Vitu 21 Ambavyo Ni Lazima Kufanya Hata Kama Una Kipaji Kikubwa


KIPAJI NI DHAHABU
Rafiki yangu, nimeandika kitabu. Kinaitwa KIPAJI NI DHAHABU. Ili kupata kitabu hiki, wasialiana na mi kwa 0755848391 sasa

Rafiki, una kipaji si ndio! Hongera sana, mbali na kuwa una kipaji na unakifanyia kazi na una maono makubwa ya kukipeleka mbali kipaji chako mpaka kwenye ngazi za kimataifa. Ila kuna vitu vya msingi sana ambavyo hupaswi kuacha kufanya hata kama una kipaji kikubwa. kwenye hii sura ninaenenda kukushirikisha vitu 21 ambavyo hupaswi kuacha kufanya hata kama una kipaji kikubwa

1. Unapaswa kuweka akiba.

Rafiki yangu, bila kujali una kipaji kikubwa kiasi gani, haupaswi kuacha kuweka akiba. Mara zote hakikisha kwamba unaweka akiba kutokana na kiasi cha fedha ambacho unapokea. Hata kama ni kidogo kiasi gani. hakikisha kwamba mara zote unatoa kiasi kidogo na unakiweka kama akiba. Moja ya shida ambayo huwa inawakumba watu wenye vipaji wanapofikia umri wa kustaafu ni kuwa wanakuwa hawana akiba wala hela ambayo wanaweza kutumia. Yaani, mtu amekuwa anapambana kwa miaka mingi, ila sasa unapofika wakati kula matunda ya jasho lake, anakuwa hana matunda ya kula. Rafiki yangu, nataka wewe ujiondoe kwenye huu mtego kwa kuhakikisha kwamba unaweka akiba na kuwekeza. Na kiwango cha kuweka akiba siyo kikubwa sana, ni aslimia kumi tu ya kila kiasi ambacho kinaingia kwenye mfuko wako. Rafiki yangu, hiki ni kitu ambacho unapaswa kukipambania kila mara.

Ila kwa hapa ningependa kukueleza mambo yafuatayo kuhusu uwekaji wa akiba

Kwanza, leo hii nenda kafungue akaunti benki ambayo utakuwa unaweka akiba yako. Utafiti unaonesha kuwa watu wenye akaunti za benki, wanakuwa na utaratibu wa kujiwekea akiba, ukilinganisha na wale ambao hawana akaunti za benki.

Anza kuweka akiba yako, hata kama ni kidogo. Ubora benki wanaruhusu kuweka kiasi cha chini ambacho ni elfu moja. hivyo, kila ukipata kiasi fulani cha fedha rafiki yangu, hakikisha kwamba unaweka akiba bila kukosa. Hiki kiasi hiki, kitakuja kukusaidia siku za mbeleni kwenye uwekezaji au hata malengo yako ya kukuza kipaji chako zaidi.

NB: usiweke fedha yako chini ya godoro. Hizi zama za kuweka fedha chini ya godoro zimeshapitwa na wakati. sana tafuta kuweka akiba yako, sehemu ambayo huwezi kuifikia kwa haraka sana. Inaweza kuwa ni kwenye laini ya simu ambayo hujui namba yake siri yake ya mpesa.

Inaweza kuwa ni benki au kwenye mifuko ya uwekezaji ya pamoja ya UTT. Kwa kuwa kitabu hiki siyo cha uwekaji wa akiba wala uwekezaji, basi naomba ukasome kitabu changu kinaitwa MAAJABU YA KUWEKA AKIBA na kingine kinaitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hivi vitabu viwili vitakufundisha kwa kina suala zima la fedha. Wasiliana nami kwa namba 0755848391 sasa.

2. Unapaswa kuwekeza

Rafiki yangu, kitu kingine muhimu sana ambacho unapaswa kujua na kukipa nguvu kubwa sana ni uwekezaji. Unapokuwa na kipaji, maana yake wewe unakuwa unafanya kazi kwa ajili ya kuingiza fedha. Usipokuwepo moja kwa moja maana yake siku hiyo hakuna kitu chochote kile ambacho kinaweza kufanyika kwa manufaa. Sasa kipaji chako kinakuwezesha wewe kupata fedha, na unapopata fedha unapaswa kuwekeza pia. Uwekezaji ni moja ya eneo ambalo linakufanya wewe uwe unapata fedha bila hata ya kuwepo kufanya kazi.

