Mfuatilie huyu jamaa kwa mwezi mmoja tu, wewe mwenyewe utaniambia utakachoona


Tunaishi katika dunia ambapo watu wanapenda kufuatilia sana maisha ya watu wengine. MTU anaweza kushinda mtandaoni akifuatilia maisha ya watu mbalimbali
Wasanii
Wachumba fulani
Wachungaji n.k.

Ila Kuna jamaa mmoja ambaye umekuwa unasahau kufuatilia. Na jamaa huyu siyo mwingine bali ni wewe mwenyewe.

Rafiki yangu, kwa kitu chochote kile unachofanya. Penda Sana kujifuatilia wewe mwenyewe zaidi ya unavyofiatilia maisha ya watu wengine.

Jijue maisha yako kwa uzuri.
Jua wapi unapotezea muda wako mwingi zaidi ili uweze kuwekeza muda huo kwenye vitu vya maana.
Jua ujuzi gani hauna sasa hivi, ili uanze kuujenga.
Jua  konekisheni ambazo hauna ili uanze kuzijenga.
Jua afya yako ikoje, ili uiboreshe.
Jua maarifa unayohitaji sana sasa hivi, ili uweze kuyajenga.
Jua changamoto zinazokukabili ili uweze kuzitatua.
Jua ulivyofanya vizuri leo ili uweze kujipongeza
Jua ulipokosea leo ili uweze kujirekebisha.

Ukifuatilia maisha yako na kujiwekeaa nadhiri ya kuyaboresha maisha yako kila siku. Basi ni wazi kuwa baada ya muda maisha yako yatakuwa yanazidi kuboresheka na kuwa bora zaidi na zaidi.

Rafiki yangu, jitahidi sana kufuatilia maisha yako na ili uweze kuyaboresha na Kuyafanya kuwa bora zaidi.


One response to “Mfuatilie huyu jamaa kwa mwezi mmoja tu, wewe mwenyewe utaniambia utakachoona”

  1. Ujumbe wa leo umenigusa na nimesoma hadi nikajishangaa kumbe nahitaji kujifuatilia sana nikakumbuka maneno ya kitabu chako cha cha vitu vidogo kuna sehemu inaongelea tabia kile kitabu kinanifaa sana na kinafundisha kweli jitihada zako ulizoweka katika kitabu kile sijutii kukinunua kinahamasisha kusoma hata wewe ni mvivu kusoma kitabu unatamani tu ukimalize chote na kukirudia

    Barikiwa sana kwa kazi nzuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X