Sababu 15 kwa nini haupaswi kuwa na plan B


Kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 kuikuwa na utani ambao ulikuwa unasambaa mtandaoni. Mmoja wa watu alitengeneza meme fulani hivi ambayo ilikuwa ikimwongelea waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa. Ilikuwa inasema kuwa kila mara unapaswa kuwa na Plan B kama Lowassa. Amekatwa CCM asigombee urais, amehamia CHADEMA, na sasa akishindwa kuingia ikulu kwa tiketi ya CHADEMA anahama nchi anaenda kugombea Senegal.

Sina hakika sana kama nchi iliyokuwa inatajwa ilikuwa ni Senegal kweli, ila nina uhakika na kitu kimoja tu. kitu hiki ni kuwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 hapa nchini Tanzania, kulikuwa na nchi nyingine hapa barani affrika iliyokuwa inategemea kufanya uchaguzi. Kwa hiyo, aliyetengeneza hiki kichekesho alikuwa akionesha kuwa endapo Lowassa atashindwa kuingia ikulu kwa tiketi ya CHADEMA basi angehama nchi, kwenda kugombea huko maana mara zote alikuwa na plan B.

Ok ok, siku ya leo siko hapa kumwongelea Lowassa wala kuongelea siasa, ila nipo hapa kuongelea kitu kimoja tu. PLAN B. kumekuwe[o na maoni mengi sana ya watu wakisema kwamba unapaswa kuwa na plan B kwenye maisha yako.

Tena watu wamekuwa wakisema hili kwa msisitizo mkubwa sana, kwamba endapo utashindwa kwenye plan A, yaani, ile plan ambayo unaifanyia kazi sasa hivi, basi utapaswa kuhamia kwenye plan B. Siku ya leo nipo hapa kukwambia kuwa haupaswi kuwa na PLAN B kwenye maisha yako na zifuatazo ni sababu 15 kwa nini haupaswi kuwa na PLAN B

KWANZA, SIYO SALAMA KWA AFYA YAKO

Wengi wanafikiri kuwa ukiwa na plan B, basi mpango fulani ukishindwa  utaachana nao na kuingia kwenye mpango mwingine. Hiki kitu ndicho kimewafanya watu wengi washindwe kuendelea kwenye maisha. Unakuta mtu ana mpango mzuri, ila sasa haufanyii kazi mpango wake kwa kujitoa kwa sababu ana mpango mwingine unaoelekeana na huo ambao anauita PLAN B.

Tuchukulie mfano tu wa mtu ambaye amehitimu chuo na anatamani kuanzisha biashara. Unakuta mtu wa aina hii anashindwa kuanzisha biashara au hata akiianzisha hiyo biashara inashindwa kukua kwa sababu moja tu, mtu huyu muda wote anakuwa anafikiria kuwa nikizuga tu kwenye biashara na ikafeli naenda kutafuta kazi. Kwa hiyo, yeye muda wote anajua kuwa hata biashara isipofanya vizuri, yeye atakuwa na sehemu ya kuangikia ambayo ni ajira. Kitu hiki sasa hakiwezi kumfanya mtu ajisukume na kufanya makubwa zaidi. pale ambapo mtu anakuwa anajua kwamba kuna sehemu ya kuangukia basi, ujue wazi kuwa huyo mtu hatajisukuma kufanya makubwa.

Kijana ambaye anajua wazi kuwa nyumbani kwao kuna kila kitu (wa kishua), hatajisukuma kufanya vitu na kupambana, badala yake atakuwa anjua kwamba hata asipofanya kitu chochote, pele nyumbani vitu si vipo tu.

Wakati hali ni tofauti kwa kijana ambaye anakuwa anajua kwamba asipopambana basi siku hiyo hana ugali.

Au yule anayekuwa anajua kuwa anapaswa kupambana kwa ajili ya wazazi wanaomtegemea yeye.

Siku moja nilikuwa namsikiliza Les Brown kwenye mojawapo ya mazungumzo yake. Les Brown akawa amesema kwamba alikuwa anauza bidhaa nyumba kwa nyumba. Hivi unajua kweli mauzo ya nyumba kwa nyumba au unayasikia redioni tu.