Kwa hiyo basi rafiki yangu, napenda kukuhakikishia kuwa uwekezaji ni moja ya jambo muhimu sana kwenye maisha yako, ambalo unapaswa kufanya. Kwa hiyo, wekeza. Kwa kuwa wewe ni mgeni kwenye uliwengu wa uwekwezaji, basi hakikisha kuwa unaanza kuwekeza na kwa kuanzia, basi anza kuwekeza kwenye mifuko ya uwekezaji wa wa pamoja.

Na ujue kiwango unachohitaji kuanza nacho ili uweze kuwekeza siyo kikubwa sana kama ambavyo unaweza kufikiria. Ni kiwango kidogo tu, ukiwa na elfu kumi unaweza kufungua akaunti kwenye mfuko wa umoja na baada ya hapo unaweza kuendelea kuwekeza zaidi na zaidi kwa kuweka kiwango cha chini cha elfu tano.

Baada ya kuwa umefanya kazi kwa miaka yako yote, haupaswi kuwa mstaafu aliyefulia.

Siku siyo nyingii nilikuwa nikisoma nikifuatilia historia ya Michael Jordan, nilichokuja kugundua kutoka kwa huyu jama ni kwamba, amewekeza kiasi cha kumwezesha kununua timu ya kikapu. Alipokuwa mchezaji, kile kiasi cha fedha alichokuwa analipwa alikuwa hatumii chote.

Moja ya kitu kinachowafanya watu wenye vipaji bongo (wachezaji, wanariadha, wanamziki n.k) kufuria baada ya kustaafu ni kuwa pale wanapokuw wanaingiza fedha, basi wanaendekeza starehe kuliko wanavyowekeza. Hiki kitu unapaswa kuepukana nacho. Kuna madhara mawili ya kuendekeza starehe. Kwanza utajiona kama vile umefika kule unapotakiwa kwenda wakati bado ndio kwanza safari yako imeanza.

Pili, ukiendekeza starehe utasahau kuchapa kazi na hivyo kushuka kwenye kiwango unachofanyia kazi kipaji chako. Unaukumba wimbo wa Tundaman na Chege wanaosema Starehe gharama?

3. Unapaswa kujifunza na kufikiri kibiashara

Kinachowakwamisha vijana wengi wa kitanzania kwenye vipaji vyao ni wao kufikiri kuwa; kwa kuwa wana vipaji basi wanapaswa kupambana wao kama wao tu. Sikiliza, kama unataka kipaji chako kifike mbali, basi kiweke kibiashara.

Hii ndio kusema kwamba, angalia namna ya kuwahusisha watu wengine wakusaidie kwenye kipaji chako. Hawa wanaweza kuwa ni watu watakaokusaidia wewe kusambaza kile unachofanya, au wale watakaokusadia kuwafikia wateja wako. Kwa vyovyote vile, hakikisha kwamba kipaji chako hakikugandi, kifanye kuwa biashara ndio utafika mbali zaidi. Ndio maana huwa unaona wengine wanakuwa na meneja na vitu kama hivyo. Naombe nieleweke,kwenye hili kwamba, hakuna mtu ambaye huwa anafanya makubwa kwa kutumia dhana ya jeshi la mtu mmoja. Jeshi la mtu mmoja siyo practical kwenye ulimwengu wa leo. Ni kweli utaanza peke yako, lakini huwezi kutoboa kiwango cha kimataifa ukiwa ni jeshi la mtu mmoja! Unahitaji timu!

4.Unapaswa kujifunza ujuzi wa kuongea na kuwasilisha kile ulichonacho mbele ya watu

Hata kama una kipaji ni kama cha Khaby Lame, bado utapaswa kujifunza kuongea mbele watu. kwa sababu kuna siku utapaswa kuongea mbele ya watu. Watu watakuhoji na wewe utalazimika kuwasilisha mada mbele yao katika namna ambayo inaeleweka, kumbe kuongea mbele ya watu ni moja ya jambo ambalo haliepukiki rafiki yangu.

