Kwa nini unajipunja hivyo?


Wahaya wana usemi unaosema hivi, “endirira ekagaba emikira yayeyebwa”. Ukiniuliza tafsiri yake sijui ila nitakupa stori😂😂.

Inasemekana hapo zamani za kale kulikuwa na mkutano wa wanyama. Kitu kikubwa kwenye mkutano huo ulikuwa ni ugawaji wa mikia.

Mnyama aliyepewaa jukumu la kuwagawia wanyama wengine mikia ni mnyama mmoja ambaye kwa kihaya anaitwa NDIRIRA. Kiswahili chake sikijui aisee😂😂. Anayejua ataniambia baadaye nirekebishe🙈🙈.

Sasa mnyama NDIRIRA aligawa mikia kwa wanyama wote. Wengine akawapa mikia mirefu, wengine akawapa mikia ya saizi ya kati na wengine mikia mifupi.

Halafu, mikia ikaisha….

Mwisho wa siku yule mnyama alijisahau, akawa amebaki na kitu kilichokuwa hakieleweki ni mkia au siyo mkia….

Akaambulia hicho tu…

Sasa kwa nini nimeandika hivi leo.
Nataka nikwambie kuwa usijipunje. Una ndoto kubwa, zifanyie kazi na kitakachokuwezesha wewe kufikia hizi ndoto kubwa ni mwongozo sahihi.

Mwongozo huu ndio nimeuandika kwenye kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO.

Hakikisha unapata mwongozo huu wa kipekee sana, utakaokusaidia wewe kuzifanyia kazi ndoto mpaka kuzifikia. Usipopata mwongozo utakuwa unajipunja.

Mwongozo huu unapatikana kwa 20,000/-.

Utatuma fedha kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA halafu utaniambia uko wapi ili uweze kutumiwa kitabu hiki.

Gharama kidogo za usafiri zitaongezeka kulingana na eneo ulipo.

Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
www.songambele.co.tz
0755848391
Morogoro-Tz


7 responses to “Kwa nini unajipunja hivyo?”

  1. My friend Godius nakusalimu kaka yangu kwa upendo mwingi sana. Huwa ninaona na kuthamini harakati zako za kutuelimisha watu wote na hasa vijana kwa kutumia kalamu yako. Bigup sana kamanda. Sema kwa upande wangu niko kwenye mapambano yaani front line. Zaidi tutaongea ndugu yangu

  2. Asalaam kaka

    Hakika nakufuatilia sana na sipendi kusoma jumbe zako kama sijatulia maana nazielewa sana

    Nafurahia kazi zako na nakuahidi kukuunga mkono katika vitabu vyako vyote napenda hard copy

  3. Hongera kaka kwa makala zako nzuri hakika tangu nimekufahamu kuptia Temino ya Clouds fm nazidi imarika via your positive inspiration- See You At The Top

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X