Ni marufuku kwako kutumia hii kauli kuanzia leo hii


Moja ya kauli ambayo watu wamekuwa wanapenda kutumia ni kauli ya ninapoteza muda. Mtu anapotumia kauli hii maana yake hana kitu chochote cha maana cha kufanya kwa sasa, hivyo, kitu pekee anachoweza kufanya ni kupoteza muda.

Hivi kweli rafiki yangu, unaweza kukosa kitu cha maana cha kutumia kwenye muda wako. Kuanzia leo hii nataka kabisa uachane na dhana ya kuwa unapoteza muda. Ukijikuta upo kwenye hali ya kupoteza tu muda ili saa zisogee, basi jiulize ni kitu gani cha maana ambacho unaweza kufanya

Au jiulize ni uzalishaji  gani ambao unaweza kuutumia ndani ya huo muda wako. Rafiki yangu, kwa vyovyote vile usikubali kuwa mmoja wa watu ambao wanapoteza muda.

Muda ni mali, sasa kwa nini ukubali kupoteza mali. Utumie muda wako kwa manufaa kuanzia leo hii. kama huoni kitu gani ambacho unaweza kufanya na muda wako, basi chukua kitabu usome. Tena unaweza kuanza kwa kusoma hata kitabu cha bure ambacho huwa natoa hapa jukwaani. Kukipata nitumie ujumbe wenye baruapepe yako kwa whatsap namba 0755848391. Name nitaktuma kwako bila kuchelewa.

Kwa vyovyote vile rafiki yangu, usikubali kabisa kuwa unapoteza muda kwenye maisha yako. Muda ni mali, ujali na utumie vizuri sana. Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X