Maswali Yanaoulizwa Mara Kwa Mara Kuhusu Semina Ya Uwekezaji Kwenye Hisa


Unaendeleaje mwekezji siku ya leo ningependa kujibu maswali ambayo watu wamekuwa wanauliza mara kwa mara kuhusu semina ya uwekezaji kwenye hisa?
1. Semina itaendeshwa wapi?
Semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao kupitia kundi maalumu la whatasap. Na inaenda kudumu kwa siku 10 mfululizo. Yaani, kuuanzia tarehe 1.8.2022 mpaka tarehe 10.8.2022
2.Je, atakayehudhuria semina atajifunza vitu gani kwenye hii semina?
Hii ni semina ya uwekezaji kwenye hisa. Hivyo, mtu yeyote ambaye atahudhuria hii semina atapata elimu yote ya msingi kuhusu uwekezaji kwenye hisa.
 Hiyo mwisho wa semina hii nategemea kuwa kila mshiriki
👉🏿 atakuwa anajua maana ya hisa, hatifungani na VIPANDE.
👉🏿Viashiria vitakavyokuonesha kwamba hapa unapaswa kununua hisa au unapaswa kuuza hisa zako.
👉🏿 Atakuwa anajua namna ya kuchambua kampuni moja baada ya nyingine na hivyo  kufanya uamuzi bora juu ya kampuni ya kuwekeza.
👉🏿kila mshiriki atapata maelekezo ya kufungua akaunti ya kuwekeza na matarajio yangu kuwa kabla semina Haijaisha wengine watakuwa wameshaanza kuwekeza
 👉🏿kila mshiriki atajua namna ya kutumia simu yake katika UWEKEZAJI kwenye soko la hisa na vipande.
👉🏿Atajua kuhusu mnada wa dhamana za SERIKALI na namna ambavyo anavyoweza kununua dhamana hizi.
Halafu tutaona kati ya hisa, hatifungani kipi unaweza kuanza nacho na namna ya kutumia vitu vyote vitatu kutengeneza utajiri.
3. Je, kuna vitu vingine ambavyo mtu akayehudhuria semina atapata.
Ndio vipo. Sambamba na kuhudhuria semina hii ya kipekee unaenda kupata kitabu cha bure tena hardcopy ya kitabu cha JINSI YA KUWEKA AKIBA NA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.
Hiki kitabu utakipata bure bila ya kuongeza gharama ya ziada.
4. JE, Kuna gharama ambazo zitahusika kwenye kuhudhuria semina
NDIO GHARAMA ZIPO, na gharama hizi ni shilingi 21,000/- tu. Ukilipia hiki kiasi utaweza kuhudhuria semina ya siku 10. Na utapata bonasi ya kitabu cha JINSI YA KUWEKA AKIBA NA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE
5. Je, kitabu kinatumwaje kwa watu wa mikoani? Je, kuna Gharama za ziada ya kutuma
Kitabu kitatumwa kwa basi MPAKA mkoani na hakuna Gharama ya ziada inahohitajika ili utumiwe kitabu.
Hii nimesema Ni bonasi unaipata kwa kuhudhuria semina. Hivyo huchajiwi Gharama ya ziada. Wewe Ukilipia 21,000/ tu ya semina unakaa mkao wa kula.  bure.
Kumbe kwa kuhudhuria semina hii Ni Kama unaua Ndege wawili kwa jiwe moja.
Unapata mafunzo ya kina kuhusu UWEKEZAJI kwenye HISA. Na bado unapata kitabu bonasi ya kitabu cha JINSI YA KUWEKA AKIBA NA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.
6. Kitabu nitakachopata kinaendana na masuala ya hisa?
Ndiyo. Kinaitwa JINSI YA KUWEKA AKIBA NA KUANZA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.
Thibitisha kuwa utahudhuria semina hii ya kipekee kwa kutuma ujumbe kwenda 0684408755 Karibu sana.
Jiunge na kundi letu la uwekezaji kwenye hisa hapa
https://chat.whatsapp.com/FbzmwEVkObKIuqeR4pIZmu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X