Nadhani imewahi kukutolea maishani kwamba unapenda kuanzisha kitu na kukifanyia kisha baada ya muda kidogo unaachana nacho. Au baadaye unaanza kujiambia kwamba nitakifanya kesho au wiki ijayo.
SIKU ya leo Nina mbinu ambayo inafahamika kama Seinfeld Calendar.
Kuifahamu Seinfeld Calendar ngoja kwanza tujue Seinfeld mwenyewe alikuwa nani kiufupi.
Huyu alikuwa ni mwigizaji ambaye kwa miaka mingi alikuwa akitengeneza maigizo yaliyokuwa yanakonga nyoyo za watu. Watu walishangaa kwa nini alikuwa hashuki kwenye chati.
Sasa SIKU moja ndipo alipoeleza hii Siri take ya mafanikio. Akisema kwamba, Siri kubwa ya mafanikio yake ni kuwa huwa anaandika maigizo kila SIKU. Kadiri anavyoandika ndivyo anapata hamasa na mawazo mapya ya kuigiza kila SIKU.
Aliendelea kwa kusema kwamba yeye huwa ana kalenda kubwa ambayo huwa anaiweka chumbani kwake au sehemu yoyote ambapo inaonekana. Halafu anakuwa na mark pen kubwa nyekundu. Kwenye kalenda anaweka X kubwa SIKU ya mwisho ambayo anataka igizo lake liwe limekamilika. Halafu anaanza kulifanyia kazi Sasa.
Kila siku anapofanya kazi anaweka X kubwa. Muda siyo mrefu anakuwa ameweka X nyingi, kiasi kwamba mchakato wake unakuwa Ni kupongeza X ZAIDI kwenye kalenda. Anasema kadiri inavyokaribia siku ya mwisho ya kukamilisha jukumu, ndivyo anakuwa anajisukuma zaidi ili kukamilisha jukumu husika. Huku akifurahia mchakato wa KUWEKA X ZAIDI kwenye kalenda.
Rafiki yangu, una jukumu kubwa? Unataka liwe limekamilika Mpaka siku gani? Basi chukua kalenda leo. Weka X kwenye tarehe ambapo ungependa kukamilisha jukumu lako. Kisha anza kulifanyia kazi kuanzia Leo ukiweka X moja baada ya nyingine.
Kila la kheri
Godius Rweyongeza (songambele)
0755848391
Morogoro