Mauzo ya nyumba kwa nyumba ni yale ambayo unakuwa unaenda unagonga nyumba moja baada ya nyingine na kuwaambia bidhaa uliyonayo, huku ukiwashawishi wanunue. Mfano, unachukua kitabu changu cha  NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Unaenda nacho nyumba kwa nyumba ukikiuza. Unagonga kila nyumba na kuwaambia kuwa hapa nina kitabu kizuri kinachoweza kukusaidia wewe kufanikisha lengo lolote kubwa kwa kuchukua hatua ndogondogo kila siku. Unatoa maelekezo kedekede, kisha unawaambia watu wakupe hela uwaachie kitabu.

Sasa haya mauzo, yanahitaji moyo sana. Maana unapokuwa unagonga mlangoni mwa mtu, unakuwa huna uhakika kama huyo mtu anataka hiyo bidhaa au hataki. Unakuwa hujui kama huyo mtu atapenda kupata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA au la hatataka,

Hujui kama huyo mtu ana shida ya sabuni yako, au tayari anazo sabuni.

Mauzo ya aina hii, kibongobongo wanafanya wachache sana, hata wale wanaozunguka mitaani na laini za simu hawajafikia hicho kiwango cha kugonga mlango mmoja baada ya mwingine. mara nyingi wanapita tu mtaani wanatembea.

Sasa kwenye mauzo ya aina hii, kuna matatu ambayo unaweza kukutana nayo.

  • Mteja anaweza kukwambia, ndio nataka bidhaa. Tukitumia mfano wetu hapo juu, anaweza kusema anataka kupata kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA
  • Au anaweza kukwambia kwa sasa hapana, labda siku nyingine
  • Au anaweza kukwambia, hapana
  • Au anaweza kukwambia hapana pamoja na matusi juu yake.

Sijui unanielewa. Sasa hakuna kitu kinakatisha tamaa kama majibu mawili ya mwisho, hasa unapokuwa unajijua una bidhaa nzuri ambayo ingeweza kumsaidia mteja kama ambavyo mimi nina kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na ninajua sana kuwa kinaweza kukusaidia wewe. Rusha basi, elfu ishirini ili upate nakala yako (Hardcopy). Namba ya kurusha hela ni 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Kitu hiki, huwa kinawafanya watu wachache sana wajihusihe na na mauzo haya. Ila sasa, ubora wa mauzo haya ni kwamba, kadiri unavyokutana na watu wengi zaidi, ndivyo unavyouza zaidi. Ukikutana na watu kumi. Saba au nane watakataa, ila watatu au wawili watanunua. Kwa hiyo, unakataliwa sana ila pia unauza zaidi. Sasa Les Brown alisema kwamba, yeye alikuwa analazimika kuendelea na mauzo haya kwa sababu tu hakuwa na njia nyingine ya ziada kwenye maisha yake ya kupata kipato isipokuwa hiyo.

Anasema kuna rafiki yake walianza pamoja hii kazi ila aliishia njiani,kwa sababu alikuwa na plan B. ila yeye hakuwa na plan nyingine yoyote ile isipokuwa kuhakikisha kwamba ameuza, maana la sivyo, mama yake asingeweza kupata chakula siku hiyo.

PILI WATU WALIOFANIKIWA SIYO WALE WENYE PLAN B

Watu wengi walioweza kufanikiwa kwenye maisha siyo wale waliofanya jambo fulani wakiwa na plan B kwenye kichwa chao, bali wale waliofanya lile jambo kwa moyo wote wakiwa wanajua kuwa ni au walifanye hilo jambo na kulifanikisha au la wafe wakiwa wanapambia hilo jambo.

Siku moja nilikuwa nasikiliza hotuba ya Arnold Schwaznegger. Kwenye hiyo hotuba Arnold alisema kuwa yeye kwenye maisha hapendi kuwa nap la B.

Mimi mwenyewe sipendi kabisa kuwa na plan B. kwa vyovyote vile, kwenye maisha watu wenye plan B huwa hawafanikiwi.,waliofanikiwa kwenye maisha ni wale ambao walikuwa na plan moja tu, wale walioweka nguvu na muda wao wote kwenye kitu kimoja na wakakifanya bila kurudi nyuma.

