Vitu vitano (05) Vitakavyokufanya uheshimike


Rafiki yangu bila shaka unaendelea vyema kabisa. siku ya leo ningependa kukushirikisha vitu vitano ambavyo vitakufanya wewe uweze kuheshimika kwenye kazi, kwenye mahusiano na kwenye maisha kiujumla. Kwa hiyo, kama unataka kuheshimika rafiki yangu, hivi hapa ni vitu vitano ambavyo unapaswa kuanza kufanyia kazi mara moja.

1. KITU CHA KWANZA NI KUCHAPA KAZI

Kazi ni kitu ambacho kinampa mtu heshima. Na hata maandiko mbalimbali yamethibitisha na kusisitiza hili la kufanya kazi kwa namna tofauti tofauti, huku maandiko maarufu yakiwa yale yanayosema kwamba asiyefanya kazi basi asile. Rafiki yangu, kazi ni moja ya kipimo cha utu.

Kwa hiyo, kama unataka kuheshimika kwenye jamii, basi fanya kazi.

Kwa watu wengi unapoongelea kazi, basi kinachokuja kwenye kichwa chao au kwenye akili zao ni kuwa ajira.  Yaani, kazi fulani hivi ya kukaa ofisini huku kukiwa na kiyoyozi, huku wenyewe wakiwa wananesa kwenye kiti fulani hivi amazing! Rafiki yangu, kuna tofauti kubwa sana kati ya kazi na ajira.

Kamusi ya Kiswahili sanifu inasema kazi ni shughuli anayofanya mtu kama vilekulima, kuandika au kufundisha.

Huku ikisema kuwa ajira ni kazi izitolewazo au zifanywazo kwa malipo katika kampuni serikalini au kwa mtu binafsi.

Kumbe kwa mantiki hiyo ndiyo kusema kwamba, kazi zipo nyingi. Kufanya kazi siyo lazima uwe umeajiriwa chini ya mtu, unaweza kufanya kazi hata kama hujaajiriwa. Unaweza kujishughulisha wewe mwenyewe. Kwa mfano unaweza kuanza kutengeneza vitumbua na kusambaza kwa kuanzia mtaani kwako. hivi kweli kitu kama hiki nacho kinaweza kukushinda?

Kitumbua kimoja kinauzwa shilingi 100. Kila siku ukijiwekea lengo la kutengeneza vitumbua na kuuza vitumbua 500, maana yake kila siku utakuwa unaingiza kiasi cha shilingi  elfu hamsini.  ili uweze kufanikisha lengo lako hili la kuuza vitumbua 500 kila siku unahitaji walau uwe na kijana mmoja ambaye anajituma na anafanya kazi kwelikweli. Mmoja wenu, anaweza kuwa yeye au wewe anakaa chini na kutengeneza vitumbua, huku mwingine akizunguka mtaani na kusambaza vitumbua kwa watu wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye maeneo yenye mkusanyko mkubwa watu kama stendi na sokoni.

Rafiki yangu, kwa jinsi hii unakuwa umejitengenezea kazi lakini wakati huohuo unakuwa tayari umetengenza ajira. Kwenye hiyo shilingi elfu hamsiini uliyouza ndani ya siku husika, ukitoa gharama au mtaji wa biashara yako. Huwezi kukosa kubaki na hela ya kwako, tena hela ya maana tu. ebu tuchukulie baada ya kutoa gharama zote ukabaki na elfu ishirini tu. Hii siyo hela kidogo, ukiwa unaingiza kiasi hiki cha hela kwa mwezi ni sawa na laki sita!

Wewe unakuwa siyo mtu wa viwango vya kawaida. Mpaka hapo unakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja, ukiendelea kukaza unashangaa baada ya miaka mwiili una kiwanda chako cha kutengeneza vitumbua. Usicheke, ujue hapa naongea vitu siriazi!

Kwa hiyo, rafiki yangu, achana na dhana ya kulia kuwa hauna kazi kuanzia leo hii. tafuta kazi na anza kufanya kazi.

  • Inaweza kuwa ni kutengeneza vitumbua kama nilivyokwambia
  • Inaweza kuwa ni vitu vingine kama kuuza karanga, kulima mboga, na vitu vingine vingi
  • Nadhani kuna mawazo mengi ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi leo hii, tena ambayo yanahitaji mtaji mdogo tu!

Tatizo kubwa linalowakumba vijana wengi ni kudharau kazi wakati hawana kazi. Na hii zaidi ni kwa wasomi ambao wamehitimu vyuo na ngazi nyingine, wanaona kwamba baadhi yakazi siyo kazi za viwango vya, hivyo, kitu pekee ambacho wao wanaamua kufanya ni kukaa bila kufanya kazi.

