Kitu Kimoja kinachokwamisha mafanikio ya watu wengi


Kuna watu huwa wanapokeaa mafunzo kutoka kwangu kwa njia ya barua pepe. Kila siku huwa nawatumia ujumbe mmoja ulioshiba.

Sasa juzi niliwatumia ujumbe mmoja kuhusu fursa. Kila aliyesoma huo ujumbe alionekana ameguswa na ule ujumbe kwa namna yake. Kitu ambacho kimenifanya nikae tena Leo kuandika ujumbe mwingine.

Leo nitakushirikisha ule ujumbe niliowatumia, lakini kwanza nataka nikwambie Hivi. Kinachoua mafanikio ya watu wengi ni kupenda kufanikiwa kwa haraka.

Inakuwa Hivi, mtu anapambana kwa NGUVU zake zote. Anapata pesa na anaanza kuonja mafanikio.
Sasa kwa kuliona Hilo anaamua kujitanua zaidi na zaidi ili afanikiwe haraka zaidi.

Tamaa ya kufanikiwa haraka zaidi inampelekea kwenye kuwekeza fedha zake hata kwenye vitu ambavyo hajui na baadaye anapoteza fedha zake.

Kwenye kipindi hiki ambacho kimekuwa naandaa semina ya uwekezaji kwenye HISA, nimeongea na watu mbalimbali. Na hiki kitu nimegundua kinajirudia kwa watu wengi.

Habari za akina Mr. Kuku, au habari za kikoba Cha mtandaoni, au habari rusha laki moja, tukurushie laki mbili ndani ya siku tatu.

Rafiki yangu ninachotaka ufahamu Ni Kuwa fursa zipo nyingi. Na siyo kila fursa inakufaa wewe. Fursa nyingine, waachie wengine.

Wewe komaa vizuri na eneo ulilopo, ukweli ni Kuwa litakutoa.
Maana kila sekta imetoa watu WALIOFANIKIWA.
Kuna watu wanauza magodoro Kama wewe, wameweza kutoka kwa Hilo tu.
Wengine wametoka kwa kilimo
Wengine wametoka kwa kuuza nguo
Wengine wametoka kupitia mitandao
Wengine ualimu n.k.

SEKTA yoyote Ile uliyopo Sasa Hivi, Ina uwezo mkubwa sana wa kukuinua na kukufanyia Kuwa mkubwa zaidi.

Kikubwa endelea kufuatilia ili uijue zaidi.
Endelea Kuwa Bora kwenye sekta yako.
Tafuta masoko na uuze zaidi bidhaa yako
Mafanikio yatakufuata tu.

Baada ya Kuwa nimesema hayo, naomba Sasa nikushirikishe ujumbe niliowashirikisha watu kwenye baruapepe zao juzi. Naamimi utaupenda.
Kitu muhimu Cha kufahamu ni kuwa, ujumbe huu sijauandika mimi 👇🏿

Ukipata nafasi ya kufika kule Mbozi, Mbeya ukakutana na habari za watu wanaotajirika kutokana na kilimo cha kahawa, kwa kweli unaweza kuwehuka, na kujiona kama mtu uliyechelewa kweli kweli.

Wakati unarudi, kama ukishuka Mafinga, Njombe na kufuatilia stori na kutazama mamilionea walioupata umilionea kutokana na biashara ya miti na mbao, unaweza kudhani kwamba hapa duniani fursa inayowatoa watu kiuharaka ni mbao pekee!

Pitia maeneo ya Ruaha Mbuyuni, Iringa kutana na wakulima wa nyanya na vitunguu wakikuonesha coaster walizonunua kwa kilimo cha msimu mmoja pekee. Aisee kama una akiba utanunua shamba muda huo huo na kuachana na ajira kama ulikuwa mwajiriwa.

Ukitoka pale ukaenda mpaka Mang’ula na Ifakara Morogoro, ukakutana na habari za watu wanavyopiga hela kwenye mpunga, kichwa chako kinaweza kuwaka moto. Unaweza kujizaba vibao na kujimaindi, afu utajiuliza, “Nilikua wapi siku, zote hizi?”

Ukitoka kule jisogeze mdogo mdogo hadi Kariakoo, Dsm kisha kutana na wafanyabiashara wa maduka pale ambao wana gepu la kufuata bidhaa kule China, Uingereza na Dubai. Utapigwa na butwaa utakapoona watu wakiongelea milioni mia tatu, milioni mia saba, bilioni mbili kama vile wanaongelea elfu kumi kumi. Usipokua na utulivu unaweza kuamini kwamba biashara zinazolipa ni maduka na unaweza kuanza kufight kupata fremu pale!

Usiende kwanza Zanzibar, bali chukua hata bus au Fastjet uende chapchap kule Arusha. Hapo kutana na stori za mabilionea wa madini wanaotikisa jiji. Ukisimuliwa ABC za madini na namna ya kucheza nayo, unaweza kuacha kila kitu na kuanza kuhangaika na biashara ya madini. Hapo sijakutajia jeuri utakayoiona kwa watu wanaofanya biashara ya utalii. Nakwambia hela ulizozisikia Kariakoo utaziona ni cha mtoto sana!

