Vitu Vitano Unavyopaswa Kutembea Navyo Kila Mahali


Ni vitu gani huwa unaambatana Navyo kila mahali unapoenda. Je, ni simu, kitabu au Nini? Leo hii ninakuletea orodha ya vitu Vitano Unavyopaswa kuambatana Navyo kila mahali na ubora Ni kuwa havina gharama ya ziada kuvifanya

Kujiamini. Jiamini kwenye kila kitu unachofanya. Kama unafanya kitu ambacho hakikufanyi ujiamini, basi hapo kuna mawili.
Achana nacho usikifanye kabisa ili uweze kufanya kitu kingine kitakachokufanya ujiamini. Au Anza kujiamini kuanzia leo hii.

Upendo wa Kazi.

Rafiki yangu, tembea na upendo wa Kazi kila mahali. Yaani, kazi unayoifanya ifanye kwa moyo wako wote bila kijibakiza.
Kama huwezi Kuwa na upendo kwenye Kazi yako unayofanya sasa hivi una machaguo mawili moja Ni kuachana nayo na usiifanye kabisa ili uweze kutafuta kitu ambacho unakipenda au chagua kitu ambacho unakipenda na ufanye hicho.

Tabasamu
Haikugharinu kitu chochote kutabasamu popote pale utakapokuwa. Kama kuna kitu ambacho unapaswa kukifanya kila marra Basi Ni kutabasamu
Anza leo hii

Kuwaacha wengine zaidi ya ulivyowakuta

Jitahidi sana kila mara Unapokutana na mtu kuhakikisha kwamba unamwongezea kitu cha ziada
Kwenye mazingira yetu tumezungukwa na wakatisha tamaa wengi. Watu ambao wanarudisha maisha ya watu nyuma zaidi.

Sasa unaonaje na wewe badala ya Kuwa mkatisha tamaa, ukiwa MTU wa kuwapa watu matumaini. Mara zote watie watu moyo na ONGEA maneno ya kuwainua ili waweze kufanya kazi na shughuli zao kwa ubora ZAIDI ya wanavyofanya.

Kama hujapenda kitu badala ya kumkatisha tamaa anayekifanya, toa mbinu ya kukiboresha. Ila siyo kuishia tu kulalamika.

Kila mtu anaweweza kulalamika. Kulalamika siyo Bei kubwa, ndiyo maana kila mtu anaweza kufanya hivyo, wewe jitofautishe kwa kuachana na kulalamika.

Maneno yako.
Mara zote tembea na maneno chanya. ONGEA kile unachomaanisha. Maneno yanaumba. Usijitamkie maneno mabaya na Wala usiseme maneno mabaya kwa wenzako. Weka nuvu kubwa kwenye kusema maneno chanya na kuwahamisha watu wengine ili waweze kufanya kile wanavyofanya kwa ubora ZAIDI.

Tunahitaji tutengeneze dunia ya tofauti na hii dunia hatuwezi kuitengeneza kwa Kuwa na watu ambao wanalalamikia kila kitu.

Hivyo, Ni vitu Vitano ambavyo unapaswa kutembea mavyo kila mahali na kila siku.

Kila la KHERI.

Umekuwa nami,

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X