5. Unapaswa kujenga tabia ya kusoma vitabu

Vitabu ni nyenzo. Unajua nyezo lakini? Shule ya msingi tulijifunza kuwa kuna mzigo na jitihada. Hiki kitu kilikuwa kinarahisisha ufanyaji wa kazi. ambapo mtu ulikuwa na uwezo wa kusukuma mzigo mkubwa kwa nguvu kidogo. sasa vitabu pia ni wenzo daraja la kwanza! Vinakusaidia wewe kusukuma maisha na kusonga mbele kwa nguvu kidogo unayoweka kwenye vitabu.

6. Kuondokana na uoga

Uoga umewafanya watu wengi washindwe kufanyia kazi vipaji na uwezo wao. Uoga umewafanya watu washindwe kuthubutu, uoga umewafanya watu wapunguze kasi ya kufanyia kazi malengo yao. Rafiki yangu, ondokana na uoga, simama kisha songambele.

7. Kuweka malengo na kuhakikisha kwamba unayafanyia kazi bila ya kuishia njiani

Mwanzoni mwa mwaka watu wengi huwa wanaweka malengo ila waengi huwa wanaishia njiani. Kila mwaka unapasawa kuweka lengo ambalo utalifanyia kazi ili kuona wapi unafikisha kipaji chako.

Linaweza kuwa ni lengo la kuongeza idadi ya watu wanaofuatilia kazi zako mitandaoni. Linaweza kuwa ni lengo la kuuza kazi zako kwa watu milioni moja. linaweza kuwa ni lengo la kuajiri mtu au watu kadhaa. linaweza kuwa ni lengo la kushirikiana na baadhi ya watu kwenye kazi zako n.k.

Kwa vyovyote vile hakikisha kwamba unakuwa na malengo. Na malengo yako yanapaswa kuwa yamegawanywa kwenye malengo ya wiki, mwezi, mwaka na hata miaka mitano au kumi ijayo.

Tonny Robinns aliwahi kusema kwamba, kuweka malengo ni hatua ya kwanza ya kubadili yasiyowezekana kuwa yanayowezekana.

8. Kukubali kuwa maisha ni wajibu wako

Kama kuna kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha vijana na watu wengi, ni pale ambapo wao wanafikiri kuwa maisha siyo wajibu wao, badala yake wanafikiri kuwa kuna mtu, ambaye anaweza kuwa ni serikali au mjomba ambaye anahusika na maisha yao. Naomba nikwambie hili na ulipokee rafiki yangu, ukweli ni kuwa maisha ni wajibu wako. Ukifeli ni juu yako na ukifanikiwa ni juu yako. Ukilifahamu hili, utaishi maisha kwa raha mustarehe sana rafiki yangu. Unajua kwa nini? Kwa sababu, hutakaa na kuanza kumsubiri mtu ili akusaidia kwenye kufanyia kazi maisha yako, badala yake utapambana kuhakikisha kamba maisha yanakuwa ni wajibu wako kwelikweli.

Utaachana na malalamiko ambayo unatoa sasa hivi. badala ya kusema kwamba serikali haitoi ajira, wewe utapambana kuona ni kwa namna gani unaweza kutengeneza ajira. Ujue unaweza kuwa unalalamika kuwa hakuna ajira, kumbe wewe ndiye unapaswa kuwa mtoaji wa ajira.

9. kuwa kiongozi

Wengi huwa wanachanganya uongozi na cheo. Kitu hiki huwafanya wengi wafikiri kuwa kiongozi ni lazima uwe na cheo. Hapana.

 Haikuhitaji uwe na watu na watu wanakuja kwako kwako kuleta kesi ili uwe kiongozi. Maana yake unaweza kuwa mkulima ila wewe ni kiongozi, mwalimu bodaboda au yeyote ila ni kiongozi. Siku zote nimekuwa nawaambia watu kwamba kila mtu ni kiongizi tangu kuzaliwa kwake.