Unapoendelea kutafakari, rudi mtandaoni. Kama ukibahatika kukutana na watu wanaoitwa Network Marketing utakoma kuchagua. Wakikuelezea stori zao, wakikusimulia walivyonunua mavouge yao, wakikuonesha picha zao walizokua wanakula bata Dubai, Paris, Madagascar na Uamerikani, nakwambia korosho utaziona takataka.

Mbao utazihesabu kama biashara ya utumwa, maduka ya Kariakoo utayaona kama michosho na mipunga ya Ifakara utaiona kama madudu flani ya walugaluga waliochelewa! Sasa mara kumi hata ya Network Marketing wa bidhaa, usiombe ukutane na fursa ya digital currency, hakika nakwambia utatembea kifua mbele ukiamini kutajirika ni ishu ya kufumba na kufumbua.

Hapo sijaamua kusafiri na wewe kwenda kwa wale tunaokinadi kilimo kama dhahabu inayoelea. Ukisikiliza wafuasi wa kilimo, ukasikiliza hesabu wanazokupatia unaweza kusema wanaohangaika na madini wanapoteza muda! Ngoja niuchune kukupeleka kwenye fursa ya samaki kuzitoa Mwanza kupeleka Congo, ngoja nisikurushe roho na habari ya korosho, ngoja nikaushie habari ya ufuta!

KUNA MAMBO MATANO YA KUFAHAMU:-*

  1. Usipokua na utulivu wa fikra, hizi habari za fursa za biashara na ujasiriamali zinaweza kugeuka kuwa kama miluzi mingi, na itakupoteza.
  2. Mtu yeyote asikudanganye ya kwamba kuna biashara bora kuliko nyingine. Kila biashara, fursa unayoiona huku duniani inao uwezo wa kutengeneza matajiri. Kuna matajiri kutokana na kumiliki shule, wengine kwa kumiliki mabasi, wengine kwa kuwa na vituo vya mafuta, wengine kwa kilimo, wengine kwa udalali n.k. Usisahau kuwa biashara inayomtajirisha mmoja, mwingine akiingia ndio inaweza kumfilisi na kumpoteza kabisa! Kawaulize waliolizwa kwenye kilimo, watakusimulia.
  3. Mtu yeyote asikuchanganye na miluzi yake hata ukaamini kwamba kuna fursa inayoweza kumfaa kila mtu. Sio kila fursa inayompa faida John inaweza kukupa faida wewe Ashura. Ukifuatilia kwa umakini utabaini kwamba mafanikio hayakai katika uzuri wa fursa, bali yanatokana na mchukua fursa. Mwingine anaweza kujifunza na kumudu kuifanya network

marketing, lakini mwingine nature ya network marketing haimfai, isipokua akienda kule Mafinga akazamia kwenye mbao, mwaka mmoja mbali unaona ana Semitrela zake mbili na mambo yanaenda.

Kuna watu wanapotea kiuchumi kwa kung’ang’ana na fursa kwa kukariri. Kisa kuna mtu alinunua Range Rover katika network marketing na wewe unaendelea kukomaa, mwaka wa tano sasa hata bodaboda huna, kumbe ungeenda zako Mbozi kwenye Kahawa sasa hivi usikute na nyumba ungekua umejenga. Kisa wanaoenda China wanatoka na wewe unahangaika na biashara za maduka, mwaka wa ishirini bado hakujasomeka na kumbe ungeenda zako kwenye madini huko Mererani muda huu ungekua umeshanunua helkopta yako!

  1. Ni kweli kwamba inatakiwa tujifunze fursa mbalimbali, lakini ifike sehemu mtu uchague kukomaa na fursa fulani pasipo kurukaruka. Utajiri hauji kwa mtu kuwa bize na kila fursa inayoingia, bali unakuja kwa kujifunza fursa nyingi na ku-stick na eneo moja, ama maeneo machache ambayo, utajitambulisha nayo na watu watakutambua. Na ukishakua katika kukomaa na maeneo yako (fursa ulizoamua kukomaa nazo), usianze tena kuyumbayumba na kutamani ya wengine.
  2. Lazima ifike mahali utambue kwamba kila mtu anahitaji fedha za kutosha lakini hatuhitaji kiwango sawa cha fedha kwa sababu makusudi na malengo yetu hayafanani. Nikisema hivi, sikushauri uhangaike na fursa kwa motive ya hela pekee, bali ufanye vitu kama sehemu ya kuufurahia mchakato wa kazi, na fedha ziwe ni matokeo na sio lengo namba moja

Fursa zipo nyingi kuwa makini katika maamuzi.

Wewe umejifunza nini kutokana na ujumbe huu

Ebu weka maoni yako hapa chini

je, ma wewe ungependa kupokea mafunzo kwa mfumo wa baruapepe?

jaza taarifa zako hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X