Usifanye kitu mara moja…


Kama unataka kubobea kwenye kitu, usifanye hicho kitu mara moja. badala yake kifanya mara kwa mara na kwa mwendelezo. Kadiri unavyofanya kitu au kazi mara kwa mara inakupa nguvu na ufanisi na hata kujiamini.

Marudio yako kwenye kufanya kazi yanakufanya uzidi kubobea na hatimaye unakuwa bingwa.

Mchezaji bora wa mpira wa miguu siyo yule ambaye anafanya mazoezi mara moja, kisha akatulia. Bali ni yule anayefanya mazoezi ya mara kwa mara.

Mwimbaji mzuri siyo yule anayeimba mara moja, kisha akasahau.. bali yule anayefanya mazoezi ya kuimba mara kwa mara.

Hata kama unajua wazi kabisa kuwa una kipaji kikubwa cha kufanya vitu, usifanye  hicho kitu mara moja, kisha ukatulia, kuwa na mwendelezo kwenye kazi au kile ambacho unakifanya. Kadiri unavyokifanya kwa mwendelezo ndivyo unavyokuwa mbobevu.

Unataka kuwa mwandishi mbobevu, basi usiandike mara moja tu na kutulia, badala yake andika mara kwa mara na maandiko mengi kadiri uwezavyo.

Unataka kufikia uhuru wa kifedha? Usiweke akiba mara moja na kutulia, au usiwekeze mara moja kisha ukasahau kila kitu, badala yake endelea kuweka akiba mara na kila unapopata fedha mfukoni.

Unataka kuwa mwimbaji wa kimataifa? Usiimbe mara moja tu na kusahau, kuwa na mwendelezo wa kile unachofanya.

Rafiki yangu, mkusanyiko wa hivi vitu vidogovidogo unavyofanya mwisho wa siku vinakuwa vitu vikubwa, kweli.

Hiki ni kitu kilichonisukuma kuandika kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Kitabu ambacho nina uhakika kitakusaidia na wewe kwenye hii safari ya kufanya makubwa

Pata nakala yako siku ya leo,  utanishukuru siku zijazo.

Nakala moja ni elfu 20,000/- tu za kitanzania. Utatumiwa popote pale ulipo. Kupata nakala hii, utatuma fedha kwa namba 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Mara tu baada ya kutuma fedha yako utatutaarifu, ili tukutumie nakala ya kitabu hiki. Unakipokea popote pale ulipo duniani.

Ubora ni kuwa kuna audiobook pia. Je, ungependa kupata audiobook ya kitabu hiki cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA? Kama jibu lako ni ndio, basi umeshakipata mpaka hapo. Tuma elfu kumi tu kwa ajili ya audiobook, itume kwenda nambari ya simu 0684408755.

Kumbuka. Hardcopy inauzwa kwa elfu 20,000/- na audiobook inauzwa kwa elfu kumi (10,000/-) tu.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X