Mara kwa mara nimekuwa nakutana na watu wazima wenye umri wa miaka 50 na zaidi au niseme watu walio kwenye umri wa miaka ya kustaafu, kila ambapo nimekuwa nikiongea na watu hawa kuhusiana na vipaji basi wenyewe moja kwa moja wamekuwa wakiniambia kuwa umri wao umeshaenda, hivyo kwao huu sio muda tena wa wao kunoa au kuendeleza vipaji.
Kitu kimoja ambacho nimekuwa nikiongea nao ni kuwa wao wanaweza kuwa sehemu ya kuwasaidia kizazi kijacho (, watoto wao, wajukuu wao na vijana wengine) kugundua vipaji vyao, kuvinoa na kuviendeleza. Hiki ni kitu ambacho naamini kinawezekana kabisa kufanyika na mzee yeyote yule anaweza kusaidia kutengeneza taifa bora kwa siku za mbeleni.
Jack Ma aliwahi kusema kwamba unapofikisha umri wa miaka 60 na zaidi ni muda wa wewe kuhakikisha unaandaa kizazi kjacho. Nadhani, wazee wote ambao wanasema kwamba kwa sasa hawawezi kugundua wala kuendeleza vipaji vyao, basi walau hata hawawezi kushindwa kushiriki kwenye kuandaa kiazazi kijacho.
Tukiwa na kizazi kizuri kinachojitambua, kizazi ambacho kila kijana anajua uwezo wake na kwa nini yuko hapa duniani. Kizazi ambacho kila kijana anatumia uwezo alio nao ndani yake, ni wazi kuwa tutatengeneza taifa zuri na bora sana kuwahi kutengeneza hapa duniani.
Na hiki ni kitu ambacho tunapaswa kupigania.
Kama wewe una watoto au wajukuu ambao unakaa nao, kwa nini usitoe sehemu ya muda wako katika kufuatilia na kuangalia uwezo wao walio nao na huku ukiwasaidia kuutumia huo uwezo kwa manufaa ya sasa hivi na siku zijazo.
Wewe una uwezo mkubwa sana
Kuna kitabu nilikuwa nasoma, ila sikumbuki mwandishi ni nani. Kwenye hiki kitabu mwandishi akawa anaeleza kuwa alikuwa anakaa bibi yake, pale kwa bibi yake walikuwa wanakaa watoto kama kumi hivi na zaidi. Sasa siku moja bibi yake alimwita pembeni huyu mjukuu wake kwa ajili ya maongezi binafsi ambapo watoto wengine hawakuwepo. Kijana alimsikiliza bibi yake kwa umakini mkubwa sana, bibi yake alimwambia kwamba, nimeangalia kati ya vijana wote wanaokaa hapa, nimeona kwamba wewe una uwezo mkubwa sana na ninakuhakikishia kwamba siku moja wewe unaenda kufanikiwa sana.
Bibi yake akamsisitiza kuwa aende autumie huo uwezo wake vizuri kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha, na mwisho kabisa akamwabia asimwambie mtu hayo aliyomwambia.
Mwandishi alisema hiki kitu 5 kilimpa nguvu kubwa sana kwenye maisha.
Baadaye alikuja kugundua kuwa bibi yake alikuwa na utaratibu wa kumwita kila kijana wake mmoja mmoja na kumwambia maneno hayohayo, kumbe siyo yeye tu alikuwa ameambiwa hayo maneno. bali watoto wengine walikuwa wameambiwa hayo maneno, lakini bado kujua hilo halikumkatisha tamaa. Alichukua kile alichoambiwa na bibi yake moyoni na kuamua kukifanyia kazi ili kuhakikisha anafanya makubwa kwenye maisha.
Wewe pia kama mzazi unaweza kuwatia moyo watoto na wajukuu kwa kuwaambia maneno mazuri ambayo yatawasukuma kufanya kitu cha tofauti kwenye maisha yao. Na muda mzuri ni sasa.
Muda mzuri wa kupanda miti
Kuna msemo mmoja wa kiafrika unaosema kwamba muda mzuri wa kupanda mti ulikuw ani miaka ishirini iliyopita, ila muda mzuri zaidi ni sasa. Unajiuliza hivi kupanda miti na kunoa vipaji sasa vinaendanaje? Ninachotaka nikwambie hapa ni kuwa kama wewe hukuweza kugundua kipaji chako ukiwa kijana, basi wewe unaweza kusaidia vijana na watoto kugundua vipaji vyao pia.
Na wakishagundua vipaji vyao, wafuatilie kwenye kuvifanyia kazi mazoezi na kuhakikisha vipaji hivyo vinakuwa vyenye manufaa kwao pia.
Nimewahi kusikia stori, kuwa baba yake Mbwana Samatta alikuwa anamfuatilia nyuma kuhakikisha anafanya vizuri kwenye mchezo, na hata alikuwa na mfumo wa kutoa zawadi au adhabu kama Samatta angefunga.
Yaani kwamba walikuwa wameweka mkataba kwamba kama Samatta atafunga goli, basi baba yake atamzawadia shilingi elfu mbili, na kama atafungwa basi yeye anapaswa kulipa faini ya elfu mbili.
Japo sina uhakika na hili kwa asilimia mia moja. lakini hiki kitu kinaweza kuwa kitu chenye manufaa kwa wazazi, kukitumia kwa watoto. Unaweza kutumia mfumo wa zawadi na adhabu kumsaidia mwanao, mjukuu au mtoto yeyote kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chake.
