Ukiongea na watu kuhusu Kipaji utasikia watu wanakwambia
Kipaji hakilipi bongo
Tafuta ajira maana kipaji hakina kitu chochote
Ngoja nisome kwanza, Mambo ya kipaji yatafuata baadaye.
Inaonekana dhana ya kipaji umekuwa haifahamiki kwa watu wengi.
Ndio maana kitabu hiki kimekuja ili kukuelewesha kuhusu Kipaji Chako na namna ambavyo unaweza kukutumia kipaji chako kwa manufaa.
Kwenye kurasa za kitabu hiki nimeeleza kipaji kwa kina kiasi kwamba kama kitabu hiki anakisoma mtoto wa miaka sita aweze kunielewa.
Kwenye sura ya kwanza nimeanza kwa kueleza kwamba kipaji ni kitu gani? Ambapo nimeeleza dhana nzima ya kipaji na jinsi kinavyofanya kazi.
Kwenye sura ya pili nimeeleza namna ambavyo unaweza kugundua kipaji chako.
Je, unajiuliza ni kwa namna gani ambavyo unaweza kugundua hicho kipaji chako? Basi nenda moja kwa moja kwenye sura ya pili.
Kwenye sura ya tatu nimeonesha mbinu unazoweza kutumia kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako. Hapa utakutana na mbinu za kukusaidia wewe kuweza kupeleka kipaji chako mbali. Na kwenye sura ya nne tutaona kwa nini watu hawathamini vipaji vyao.
Kwenye sura ya tano tutaona mbinu zitakusaidia wewe kutengeneza fedha kwa kutumia kipaji chako.
Tunaishi kwenye ulimwengu wa intaneti. Na hapa tutaingia kwenye sura ya sita ambapo tutaona namna ambavyo unaweza kupeleka kipaji chako kwenye mtandao na kunufaika na intaneti.
Kwenye sura ya saba tutaona kipaji na elimu. Kwa nini elimu inapewa kipaumbele zaidi kuliko kipaji na je, kuna ulazima wowote wa kuendeleza kipaji chako au ukomae tu na elimu?
Uko tayari kwa ajili ya safari hii ya kipekee? Basi wacha tuianze kama ifuatavyo.
Gharama ya kitabu hiki Ni 10,000/-
Ila tuna ofa ya NANENANE.
Utakipata kitabu hiki kwa ofa ya elfu tano tu.
KARIBU SANA.