Hii dhana ambayo kila kijana anapaswa kuachana nayo


Vijana tupambane, ifike hatua haya mabango yaondolewe mitaani kwetu.

Vijana wanapokuwa wanafikiria kuanzisha kitu, kitu Cha kwanza wanafikiria kupata mtaji au msaada. Nakumbuka wakati naanza chuo mwaka 2016 nilimwambia rafiki yang hivi, mpaka nahitimu chuo nataka niwe na uwezo wa kuajiri vijana kumi”. Yeye aliniambia “mpaka  nahitinu chuo nitakuwa nimetafuta na kupata wadhamini kumi” 

Sasa nadhani vijana tunapaswa kubadili fikra zetu.

Tubadili namna tunavyofikiri maana mitaji mingine tayari tunayo.
Una nguvu zako. ZITUMIE hizi kuchapa kazi
Una akili itumie kubuni vitu
Una kipaji, kitumie.
Una muda, utumie
Una ujuzi/elimu itumie pia.

Kwa vyovyote vile, usikubali kuendelea kubaki ulivyo. Nakubaliana na Martin Luther King Jr aliyesema kwamba, Kama huwezi kupaa, kimbia. Kama huwezi kukimbia tembea, Kama huwezi kutembea Basi tambaa Ila kwa vyovyote vile usikubali kubaki ulivyo. Pambana uwezo unao.

Tuachane na dhana ya kwamba Kuna mtu atasimamia na kufanya vitu kwa niaba yetu.
Maisha yako ni wajibu wako kijana. Ukiendeleza kusubiri misaada kutoka sijui wapi ili ufanikishe malengo yako. Utasubiri Sana.

Anza hata kidogo
Fanya Kitu
Wanaopata bahati Ni wale walio kwenye mwendo siyo wale wanaokaa vijiweni tu wakisubiri bahati.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X