Kama umezungukwa na watu ambao wanafanya vitu ndivyo sivyo. Usikubali kuachana na tabia yako nzuri na kuanza kufanya vitu ambavyo havieleweki. Mara zote na sehemu zote hakikisha kwamba unafanya mazuri hata kama umezungukwa na watu ambao wanafanya vitu vibaya..
Usikubali kuwa sehemu ya kuendeleza ubaya. Badala yake sambaza upendo wa kufanya mazuri.
Unaweza usione matokeo ya kile unachofanya kwa muda mfupi. Ila uhakika ni kwamba baada ya muda matokeo hayo unaenda kuyaona.
Kwa hiyo endelea kuonesha wema wako.
Asili huwa huwa haisahau. Siyo kwamba utafanya mazuri na yatasahaulika. Hapana, hayo mazuri kuna watu wanaona hata kama watakuwa ni wachache. Na hata kama wengine watajidai kama hawaoni, ila watakuwa wanaona.
Kuna siku utapata matokeo ya mbegu zako hizi za wema unazopanda.