Uchambuzi Wa Kitabu Cha The Richest Man In Babylon


Kitabu: The Richest Man in Babylon

Mwandishi: Georges Clason

Mchambuzi: Hillary Mrosso

Simu: 255 683 862 481

Utangulizi

Zaidi ya miaka 8000 imepita, mji mkuu uliojengwa kwa ustadi wa juu sana huenda kuliko miji yote duniani ulijulikana kama Babiloni. Sifa za mji huu zilitapakaa duniani kote sio tu kutokana na ustadi na ufahari wa majengo au uzuri au uimara wa kuta za mji huu bali hekima waliyokuwa nayo watu wa Babiloni. Kwa sasa Babiloni haupo tena, historia ya uzuri, uimara, ufahari na umaarufu wake umepotea kwa karne nyingi sana. Licha ya kupotea kwa mji wa Babiloni kuna baadhi ya vitu havikupotea; vitu hivyo ni hekima ya wababiloni hasa hekima na kanuni za kupata utajiri na mali. Hekima hizo zilipatikana zimeandikwa katika vibao vya mawe, zikijulikana kama sharia za dhahabu. Ni sharia hizi ndizo walitumia kutafuta utajiri, kuutunza utajiri na kuendelea kuzalisha utajiri. Hekima hizi za wababiloni ndio zinaweza kutumika kuijenga Babiloni sehemu yoyote duniani. Karibu tujifunze hekima na sharia za wababiloni kuhusu fedha, utajiri na mali.

