazi, yaani, ufanye kile ambacho wewe mwenyewe unapenda na uhakikishe kwamba umekifanya kwa ubora wa hali lya juu sana. Ukiwa na upendo kwenye kazi hakuna kitakachoshindikana, utahakikisha unajisukuma kufanikisha kazi yako kuliko ambavyo mtu mwingine amewahi kuifanya hiyo kazi na hivyo kupiga hatua kubwa kuliko mtu wa kawaida.

Upendo kwa familia yako.

Upendo kwa familia ayako ndio utakusuma wewe kuihudumia familia yako.

Upendo kwa jamii yako

Upendo kwa jamii yako ndio utakusukuma wewe kutatua matatizo yanayoikumba jamii yako. Ni kwa sababu unapenda kuona watu wa jamii yako wakipata huduma mbalimbali karibu yako, ndio maana umeanzisha biashara.

 Ni kwa sababu hupendi kuona jamii yako inahangaika kwa sababu ya maji, ndio maana, umeanzisha kisima cha maji karibu yako.

Upendo kwa taifa lako

Ni kwa sababu ya upendo kwa taifa lako ndio maana unawekeza kwa ajili ya kesho. Ni kwa sababu ya upendo kwa taifa lako ndio maana unaanda kizazi kijacho vizuri kwa kuhakikisha unakifundisha misingi ya maisha na misingi ya kazi.

Upendo wa jina lako

Ni kwa sababu ya upendo wa jina lako ndio maana unahakikisha kwamba, kila kazi ambayo unafanya inafanyika kwa ubora wa hali ya juu. Hakuna kugushi wala kufanya kazi chini ya viwango.

Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA nashauri sana usome kitabu hiki.

Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

Fanya hivyo sasa hivi.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X