Vitu vitano vya kujiepusha navyo ili ufike mbali


1. Jiepushe na vileo
Hivi vitachukua muda wako mwingina fedha lakini havitakufanya upige hatua yoyote kubwa kimaisha.

2. Jiepushe  Kuwa bize na kila kitu.
Yaani, hiki unafanya. Kile unafanya. Unapambana na kila kitu. Hapana, sililiza rafiki yangu, wekeza nguvu yako kwenye vitu vichache ambavyo unaweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kisha vifanye kwa ubora wa hali ya juu. Ikiwezekana fanya hata kitu Kimoja na ujulikame kwa hicho.

Kuna usemi wa kiingereza unaosema kuwa the jack of all trades is a master for none.
Wekeza nguvu zako kwenye vitu vichache na uvifanye vizuri, Tena ikiwezekana kitu kimoja tu.
Kwa mfano, ukisikia majina kama Mbwana Samatta unajua wazi kuwa Huyu ni MTU wa mpira.
Ukisikia Diamond, unajua kabisa kuwa konachoongelewa ni muziki.
Wewe pia weka nguvu zako sehemu ambapo utafahamika. Eneo moja ambalo utabobea na kulielewa vizuri.

3. Jiepushe kujua kila kitu
Ugonjwa unaoua watu wengi hapa duniani ni ugonjwa wa kujua kila kitu.
Jitahidi sana kujiepusha na ugonjwa huu. Kuwa mtu wa kujifunza kila mara.

Kadiri unavyojifunza kila mara Ndivyo unavyoweza kuelewa mambo mengi ambayo hapo awali ulikuwa huelewi.

Ila usipokuwa MTU wa kujifunza, unakuwa unatimiza ule usemi wa kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.

4. Epuka kuishi maisha bila mpango. Maisha bila mpango siyo maisha mazuri unayopaswa kuishi. Jitahidi mara zote kuwa na mpango malengo ambayo unayafanyia kazi.

Usipokuwa na malengo, daah rafiki yangu. Utajiona kama vile unapiga hatua wakati hakuna hatua yoyote kubwa unayopiga. Malengo, yanakuweka kwenye njia.
Malengo mara zote yanakukumbusha kuwa bado hujafika. Hivyo, weka juhudi zaidi ili uweze kufika. Malengo yanakwambia kuwa endelea kupambana na KUWEKA juhudi zaidi.
Malengo yanakupa motisha.
Penda mara zote kuweka malengo makubwa, kuyafanyia kazi na ukishayafikia weka malengo makubwa zaidi Kisha yafanyie kazi.

5. Epuka kuishi maisha ya kujilinganishana watu wengine
Mara zote jitahidi uweze kuishi maisha yako kama maisha yako bila ya kujilinganisha na watu wengine.
MTU pekee unayopaswa kujilinganisha naye Ni wewe wa jana.
Na wewe mwaka Jana.

Jiulize hivi nikijilinganisha na jana, je, leo niko bora zaidi ya jana.
Ukigundua kuwa leo hii upo bora zaidi ya jana. Basi weka nguvu zaidi kwenye kufanyia malengo ili uzidi kuwa bora zaidi.
Ukigundua Leo uneyumba na kurudi nyuma, Basi weka nguvu zaidi ili uweze kuwa Bora.

Ni hivyo tu.

Makala hii imeandaliwa na rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


One response to “Vitu vitano vya kujiepusha navyo ili ufike mbali”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X