TATU, UKIKWAMA UNARUDI NYUMA

Unapokuwa na plan B. ukikutana na kikwazo kidogo tu, hapohapo unarudi nyuma. Maana unajua kuwa utaenda kuegemea sehemu fulani. Ila pale unapokuwa unajua kuwa ni lazima nifanye hiki kitu, au la nitakufa nikiwa napambia hiki kitu, basi utapambana kwa nguvu zako zote kuhakikisha kuwa kile kitu unakifanyia kazi bila ya kurudi nyuma.

Moja ya kitu ambacho watu wengi wamekuwa hawafahamu ni kuwa vikwazo kwenye maisha lazima tu vitokee. Yaani, hakuna namna yoyote ile kwenye maisha unaweza kuishi bila ya kuwa vikwazo. Vikwazo vinatokea kwenye maisha, sasa utakuwa na plan B ngapi?

Ndio maaana kwenye ndoa unaambiwa ukishakuwa na mwenza wako unakuwa naye milele. Kwa sababu wanajua kuwa kwenye ndoa kuna vikwazo vingi, sasa ebu fikiria kila mtu akiingia kwenye ndoa na plan B. Huyo mtu ataoa au ataolewa na wanagapi? Maana kila atakapokutana na kikwazo tu, maana yake ataachana na mwenza wake na kwenda kuolewa na mtu mwingine ambaye anadhani hana changamoto. Na mwenyewe akiwa na changamoto anaachana naye tena. Ndio maana unaambiwa uishi na mwenza wako kwenye shida na raha (NO PLAN B)

Kwa hiyo, kama ilivyo kwenye ndoa, vivyo hivyo kwenye maisha. Uanapaswa kuchagua kitu kimoja na kuamua kukomaa na hicho kitu bila ya kurudi nyuma hata kama unakutana na changamoto kiasi gani.

Ubora changamoto na vikwazo ambavyo unakutana navyo kwenye maisha, siyo kwambna ni vikwazo, badala yake kila unapokutana na changamoto au vikwazo kwenye maisha, maana yake unapata somo kutoka kwenye hivyo vikwazo na hizo changamoto, kitu ambacho kinakufanya uweze kuwa imara kwa siku ambazo zinazofuata.

Ebu chukulia mfano wa kawaida tu,

Ebu tuchukulie kwa mfano umeanzisha biashara, halafu kadiri unavyoenda unakutana na changamoto ya kutoona hela kwenye biashara yako. Mwanzoni unaanza kufikiri kuwa labda hawa watakuwa ni chuma ulete. Lakini kadiri unavyoendelea kufuatilia zaidi, unagundua kuwa siyo chuma ulete, ila tatizo liko kwako. unagundua kuwa tatizo umekuwa unachukua hela ya biashara na kuifanya kuwa hela yako.

Yaani, umekuwa hutenganishi kati ya hela yako na hela ya biashara. Hivyo, unaamua kuwa kuanzis sasa utaanza kutengenisha kati ya hela yako na hela ya biashara. Unaamua wazi kuwa kamwe kwenye maisha yako, hutachukua hela ya biashara uitumie kma ya kwako. Badala yake utakuwa unajilipa wewe mshahara kama mfanyakazi kwenye biasahara yako na kiasi kingine utakuwa unakiacha kwenye biashara. Lakini unaenda mbali zaidi kwa kuhakikisha kwamba unatunza kumbukumbu za hela zote zinazoingia na kutoka kwenye biashara. Rafiki yangu, hiki kitu kidogo tu, kina nguvu kubwa sana. kubwa mno, nakwambia.

Baada ya muda ni wazi kuwa utaanza kuona matokeo ya tofauti, na matokeo ya tofauti maana yake wewe umeshatatua changamoto au kikwazo kilichokuwa kinakurudisha nyuma na sasa unaendelea mbele. Siku nyingine ukikutana na changamoto au kikwazo kingine ni wazi kuwa hutarudi nyuma, badala yake utaendelea mbele zaidi.

