Kitu ambacho kitakufanya uweze kulipwa zaidi ya unavyolipwa sasa


Watu huwa wanatafuta siri za mafanikio na kuwafikisha mbali. Kama Kuna Siri ya mafanikio ambayo Unapaswa kuifahamu ambayo itakuwezesha kuongeza kipato Chako zaidi ni kufanya kazi zaidi ya vile unavyolipwa.

Yaani, kujituma zaidi na kuchapa kazi zaidi ya ambavyo unalipwa. Hiki kitu kitakufanya uweze kulipwa zaidi.

Kwa sababu kama MTU akikupa kazi yake na ukaifanya kwa viwango vikubwa Kuliko alivyokuwa anatarajia tangu Mwanzo. Ni wazi kuwa Huyu MTU hawezi kukusahau.

Lakini pia huyu MTU atakuletea watu wengine zaidi.

Ebu tuchukulie mfano wa kawaida labda wewe Ni fundi cherehani. Mtu amekuja kwako na kitambaa anataka suti. Ukamtengenezea suti nzuri sana kwa viwango vya juu Kuliko hata alivyotazaamia.
Unadhani zamu ijayo akitaka kutengeneza suti atamtafuta nani? Au unadhani rafiki yake akitaka kutengeneza suti atamwelekeza kwa nani?

Jibu lipo wazi kabisa… yeye atakuja kwako na rafiki yako atamwelekeza kwako.

Hiki kitu ukiendelea kukifanya kwa muda mrefu. Utaweza kupongeza kipato Chako Mara dufu mpaka Mara Kumi zaidi.

Wakati wengine watakuwa wanalia kuwa hawana kazi za kufanya wewe utakuwa nazo za kutosha.

Anza kufanya kazi zaidi ya unavyolipwa. Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X