Njia nzuri ya kuwaambia watu wakulipe katika kipindi hiki ambacho gharama za miamala zimeongezeka


Nakumbuka mwaka juzi baada ya kuwewa kwa tozo za miamala kwa njia ya simu niliandika makala moja ndefu sana kuhusiana na namna ambavyo tungeweza kukabialiana na hiyo hali kwa ustadi zaidi.  Utakumbuka kwenye hiyo makala nilieleza wazi kuwa moja ya eneo ambalo tunapaswa kulitumia vizuri kwenye kuweka akiba katika kipindi hicho ambacho miamala ya simu ilikuwa imeongezewa tozo ilikuwa ni benki. Sasa hivi ninapoandika hapa, benki nako kuna makato, sasa swali ni je, wapi tena tuweke  fedha yetu. Malipo yetu yafanyikeje katika kipindi hiki.

Kabla sijaandika sana kabisa, ningependa kusisitiza jambo moja tu. Ni ukweli kutuma au kupokea fedha kwa njia ya benki au simu hakutakwepeka kwa asilimia 100. Na njia ambayo ninakuelekeza leo, inafanya kazi sanasana  kama mtu anakutumia hela na wewe huna shida nayo ya haraka. Ila kama fedha hiyo unaihitji kuitumia leo au kesho, basi njia hii haitakufaa kiviile, katika mazingira kama hayo, benki au miamala ya simu ndiyo utalazimika kutumia. Ila siyo vibaya ukiifahamu hii njia, ninaamini muamala mmoja mmoja unaweza kuamua kuwa utumwe huku.

Na njia hii ninayoiongelea ni mtu kukuwekea fedha zako kwenye akautni za uwekezaji za UTT

Kwa yule ambaye hajui UTT AMIS ni taasisi ya kiserikali iliyo chini ya wizara ya fedha.Kazi kubwa ya taasisi hii ni kukusanya fedha za watu wenye mitaji midogo na mikubwa, kisha kuwekeza fedha hizi kwa niaba ya hao watu.

Faida yote inayopatikana kwenye uwekezaji huu, inakuwa ni faida ya wawekezaji husika.

Katika hali ya tozo ambayo tunapitia kwa sasa, tumefikia hatua ambapo mtu utahitaji kuwekeka fedha zako huku. Kwa nini

Kwanza kama mtu anakuwekea fedha huku makato ni madogo wakati anakuwekea, makato ni ya mtandao wa simu husika na wala hata hakuna tozo za serikali.

Pili ni kuwa fedha yako ikikaa huku inapata ongezeko la thamani. Ikumbukwe kuwa fedha yako unayopaswa kuiweka huku ni ile fedha ambayo huihitaji kwa haraka. Kwa hiyo, kama ambavyo huwa tunawaambia watu watuwekee fedha benki, tunaweza kuwaambia pia watu watuwekee fedha kwenye akaunti zetu za  UTT na fedha zetu zikakaa huko.

Lakini pia ni sehemu salama. Kama nilivyokudokeza hapo mwanzo UTTAMIS ni ni taasisi ya kiserikali iliyochini ya wizara ya fedha. Hivyo, usalama wa fedha yako ni mkubwa sana

Ni sehemu ambayo inakuwezesha kuweka kiwago cha chini kuanzia elfu tano. Hii inategemea na aina ya mfuko ambao unakuwa umechagua, ila kwa aina nyingi ya mifuko ya UTT unaweza kuweka akiba kwa kiwango cha chini cha elfu tano tu

Ni akaunti pekee ambayo ukitaka kuangalia salio haukatwi. Utt wana mfumo wao wa kukusaidia wewe kuangalia salio ambapo ukitaka kuangalia salio unatuma ujumbe kwenda uwekezaji@utt.co.tz bila gharama yoyote ile na unaambiwa taarifa zako za uwekezaji bila kukatwa gharama yoyote ile

Kwa hiyo rafiki yangu, kama kuna malipo ambayo unapaswa kulipwa ila fedha yake huihitaji kwa haraka, basi waambie watu wakulipe kupitia UTT.

@songambele


2 responses to “Njia nzuri ya kuwaambia watu wakulipe katika kipindi hiki ambacho gharama za miamala zimeongezeka”

  1. UTT Amis ipo poa sana,na ukiwa unaweka hiyo fedha kwa kupitia wakala wa CRDB bank hakuna makato mfano unaweka sh.100,000 haikatwi unaikuta ileile uliyotaka kuweka n nzuri sana kupitia wakala,japo mawakala mpaka uwaeleweshe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X