Mfano unaweza kununua zawadi na kuja nazo pale nyumbani, hizo zawadi ukaziwekea sharti ya kuzipata.
Mfano unaweza kumwambia kuwa utapata zawadi hii endapo utafanya hiki na kile, utapata zawadi hii endapo utakamilisha hesabu zako za darasani.
Utapata zawadi hii endapo utafanya homework na kuimaliza. Hiki kitu kikampa motisha mtoto kufanyia kazi kipaji chake cha hesabu au kusoma, na hivyo kumsaidia kuboresha zaidi kile kilicho ndani yake,
Lakini pia ni motisha kwa mtoto maana anakuwa anajua kwamba endapo hatafanya mazoezi au hatakamilisha jambo fulani basi hatapata zawadi yake uliyomwandalia ambayo kwake ni adhabu.
Hiki kitu kina nguvu kubwa sana, maana mtoto anapokuwa anajua kuwa nyuma yake mara zote kuna wazazi ambao wanafuatilia kile anachofanya, basi ni hakika kuwa huyu mtoto atajitahidi kuhakikisha kwamba anafanya vizuri. Pale mzazi anapokuwa ni shabiki namba moja wa mwanae, ni wazi kuwa mtoto anakuwa hataki kumwangusha mtoto wake kwenye kile anachofanya
Tujenge utaratibu wa kufuatilia. Kazi za wanetu
Kama mzazi na mtu ambaye anaanda kizazi kijacho cha vijana, basi ni muhimu sana ukajenga utaratibu wa kufuatilia vitu ambavyo mwanao anakuwa anafanya. hata michezo ya kawaida, vinampa nguvu kubwa sana, lakini wakati huo vinamwepusha kufanya mambo ambayo siyo maana anakuwa anajua kuna mtu nyuma yangu ambaye anafuatilia kila ninachofanya.
Kwenye kitabu chake cha Think Big, mwandishi Ben Carson anaeleza namna ambavyo mama yake alikuwa akifuatilia kazi zake anazofanya na hat kumpa kazi ya kusoma vitabu viwili kila wiki. Hiki kitu tu, kilimfanya kijana huyu ajenge utaratibu wa kusoma vitabu, kitu ambacho baadaye maishani mwake kilikuja kuwa chenye manufaa makubwa sana kwake. Katika harakati za kuandaa kizazi kijacho, tunaweza kujifunza hapa pia.
Siku moja kwenye kundi mojawapo la whatsap kulikuwa na mjadala wa namna ya kuandaa kizazi kijacho, ila walikuwa wakizungumzia zaidi kwa upande wa fedha na uwekezaji. Kutoka kwenye huu mjadala nimeona nikushirikishe kipande kimoja muhimu sana ambacho na unaweza kunufaika nacho.
…..kufundisha watoto ni raha sana
…take it easy as a game play
Mfano:
Unawapa Task eg.MAKING MONEY
1) Mwambie somo lolote akipata above 90%… ana jishindia Tzs10,000.Hivyo more 90% means more money..getting rich
2) Na hizi pesa ….yeye ndio ana keep recprds kwenye note book yake.Humpi cash.Akitaka kuspend kwenye toys anapunguza kwenye balance yake.
3) Mshindanishe na nduguze.They will all improve the grades….enjoy the proces,stay motivated….while learning about Money, practically….with adrenalin pump
5)Pia mpe vitabu kuhusu Money ,Investments na Self Development…….. kila kitabu akimaliza aandae presentation…..anakuhadithia, [akifanya vizuri] mzawadie Tzs15,000 [kwa] kila presentation…..utashangaa walivyo smart na idadi ya vitabu atakavyosoma
6) Akifika 18yrs, akapata NIDA, immediately …mpe balance yake…anaanza trading and investment….on his own…..tena kwa pesa yake aliyoitengeneza mwenywewe.
*Money Runs The world…..kids enjoy earning it too*
…i have tested it…several times…. it works very well….. kids are lovely learning partners.Utajikuta na wewe unajifunza mengi ili kumlainishia…akuelewe..same time mna tengeneza bonge la parent-child relationship
…also gets you to learn human behaviour arround money & investments via little beings
…ukija baadae kumfundisha technical and fundamental approaches…..hashangai chochote….kuhusu patterns,candlestics,risk management,money psychology,sentiments etc….kwani ulianzia kwenye DNA of money….yaani X & Y chromosomes of money , to be specific
Maisha yanapokupa limau unatengeneza juisi
Mzee mmoja baada ya kuona kwamba umri wake umeenda na hawezi tena kuingia uwanjani na kuanza kujifunza mpira, aliona atatumia kipaji chake kufundisha watoto na vijana mpira wa miguu, hivyo alijifunza ukocha wa mpira wa miguu na kuanza kutoa mafunzo kwa kizazi kijacho. Baada ya hapo alienda mbali zaidi na kuwa na shule maalumu ya kuwafundisha vijana na kuandaa kizazi kijacho. Kwa jinsi hiyo hakuruhusu kipaji na uwezo wake ufe bila ya yeye kuutumia kama ambavyo alikuwa anatakiwa kuutumia.
Wewe pia pengine umri wako umeenda na unaona kwamba huwezi kurudi nyuma na kuanza kunoa kipaji chako upya, ila kitu kimoja cha uhakika ni kuwa kuna namna unavyoweza kusaidia kizazi kingine huku wewe ukinufaika pia.
Pengine unaweza hata kuandka kitabu na kutoa mafunzo kwa vijana na kuwaasa wasifanye makosa kama ya kwako uliyofanya kwenye kunoa na kuendeleza kipaji chako.