Kuna ndugu mmoja alianzisha biashara huku akitegemea kwamba watu wangemiminika kwenye biashara yake siku ya kwanza. Ila watu hawakumiminika kama alivyokuwa anatarajia. Siku ya kwanza alitokea mtu mmoja wa kuuliza kuhusiana na biashara yake na kile ambacho anafanya. siku ya pili watu kadha wa kadha pia walipitia na kuangalia kuuliza uliza ila hawakununua.
Siku ya tatu ndipo alikuja kufanya mauzo ya kwanza.
Kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusoge ambele ndivyo watu walikuwa wanazidi kuongezeka kwenye kununua kwake.
Kumbe siyo kwamba kila ukianzisha kitu watu watamiminika kwako na kujipanga ili wapate kitu chako. Hapana, itachukua muda, maana kadiri watu watakavyokuwa wakiona ukiendelea kufanya hicho kitu ndivyo ambavyo hao watu watakuwa wakivutiwa kuja kwako.
Ukimhudumia vizuri yule mteja wako wa kwanza, atarudi kwako tena siku nyingine. nap engine hatarudi peke yake. Bali atarudi pamoja na rafiki zake na hivyo kuongeza idadi ya watu ambao wanapata huduma kwako.
Usidharau hizi hatua ndogo ndogo unazopiga. Na usiwe na haraka. Vumilia pale unapokuwa hupati matokeo makubwa mwanzoni huku ukiendelea kuweka juhudi zaidi ili uweze kufikia mafanikio unayoyataka.
Kila la kheri