Mfano siku nyingine ukikutana na kikwazo cha mauzo kidogo, suluhisho la kikwazo hiki siyo kuacha kufanya ile biashara unayofanya na kukimbilia kufanyia kazi plan B. Badala yake suluhisho lake ni wewe kutafuta wateja zaidi. na ili kupata wateja zaidi maana yake unapaswa kujifunza mbinu mpya za mauzo na masoko. Kumbe ukiwa na plan B, maana yake unakosa akili ya kujiongeza na kufanya makubwa zaidi, ila ukiwa na plan hiyohiyo na ukakomaa nayo, unakuwa na akili ya ziada.

Kabla sijamalizia hii pointi ningependa nitoa kwa ufupi sana hadithi ya Heran Cortes. Huyu jamaa alienda na jeshi dogo kupigana vita na jeshi kubwa. Walienda na boti na baada ya kuwa wameshuka salama kwenye boti, aliamuru boti zote zichomwe moto.

Kitu hiki kilituma ujumbe kwa wanajeshi wake kuwa hakuna plan B. Maana yake, walipaswa kushinda hiyo vita, au la walipaswa kufia hapohapo.

Sasa hiki kitu kina maana gani kwako, maana tumeshatoka kwenye hizo zama za kivita, ila kitu kimoja cha uhakika tunachojifunza kutoka hii stori fupi ni kutokuwa na plan B kwenye maisha. Plan B,  inakwamisha. Plan B inakufanya uwe na sehemu ya kuegemea na hivyo, unashindwa kutimiza wajibu wako kwa viwango vikubwa.  Niendelee au niishie hapa!

Ebu basi subscribe kwenye channel yangu ya youtube kwanza halafu tuendelee. BONYEZA HAPA kufanya hivyo.

NNE; HAUFIKIRII INJE YA BOKSI

Siku za karibuni nimekuwa naongea na rafiki yangu mmoja ambaye huwa anafuatilia mafunzo yangu kwa njia ya mtandao. Anafanya kazi ya ubodaboda,ila anaonekana kama ameikatia tamaa. Maana ni kama haoni matokeo kwenye kile anachofanya na hata malipo yake anaona siyo makubwa sana. wiki iliyopita, nilimpa mbinu kadha wa kadha za kumsaidia kuongeza wateja zaidi na hivyo kulipwa zaidi.

Sasa jana wakati naongea naye akaniambia ameanza kuona matokeo. Nikawa nimemwambia kuwa asifanye hicho kitu mara moja tu, badala yake awe na mwendelezo. Kwa siku ya jana nikamwambia kitu kimoja tu, nikawambia nenda ukannunue mfuko wa pipi. Halafu kwa kila abiria unayesafiri naye hakikisha kwamba unampa pipi ili aende anakula. Hiki kitu kilimshangaza kidogo ila alikifurahia sana.

Akaanza kuniambia habari za basi ambazo huwa zinatoa pipi, biskuti na soda. Akaniambia kuna mwalimu wake alisafiri na basi wakampa pipi, soda na biskuti na tangu siku hiyo mwalimu huyo akawa ameapa kuwa atasafiri na basi hiyo hiyo siku zote ili apate soda, biskuti na pipi.

Nikawa nimemwambia kuwa unapokuwa umesafiri na basi, unalipia nauli karibia elfu hamsini, sitini au sabini. Kwenye hiyo nauli yako, wenyewe wanatoa elfu mbili tu, wanakununulia wewe pipi mbili, soda moja na biskuti. Unapewa na huwasahau, sasa hiki kitu unaweza kukitumia. Ukimpa mtu pipi ya shilingi mia moja kutoka kwenye elfu mbli ya usafiri wako wa bodaboda unakuwa hujapunguza kitu kikubwa. ila unakuwa umejenga mteja wako wa nguvu maana siku nyingine yule mtu akitaka usafiri, hataanza kumtafuta bodaboda mwingne, badala yake atakutafuta wewe ili apate pipi ya kulamba njiani, wakati unamsafirisha. Daah, halafu darasa la kulipia kabia mimi nakupa bure hapa, hahaha.

