Ni makosa Yapi Kati Ya Haya Matatu Umewahi Kuyafanya Maishani Mwako?


1. Kuwa na wazo la BIASHARA au uwekezaji Ila ukachelewa na baadaye watu wengine wakalifanyia kazi

Umewahi Kuwa na wazo la BIASHARA ambalo ulikuwa ukifikiria kulifanyia kazi Ila ukachelewa kulifanyia kazi. Baadaye likafanyiwa kazi?

2. Kuweka Mipango mikubwa mwanzoni mwa mwaka ambayo hukuwahi kufanyia Kazi?
Au labda umewahi Kuwa na mpango mkubwa sana, mwanzoni mwa mwaka. Mpango  wa kuanza kusoma
Mipango ya kupanda miti
Mipango ya Kujenga n.k Ila hukuwahi kuifanyia kazi?

3.  Kuwa na kazi kubwa ambayo ulisubiri kuifanya siku ya mwisho.

Au pengine umewahi kupewa kazi ya kufanya ofisini, ukaisubirisha mpaka siku za mwisho mwisho ndio ukaja kuifanya na baadaye ukawa uneifanya hovyo.

Kama umewahi kufanya kosa lolote hapo na kama bado Kuna kosa unafanya hapo, maana yake umekuwa unasubiri kufanya kitu kikubwa kwa wakati mmoja. Yaani, umekuwa unasubiri ufanye kitu kwa mapinduzi badala ya kufuata mfumo wa mageuzi.

Unajua mapinduzi ni Nini.

Mapinduzi ni mabadiliko ambayo huwa yanatokea ndani mfupi Sana. Yanaweza kuchukua sekunde, dakika au siku chache. Ila yakitokea huwa yana tabia ya kurudiwa tena.

Ila mageuzi kwa upande mwingine huwa yanachukua muda. Miaka na miaka. Ila yakitokea, huwa yametokea na huwa hayarudi nyuma.

Sasa wewe kwenye maisha yako unahitaji mageuzi. Kufanya vitu hata kama ni kidogokidogo bila ya kurudi nyuma. Na hapa ndipo unahitaji mwongozo wa kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA.

Hiki kitabu kimeeleza kwa kina, namna unavyoweza kuitumia NGUVU Hii ya VITU VIDOGO kufanya MAKUBWA.

Hakikisha unapata nakala yako leo hii. Nakala moja ya kitabu hiki ni 20,000/- tu.

Na unatumiwa popote pale ulipo duniani.
Audiobook na softcopy pia vipo.
Fanya malipo kwa 0755848391 Sasa ili utumiwe  nakala yako.

NAKUKUMBUSHA TU: Endapo hutachukua hatua ya kupata kitabu hiki cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA miaka mitano ijayo utakuwa unaendelea kufanya makosa hayahaya Tena kwa kuyarudia.

Na hicho kitu ndicho Albert Einstein alikiita ujinga pale aliposema, “ujinga Ni kurudia kufanya Mambo yaleyale huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti.”

Chukua hatua sasa. Pata nakala yako kwa elfu 20,000 tu. Tuma fedha kwa namba 0755848391

Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
Morogoro-Tz
+255755848391

Karibu sana


One response to “Ni makosa Yapi Kati Ya Haya Matatu Umewahi Kuyafanya Maishani Mwako?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X