Unawezaje Kugundua Kitu Unachopaswa Kufanya Hapa Duniani?


Mwishoni mwa mwezi uliopita nilikwenda Clouds Fm kwenye kipindi cha TEMINO. Kipindi kinachoendeshwa na Harris Kapiga pamoja na Adv. Henry Mwinuka. Sasa baada ya kipindi wakati nikiongea na Adv. Mwinuka kuna swali nilimwuliza, ndipo akawa ameniambia kwamba kipindi anaingia chuoni kuna vitu viwili alikuwa anapenda kufanya.

Moja, ilikuwa ni utangazaji na pili ni sheria. Akawa anasema kwamba siku za kwanza kabisa za yeye kuingia chuoni alikuwa hajafikia uamuzi sahihi wa kitu gani anapaswa kusoma. Hivyo, alikuwa anajifunza kuhusiana na uandishi na wakati huo huo alikuwa anajifunza kuhusu sheria. Anasema kwamba kwa utaratibu wa chuo chao ulikuwa unaruhusiwa ndani ya wiki mbili kuhudhuria kozi yoyote unayotaka na mwishoni mwa hizo wiki ndio sasa ulipaswa kufanya uamuzi wa mwisho wa kozi ipi haswa unapaswa kusoma.

Sasa kwa nini siku ya leo nimeanza kwa kuandika kitu kama hiki. Lengo langu ni moja tu, nataka nikusaidie wewe ambaye hujaua ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya.

Na wewe unaweza kutumia njia hii ambayo aliitumia Adv. Kwenye kuchagua kipi cha cha kufanya maishani mwako.

Kama mpaka sasa hivi huelewi ni kitu gani ambacho unapaswa kufanya, basi unatakiwa kujaribu vitu mbalimbali. halafu kwenye hivyo vitu mbalimbali unavyojaribu, utagundua kitu kimoja ndio kinakuvuta na unakipenda zaidi hicho kuliko vingine.

Basi hapo unaweza kuchana na vitu vingine vyote ambavyo unafanya na kuwekeza nguvu zako kwenye hicho kitu kimoja sasa ambacho unafanya.

Kadiri unavyokuwa unajaribu vitu mbalimbali ndivyo unagundua vitu ambavyo unapenda na hivyo unaweza kuweka juhudi huko.

Lakini pia, unaweza kugundua kile unachopaswa kufanya hapa duniani kupitia maswali ambayo watu wanapenda kukuuliza mara kwa mara. Au ushauri ambao watu wanaomba kwako mara kwa mara. Inawezekana watu wameshaona kwamba kuna kitu unweza. Hivyo, kwa kuagalia kitu ambacho  watu huwa wanakuja kwako kuomba ushauri mara kwa mara, ndio unaweza kugundua kitu ambacho unapaswa kufanya hapa duniani.

Kuna kitu pia, unaweza kuwa unatumia nguvu na uwezo wa kawaida tu, ila ukawa unakifanya na watu wanapenda. Hiki nacho kinaweza kuwa ndio unapaswa kufanya hapa duniani.

Pia, kama una kumbukumbu za vitu ulivyokuwa unapendelea kufanya utotoni. Hizi ni nzuri maana kipindi ulikuwa bado hujapitia mnyoosho kama uliopitia sasa hivi. Ninaposema mnyoosho, namaanisha kwamba sasa hivi jamii imekunyoosha na kukufinyanga kama inavyotaka, tofauti na ulivyokuwa mtoto. Ulipokuwa mtoto ungeweza kusema kwamba nitakuwa rubani, na watu wengekupongeza kwa kusema hivyo. Ila kuna umri uliofikia ambapo wewe mwenyewe ulikuwa unaogopa kusema kwamba unataka kuwa rubani. Si ndio?

Hapo sasa fahamu kwamba ulishaanza kupitia kwenye mnyoosho. Na kama ungepata ujasiri wa kusema hivyo, basi ni wazi kuwa watu wangekucheka na kukuonesha kwamba haiwezekani. Huo ndio mnyoosho ninaouzungumzia leo hii.

Kitu hiki kimekufanya umesahau ndoto na malengo yako na hata kusudi lako.

Sasa leo hii rudi utotoni na ujiulize ni kitu gani ulichokuwa unapenda kufanya utotoni.

Moja ya kitu ambacho nimeeleza kwa kina kwenye kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO ni namna gani unaaweza kugundua ndoto zako.

Kuna sura mbili maalumu kwa ajili ya hili suala. Nashauri uweze kusoma kitabu hiki hapa leo hii, maana kitakausaidia sana kwenye kugundua kitu unachopaswa kufanya hapa duniani. Lakini pia kitakupa mbinu za kuweza kukifanyia kazi.

Siku ya leo una machaguo matatu:

  • Moja Ni Kuendelea na maisha yako Kama yalivyokuwa siku zote bila kusudi maalumu.
  • Pili kuendelea kuishi ambayo jamii imekuchagulia, ambayo pia hayana kusudi lolote la kufanyia Kazi na
  • Tatu, Kuchagua kusoma kitabu Cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO Ili uweze kukujua kusudi lako na kulitimiza.

Gharama ya kitabu hiki ni 20,000 tu. Kupata kitabu hiki wasiliana nami kwa 0755848391 karibu

Kitabu pia kina audiobook take ambayo kwa Bei ya ofa Leo tu. Utaipata kwa 15,000/- tu.

Wasiliana nami sasa ili uweze kupata nakala yako Sasa. Namba ya mawasiliano ni 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X