Kama nakuona na wewe unavyoenda kuitumia hii mbinu niliyompa jamaa jana. Hahaha

Ila kitu kikubwa ninachotaka kumwambia ni kuwa mawazo ya kuboresha biashara au kitu chohote kile hayatoki kwa watu ambao wana plan B. mtu mwenye plan B akifeli anawaza kwenda kwenye kilimo, kwenye kilimo akilima tikiti zikamwangusha anawaza kwenda kwenye madini, kwenye madini akikutana na changamoto anawaza kwenda bandarini maana anasikia habari za watu wanaopata mabilioni. Akiwa hajatulia bandarini anasikia habari za watu wanaouza mbao Iringa anaenda Iringa. Akiika tu iringa, habari za kilimo cha mpunga Ifakara zinamfikia anahamia ifakara, sikiliza rafiki yangu, huwezi kutoboa kwenye maisha ukiwa na plan nyinginyingi hivyo. Kuwa na plan moja kisha komaa na hiyo.

Ubora ni kuwa kadiri siku zinavyokuwa zinaendelea kusogea mbelea wewe mwenyewe unakuwa unazidi kuimarika na kuwa bora zaidi.

Kabla sijaendelea mbele zaidi, naomba ufanye kitu kimoja. Weka barua pepe yako hapa chini,ili uwe unapokea mafunzo zaidi kutoka kwangu kwa njia ya baruapepe.  Fanya hivyo sasa hivi ili tuendelee

TANO; PLAN B  INAKUKWAMISHA KUFANIKISHA PLAN YAKO KUU

Ule muda unaouweka kwenye kufikiria plan B. Ule muda unaoutumia kufanyia kazi plan B, ni muda ambao unaupoteza, badala yake muda huu wote ungeweza kuuweka kwenye jambo lako kuu na kulifanyia kazi mpaka likafikia viwango vikubwa.

Ujue unapokuwa na mambo mengi ambayo unafikiria kufanya, unakuwa hauweki akili yako na nguvu zako sehemu moja, ila unapokuwa na jambo moja na unapokoma na huilo jambo maana yake hata ukikutana na kikwazo au kitu chochote kile cha kukukwamisha, maana yake utapambana  kuhakikisha kwamba unalifanyia kazi jambo husika mpaka uweze kulifanikisha.

SI TA; TAFITI ZINAONESHA KUWA PLAN B ni chanzo cha KUTOKUFANYA VIZURI

Wanasayansi katika chuo kikuu cha Wharton na chuo Wisconsin walifanya utafiti kwa watu ambao waliwagawa kwenye makundi mawili. Kundi la kwanza lilikuwa la watu ambao walikuwa waliambiwa wafanye jambo fulani. Na kundi la pili liliambiwa lifanye jambo fulani, ila kwanza lilipaswa kufikiria endapo mambo hayataenda kulingana na matarajio yao itakuwaje. Kwa lugha nyingine ni sawa na kusema kwamba kundi la pili lilitakuwa kuwa na plan B.

Mwisho wa siku majibu ya utafiti huo yalioonesha kuwa waliokuwa na plan B hawakufaya vizuri ukilinganisha na wale waliokuwa na plan moja tu.

Mimi sina cha kuongeza, maana utafiti umeongea na umemaliza.

Hivi nilisema kuna sababu 15 ee kwa nini haupaswi kuwa na plan B. Na bado unataka niendelee au niishie hapa! kama umependa makala hii, utapenda pia kitabu changu kipya cha JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO. Weka oda leo upate punguzo la kitabu hiki, soft copy itaanza kupatikana tarehe 10.10.2022. Na gharama ya softcopy ni 10,000/- ila ukilipia kabla ya tarehe 10, utaipata kwa elfu saba tu. Kwenye hiki kitabu nimejadili kwa kina mada hii ya plan B. Nina uhakika utaipenda tu. na sababu zilizobaki nimezimalizia kwenye kitabu.

Umekuwa nami GODIUS RWEYONGEZA

Asante sana kwa kusoma makala hii. hakikisha unajaza taarifa zako hapo chini ili uwe miongoni mwa watu ambao wataku wanapokea makala zangu kwa njia ya baruapepe. Huwa naandika makala nyingine zaidi na kuzituma kwa njia ya baruapepe. Ningependa na wewe uzipokee hizi makala, jaza taarifa zako hapa chini ili uzipate.


One response to “Sababu 15 kwa nini haupaswi kuwa na plan B”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X