Umefanya uamuzi uliobora sana


Habari ya leo

Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
Ninajua kwamba umeomba kupata KITABU CHA BURE . lakini pia nimeona siyo vibaya ukijua mimi ni nani na kitu gani utegemee kupata kwangu na SONGAMBELE kiujumla.

Bila kuongeza la ziada napenda kukutaarifu kuwa kitabu chako kimeshatumwa kwenye baruapepe yako, ila kama hukioni unaweza kukipakua kwa KUBONYEZA HAPA

Kwa miaka zaidi ya mitano sasa nimekuwa nikiandika kwenye blogu hii ya SONGA MBELE. Kwenye blog hii nimekuwa nikiandika makala mbalimbali kuhusu biashara, ndoto zako na malengo yako na jinsi ambavyo unaweza kuyafikia.

Lakini zadi ya hapo, nimewasaidia watu kama wewe kuweka malengo, kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza. Wengine bado ninaendelea nao mpaka leo hii.

Hiki kitu ndicho ningependa nifanye kwako pia

Kila mara nitakuwa nakutumia jumbe fupi na makala zenye kukuelimisha na zitakazokusaidia wewe kuweza kupiga hatua na kufika mbali zaidi kwenye baruapepe yako. Nitafanya hivyo aidha kupitia kwenye makala, video na mafunzo ya sauti.
Lengo ni kukusaidia wewe kufikia malengo yako haraka iwezekavyo.
Na hilo litawezekana kama wewe utaendelea kuwa na mimi
Kiufupi, ukikaa pamoja nami

 • utajifunza namna ambavyo unaweza kuweka malengo.
 •  kuyafanyia kazi mpaka kuyatimiza kwa kutumia mbinu ambazo mimi na wengine wengi tumetumia kwa manufaa
 • Pia utajifunza namna ya kuanzisha na kukuza biashara yako
 • Bila kusahau kipaji chako

Baada ya kusema hayo, naomba ubonyeze hapa kupakua kitabu chako cha BURE

Kitabu hiki kitakusaidia wewe; kuanza kusoma vitabu. kitu ambacho ni muhimu sana hasa kama unataka kufikia malengo yako.
Vitabu vina mchango mkubwa kwa mtu ambaye anataka kufanya  makubwa na kuufikia ukuu.
Na ndio maana kwenye safari yetu tunaanza kwa kukuonesha MAAJABU KUSOMA VITABU.
Na bado nina vitu vingi vya bure vya kukusaidia wewe kufanyia kazi malengo mpaka ukayafikia.

Kitu unachopaswa kufanya wewe ni kuhakikisha kila mara unatembelea barua pepe yako ili kupata mafunzo zaidi lakini pia kutembelea blogu ya SONGAMBELE. kila mara maana hapa naandika makala mbili mpya kila siku

Tutaongea
Ni mimi Godius Rweyongeza (Songambele).
SONGAMBELE

NB: Kama umepokea kitabu hiki cha zawadi. Naomba unitumie ujumbe kwa barua pepe yangu ya godiusrweyongeza1@gmail.com kuniambia umekipokea.
Nitafurahi sana kuona ujumbe wako. na nitaweza kuujibu ujumbe wako punde tu baada ya kuupokea. Huwa najibu jumbe zote ambazo zinatumwa kwangu.


15 responses to “Umefanya uamuzi uliobora sana”

 1. This is real way to help us bcz my self am always like to read in my phone rather than book..so may GOD bless

 2. Nimefurahi Sana asubuhi ya Leo. Nimechukua simu yangu tu nikiwa kitandani na baada ya kufungua WhatsApp yangu nimepata ujumbe kutoka kwako. Mara hiyo hiyo nikapata zawadi. Nashukuru muumba Kwa ILO.

  • Waoh, karibu sana. Hongera Sana kwa kupata kitabu hiki Cha kipekee nakutakia usomaji mwema.

   Usisite kunipa mrejesho baada ya kukisoma.

   Halafu pia vitabu vingine vizuri Kama hicho vipo. Karibu sana

 3. Leo tarehe 14/2 n cku ya kuoneha upendo skutegemea kupata zawad asante bro nmepata zawad kutoka kwako Mungu akubariki unapotu elimisha🙏🙏

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X