Kama wewe unaweza kuamka asubuhi na kupangilia mipango yako jinsi itavyoonda na kujiwwkea ratiba nzuri na kuifuata basi wewe ni kiongozi. Kama wewe hauna mtazamo wa kushawishi watu kufanya vizuri zaidi katika shughuli zao basi wewe ni mfuasi.
Hata kama utakuwa na cheo cha uongozi watu hawataweza kukufuata kwa sababu wanaona matendo yako hayaendani na kile unachosema.

Kiongozi wa ngazi ya juu ambaye muda wote amejifungia hataki kuongea na watu wala hataki kuwa karibu na watu basi huyo sio kiongozi ni mfuasi.

10. kuamka mapema

Siwezi kukumbuk ni marangapi nimekuwa nikisisitiza juu ya umuhimu wa kuamka mapema, lakini bado nalazimika kuendelea kufanya hivi. kuamka asubuhi na mapeka kuna manufaa mengi sana.

Kwanza unaamka muda ambao watu wengi wamelala. Hakuna kelele (labda kama unakaa ghetto na washikaji, wanaowasha muziki usiku kucha,hahah). Muda huo hakuna mtu wa kukupigia simu, labda kama utaamka kuongea na mchumba wako aliye Moshi wakati wewe uko Mwanza. Hakuna watu wanakuja kukugongea chumbani kwako. yaani, ni wewe tu na Mungu wako.

Kitu hiki kinakupa nafasi nzuri tu yaw ewe kupata muda wa kufikiri, kupanga ratiba yako ya siku hiyo, kupanga watu ambao utaenda kuwapigia, kupanga watu ambao utaenda kukutana nao na mengine mengi. Kwa hiyo basi rafiki yangu, itumie nafasi ya kuamka asubuhi na mapema vizuri sana.

Nakubaliana na Benjamin Franklin aliyewahi kusema kwamba, kuamka asubuhi na mapema na kulala mapema kunamfanya mtu awe na afya njema, tajiri na mwenye busara.

11. kuinuka baada ya kuanguka

Maisha ni safari rafiki yangu, na kama ilivyo safari yoyo tile. Lazima kwenye kusafiri kwako kuna sehemu ambapo utakutana na mlima, hivyo utapanda huo mlima, na kuna sehemu utakutana na bonde, utashuka. Rafiki yangu, hizi zote ni sehemu za maisha na zinatokea kwenye maisha yetu ya kila siku. Sasa inapotokea umejikwaa kwenye safari yako, basi usije ukarudi nyuma na kuacha kufanyia kazi kile unachopaswa kuwa unafanyia kazi. Endelea kupambana rafiki yangu, mpaka kieleweke. Ukianguka inuka. Inawezekana.

12. Kuanza na kile ulichonacho

Wengi huwa wanasubiri wawe na kila kitu ndio waanze, wewe usisubiri kuwa na kila kitu ili uweze kuanza. Anza na kile ulichonacho.

  • Usisubiri uwe maarufu ili unoe kipaji chako, anzia hapo hapo ulipo na hicho ulichonacho.
  • Usisubiri uwe kama rais Mwinyi ili uandike kitabu. Andika kitabu, halafu hiyo ngazi yake utaifikia mbele ya safari.
  • Usisubiri mpaka uwe na fedha ili uanze kuweka akiba, anza kuweka akiba kwa kiwango hicho hicho ulichonacho. Ngoja nikwabie kitu, asilimia kubwa ya vitu unavyohitaji kufanya, unaweza kuanza kuvifanya sasa hivi bilaya kuchelewa.

13. epuka kujilinganisha na watu wengine

Daah, kama kuna kitu kinawatafuta vijana wengi basi ni hiki; kujilinganisha.

  • Eti kwa sababu fulani kaajiriwa basi ngoja na mimi nipambane ili niajiriwe.
  • Eti kwa sababu fulani kajenga nyumba kijijini kwetu basin a mimi mpaka nikajenge.
  • Eti kwa sababu, fulani yuko kwenye mahusiano na mimi lazima nimpate wa kwangu. Haya bwana kampate,hahaha

Ukijilinganisha, ni wazi kuwa hutaweza kuishi maisha yako kwa namna ambavyo unataka wewe. Maisha yako yatakuwa ni magumu sana,sana. Ishi maisha yako na furahia hilo. Furahia hatua wanazopiga wengine, maana siyo kila hatua lazima na wewe uipige kwa wakati huohuo.

