Leo nimekumbuka moja ya usemi muhimu sana. Usemi huu ni kuwa huwezi kula kabla ya kulipa gharama.
Eneo pekee unapoweza kula na kunywa bila kulipa gharama ni mgahawani. Hapa unaweza kuagiza chochote unachotaka, ukala na kushiba na kisha ukalipia.
Ila kwenye maisha ya kawaida, ukitaka kula vinono sharti ukubali kuvigharamikia.
Kuthibitisha hili wahenga wetu waliweka wazi hili waliposema kuwa unavuna kile ulichopanda.
Ukienda shambani kuvuna wakati hukupanda ujue huo utakuwa wizi.
Ninachotaka kukwambia siku ya leo ni kuwa, unapokuwa unafikiria kuvuna. Jiulize je, umepanda mbegu za kile unachotaka kuvuna?
Unataka maisha mazuri ni kweli umepanda mbegu za hayo maisha mazuri?
Hii ndio kusema kuwa Kama Kuna aina fulani ya maisha unatamami kuwa nayo, Basi kuwa tayari kuyatengeneza kwanza.
Mara zote na sehemu zote huwa unavuna ulichopanda.