 1. Siku zote kama unataka ushauri wa kukusaidia kuvuka au kufanya jambo lolote kwenye maisha jaribu kutafuta watu sahihi. Kama vile mfalme na watu wa Babiloni walivyomtafuta Arkadi ili awashauri na kuwapa siri za kupata utajiri na mafanikio.
 2. Kupata mwalimu au mtu sahihi wa kukushauri sio tu atakwambia cha kufanya, bali atakuelekeza namna ya kufanya jambo kwa ufasaha zaidi. Mfano mzuri ni Arkadi sio tu alikuwa mshauri mzuri lakini pia aliwafundisha wengine kwa mifano yake mwenyewe na maisha yake yalikuwa mfano mzuri.
 3. Ni ujinga kuamini kuwa utajiri wa mtu upo katika mifuko ya pesa alizonazo, utajiri wa kweli ni kuwa na mirija inayoingiza fedha katika mifuko yako bila kukoma.
 4. Kuwa na mapesa mengi au dhahabu mifukoni sio ishara ya utajiri au mafanikio, wababiloni wanasema utajiri na ishara zake ni kuwa na mirija isiyokauka inayokuingizia fedha, mirija ya dhahabu golden streams.
 5. Haijalishi matumizi yako ni makubwa kiasi gani, kama una mirija ya uhakika ya kukuingizia kipato katika mifuko au hazina zako bado unaweza kuishi kwa uhuru sana.
 6. Kama hauna utajiri au mali kwenye maisha yako sababu kubwa inaweza kuwa ni kushindwa kujifunza kanuni za kupata utajiri au ulizipuuzia kanuni za kupata au kujenga utajiri. Mfano, Wababiloni wengi walikuwa masikini kwa kutokujua kanuni na sharia za kupata utajiri.
 7. Utajiri hauji tu kwa bahati nzuri au mbaya, utajiri na mafanikio ni matokea ya kujifunza na kufanyia kazi sharia za kupata utajiri. Mfano mzuri ni kutoka wa Nomasir, amabaye alipoteza kila kitu baadaye akakaa chini akajifunza tena kanuni za kupata utajiri alizopewa na baba yake na akafanikiwa kufikia utajiri.
 8. Ili usipoteze muda ukizengea zengea jangwani, jifunze kwa moyo wako wote na kwa akili zako zote kanuni na sharia za kupata utajiri, kutunza utajiri ambazo ziliasisiwa na kutumika na watu wengi maarufu waliofanikiwa hapa duniani.
 9. Mafanikio ya kudumu hayaji tu kwa kufanya kazi kwa bidii pekee, unahitaji kupata maarifa na hekima katika kazi na namna ya kuyatunza mafanikio utakayoyapata.
 10. Njia ya kwenda kwenye utajiri ni kuhakikisha katika mapato yako yote unayopata tenga asilimia kumi pembeni kama akiba yako binafsi.
 11. Haijalishi unaingiza mapato kidogo kiasi gani kwenye shughuli zako, hakikisha unatenga asilimia kumi ya mapato yako kama malipo yako.
 12. Wababiloni wanatufundisha kuwa, tujilipe wenyewe kwanza, na hapa kwenye kujilipa isiwe chini ya asilimia kumi (10%) ya mapato yako.
 13. Wababiloni wanashangaa sana, tunaweza kumlipa kila mtu lakini tunashindwa kujilipa wenyewe, hii ni moja ya sharia ya dhahabu waliyojifuza watu wengi waliofanikwa ikiwamo wababiloni wenyewe.
 14. Kila kiasi kidogo unachoweka kama akiba kwa ajili ya uwekezaji ni mtumwa wako wa baadaye kukufanyia kazi ufanikiwe.
 15. Kila fedha au dhahabu unayoipata na kuweka akiba, iwe kwa lengo la kukufanyia kazi ili ufanikiwe zaidi.
 16. Kama unataka kuwa na utajri endelevu, kila mapato unayopata yanatakiwa yaendelee kukuzalishia mapato zaidi, hasa sehemu ya mali ulizowekeza au kuweka akiba.
 17. Kama umeamua kujilipa mwenyewe kama wanavyoshauri wababiloni, haitakiwi kuwa chini ya asilimia kumi ya mapato yako. JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA.
 18. Wababiloni wanasisitiza sana, hatakama mapato yako ni kidogo kiasi gani, jambo la kwanza kufanya kwenye mapato yako ni kujilipa kwanza, iwe asilimia kumi ya mapato yote.
 19. Ukipata fedha zako, usinunue nguo kwanza, usinunue viatu, usinunue gari, usinunue simu, usinunue mabati, usikimbilie kulipa madeni kwanza, jilipe mwenyewe kwanza.
 20. Baada ya kujilipa mwenyewe asilimia kumi ya mapato yako, hapo ndio uanze kufikiria matumizi mengine jinsi ikupendezavyo.
 21. Kama unataka ukweli kuhusu kodi nenda kwa watu wa kodi, kama unataka ukweli kuhusu ng’ombe nenda kwa wafugaji wa ng’ombe, ukienda kwa watu tofauti itakugharimu sana muda na rasilimali nyingine kama fedha.
 22. Tamaa, hisia, uchoyo ni mambo ya kuyazuia sana katika safari ya kwenda kwenye mafanikio na utajiri.
 23. Endelea kufanyia kazi bajeti yako ili ikufae na ikusaidie katika safari yako ya mafanikio na utajiri.