Wakati wengine wanajenga kijijini, wewe uko hapa unawekeza kwenye UTT. Mtu anaweka milioni 50 kwenye kujenga nyumba ya kuishi na familia yake, wewe unaweka milioni hamsini UTT, kwenye mfuko wa hatifungani, unaotoa gawio kila mwezi. Nani kawin hapa? Kama huelewi uwekezaji huu wa kwenye mifuko ya Utt, unaweza usinielewe ninachojaribu kukueleza hapa, ndio maana nakushauri upate kitabu changu cha maajabu ya kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande ili uweze kunielewa vizuri hapa. Ebu rusha elfu tano tu, kwenye simu yangu nikurushie hiki kitabu. Namba ya simu 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

14. Epuka kufuatilia maisha ya watu wengine

Moja ya kitu ambacho unahitaji kuhajkikisha kwamba unaachana nacho kama unataka kufika mbali na kuachana na suala zima la kufuatilia maisha ya watu wengine. Kuna watu wengine wanajua mwenendo wa maisha ya watu wengine, kuliko wanavyo jua kuhusu maisha yao. Hli ni kosa kubwa ambalo unaweza kufanya kwenye maisha yako. Hakikisha kwamba unayajua maisha yako kuliko mtu mwingine au kwa lugha nyingine jifuatilie wewe mwenyewe kuliko unavyomfuatilia mtu mwingine. hivi kwa mfano, kama wewe ungekuwa ni kampuni, je, watu waengewekeza kwenye hiyo kampuni kununua hisa zake, wewe mwenyewe ungewekeza kwenye kampuni wewe kununua hisa zako mwenyewe! Kama jibu ni hapana, maana yake unahitaji kujiboresha.

Na njia nzuri ya kujiboresha, ni wewe kuacha kufuatilia maisha ya watu wengine, na kufuatilia zaidi maisha yako wewe mwenyewe.

15.kutokuhofu kuhusu kile ambacho watu wengine wanafikiri juu yako

Watu wengine wanasemaje kuhusu wewe? Kwa chochote kile unachokuwa unafanya, fahamu kuwa kuna watu ambao watakusema.

Hata ukicheka, kuna watu watasema, hebu mwone na huyu anavyocheka. Sasa unataka nichekeje? Binadamu bwana…

Kwa hiyo hilo lifahamu na wala lisikuchanganye.

Kama kuna kitu cha kuondoka nacho hapa ni kuwa kila mtu ana kazi yake. Wewe kazi yako ni kuhakikisha kuwa kipaji chako king’aa. Wengine kazi yao ni kuhakikisha kuwa wanakusema.

Nadhani umenielewa hapo.

14. kuwa na mipango ambayo unaifanyia kazi

Hakuna mtu ambaye huwa anaandika mipango ya kuwa mnene, mzembe,mjinga, asiyejali au baba/mama aliyetelekeza watoto.

Lakini ukweli ni kuwa kama hutaweka mipango ya kuwa afya njema, mchapakazi, anayejali, ni sawa na kuweka mipango ya kuzembea.

Kwa hiyo usije ukajishangaa umekuwa mnene, mzembe, asiyejali. Hukuweka mipango ya kuwa na hivi vitu, ila kwa kutokuweka mipango, unakuwa unastahili kuvipata.

Nimeandika sana, sasa mpaka naandika kuandika faslsafa. Ebu niishie hapa mengine nayaacha kwa ajili ya siku zijazo.

Kama una swali, maoni, au kitu chochote ungependa kusema, basi au hata ungependa kuchangia kidogo kwa ajili ya kuwezesha makala bora ziendelee kuwa hewani, basisi usisite kutucheki kupitia 0755848391.

©Haki zote zimehifadhiwa

Nimesikiliza na nitasikiliza tena


3 responses to “Vitu 21 Ambavyo Ni Lazima Kufanya Hata Kama Una Kipaji Kikubwa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X