 24. Bajeti yako inatakiwa ikusaidie kulinda fedha zako, mali zako na kukufanya uendelee kuwa tajiri, idhibiti na kuizingatia sana bajiti yako hasa ya matumizi.
 25. Hakikisha hekima na maarifa uliyojifunza katika kitabu hiki yanakusaidia, hasa katika kupata, na kulinda hazina na uwekezaji wako ili uwe salama.
 26. Tunatakiwa kuwa na uwezo wa kulipa madeni yetu kwa wakati, na pia kujizuia kununua kitu ambacho hutaweza kukilipia.
 27. Madeni ni mabaya yanaweza kukutenga na familia yako, marafiki na yanakufanya kuwa mtumwa. Mfano mzuri ni Dabasir wa Babiloni, aliyekuwa mtumwa na kufanya kazi za kutunza farasi kipindi kile.
 28. Unapolipa madeni ya watu kwa muda unaheshimika sana katika jamii, na pia utapata watu wazuri wa kushirikiana nao.
 29. Tunatakiwa kuwa na huruma kwa wote ambao hawakuweza kufanikiwa na kuwa matajiri kama sisi, tunatakiwa kuwa na kiasi katika jambo hili la huruma na misaada.
 30. Kila wakati tuanatakiwa kujiongeza na kujifunza zaidi ili tuongeze uwezo wetu wa kuzalisha na kupata utajiri zaidi.
 31. Unapojifunza na kujipatia hekima maarifa, ujuzi unaongeza nguvu ya ushawishi na kuheshimika na kukubalika katika jamii. Mfano, watu wa babiloni waliheshimika kwa hekima zao zilizowasaidia kuwa matajiri na kuwasaidia wengine pia.
 32. Bahati nzuri inamsubiri mtu ambaye yupo tayari kupokea fursa zinazojitokeza.
 33. Kinacho tufanya kushindwa kutumia fursa zinazojitokeza mbele yetu ni roho ya kughairisha mambo iliyopo ndani yetu inayotufanya kuiona hatupo tayari au tuna muda mwingi.
 34. Kama tunataka kuwa sehemu ya kuvuna utajiri na hazina kama ilivyokuwa Babiloni tunatakiwa kuifukuzia mbali roho ya kughairisha mambo isiwepo karibu na sisi kabisa.
 35. Hazina na uatajiri wa Babiloni unapatikana na kuwafikia wote ambao wameachana kabisa na roho ya kughairisha mambo. Usighairishe kabisa mambo muhimu kwenye maisha yako, yafanye kwa nguvu zako zote, hata kama unajisikia hovyo kiasi gani.
 36. Hatua unazochukua kila wakati ndio zitakufikisha kwenye mafanikio na sio matamanio uliyonayo, matamanio yaendanie na matendo.
 37. Dhahabu au fedha zimehifadhiwa kwa wote ambao wanazifahamu sharia na kanuni zake na kuzifuata.
 38. Epuka mihemuko na hisia za tamaa katika kutafuta utajiri, fuata kanuni na hekima za waliofanikiwa katika kutafuta utajiri utafika ukiwa imara na utajiri wako ukiwa salama.
 39. Fedha na dhahabu zitawapotea kwa haraka sana watu wasio na hekima, zitakimbilia kwa walio na hekima. Soma sharia saba za dhahabu zilizowasaidia wababiloni, zinaweza kutusaidia sisi pia.
 40. Kama unatamani kumsaidia rafiki yako msaidie kwa namna ambayo matatizo yake hayatakuwa mzigo kwako mwenyewe.
 41. Kama mtu ana roho ya utumwa, ataendelea na hiyo roho ya utumwa hata akiwa hayupo utumwani. Siku zote maji yanafuata mkondo wake.
 42. Madeni yanaweza kukufanya ukawa mtumwa bila wewe kujua.
 43. Mtu yeyote anayejali maisha yake na nafsi yake lazima atoke kwenye madeni, madeni yanakuondolea heshima na utulivu.
 44. Wafalme wakuu wanatumia nguvu kubwa na kila kitu walichonacho kupambana na maadui zao. Wewe adui yako ni madeni yako.
 45. Madni yatakufukuza mbali na uwapendao, mbali na mahali ulipopapenda, mbali na nchi yako, yatakufanya ujione mpweke. Mfano mzuri ni kama ilivyomtokea Dabasir wa Babiloni.
 46. Waliokukopesha sio maadui, unaowadai sio maadui, ni watu mlioaminiana na kupendana ndio maana mkakopeshana, madeni ndio maadui wenyewe. Ukitaka kurudi Babiloni nchi ya uhuru na utajiri lazima ulipe madeni yako yote.
 47. Dhamiria kulipa madeni yako ili urejeshe uhuru wako na furaha yako. Penye nia pana njia. Amua kwa dhati kupata uhuru wako wa kifedha, uhuru ni bora kuliko utumwa. Toka utumwani na urudi Babiloni nchi ya washindi na walio huru.
 48. Kama unadhamira ya kweli ya kurudi babiloni, jua kuwa elimu na mafunzo uliyopata kuhusu fedha na dhahabu umeyaelewa na kuyatekeleza.
 49. Simama tena, jisikie mtu huru, fanya na ishi kama mtu huru na aliyefanikiwa. Rudi tena Babiloni.
 50. My debts were my enemies, but the men I owed were my friends for they had trusted me and believed in me.

Many things do I enjoy but nothing takes the place of work.

Ahsanteni sana!


One response to “Uchambuzi Wa Kitabu Cha The Richest Man In Babylon”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X