Rafiki yangu, kama hauna kazi na haujui kitu gani unaswa kufanya, basi usidharau. Chagua kazi yoyote ile kisha anza kuweka juhudi kwenye hiyo kazi. Ifanye ili iweze kukuingizia kipato.

Siyo eti kwa sababu umesoma basi muda wote unabaki kusuka nywele huku ukihofia kwenda shambani kufuga na kulima, huku ukiendelea kulalamika kuw ahuna kazi.

Kuuza vitu vya mia mia

Hapo juu nimetolea mfano wa mtu ambaye ameamua kujiajiri kwa kufanya kuuza vitumbua. Tena nikatolea mfano kuwa kitumbua kimoja kinauzwa shilingi mia moja! (japo vipo vitumbua ambavyo vinauzwa zaidi ya hapo). sasa hapa ninachotaka kukwambia ni kuwa vitu vya mia mia vinawapa hela kuliko unavyoweza kufikiria.

Ndio maana unaona mpaka mabilionea wanazidi kutegeneza vitu vya mia mia! Hivi kiberiti, kinauzwa shilingi ngapi vile… Huku mtaani kwetu kinauzwa shilingi mia moja sijajua huko kwenu. Mo Dewji ni bilionea mkubwa hapa Tanzania, ila huku mtaani kuna viberiti ambavyo ametengeneza yeye.

Hivi, pipi zinauzwa shilingi ngapi vile…najua utaniambia bei tofauti zikiwemo za mia moja na mia mbili au hata zaidi..

Kuna watu wenye hela zao, wamewekeza mabilioni ya hela wanatengeneza pipi eti. Tena pipi zingine zinauzwa shilingi hamsini tu za Kitanzania.

Ninachotaka kukwambia ni nini? ninataka kukwambia kwamba usidharau vitu vidogo, maana hivi vitu vidogo mwisho wa siku huwa vinakuwa na matokeo makubwa kuliko unavyoweza kufikiri.

2. KUTHIBITI HISIA ZAKO

Najua kuna watu wengi ambao tunaishi nao kwenye jamii na huwa wanatukosea au hata muda mwingine kutulazimisha tuingie kwenye migogoro nao.

Unaweza kushangaa unatembea mtu anakukanyaga halafu anakutukana. Au unaendesha gari, mtu akaku overtake katika eneo ambalo kisheria halafu anakuoneshea ile ishara fulani hivi ya kidole….

Sasa haya yote watu wanaweza kuyafanya ili kukukasirisha wewe, ila moja ya kitu ambacho unahitaji kukifanya ni wewe kuthibiti hisia zako. muda mwingine watu wanapokuwa wanafanya vitu kama hivi, wewe unahitaji kuwa mpole na hata kuwachukulia kama watoto wadogo.

Mtoto mdogo akikutukana, basi wewe utasema kwamba huu ni utoto. Sasa na kwa hawa inapaswa kuwa hivyohivvyo, badala ya wewe kukimbizana nao na kugombana nao, badala yake weka nguvu kubwa  kwenye malengo yako na ndoto zako. Wachkulie tu kama watoto wadogo, mtoto mdogo akikutukana ni wazi kuwa wewe huwezi kumtukana na kukasirika. Badala yake utasema huu ni utoto tu

3. KUSIKILIZA ZADI YA UNAVYOONGEA

Hiki ni kitu kingine ambacho kitakufanya uweze kuheshimika zaidi ujue dunia imejaa na waongeaji zaidi ya wasikilizaji, na kusikiliza ni ujuzi ambao unapaswa kuwa nao kwenye hizi zama.

Mimi kuna watu huwa wananipigia simu na kuongea watakavyo, kwa sababu huw wanajua kuwa tu nitawasikiliza. Unkuta mtu shida yake siyo kubwa sana, ila sasa anahitaji mtu ambaye atamsikiliza kwa umakini na kumpa muda way eye kuongea. Kile kitendo cha mtu kusikilizwa kinampa pumziko la roho nay eye anakuwa kama ametua mzigo mkubwa.

Rafiki yangu, anza kujenga utaratibu wa kusikiliza badala ya kuongea sana. nakuhakikishia kuwa utajifunz amengi kutoka kwa watu kuliko pale unapokuwa muongeaji sana.

NNE, KUWAACHA WATU KWENYE NAFASI NZURI KULIKO ULIVYOACHA.

Rafiki yangu, nataka nikupe zoezi moja kuanzia siku ya leo. Na zoezi hili ni kuwa, kila unapokutana na mtu, angalia ni kwa namna gani utamwacha katika hali nzuri kuliko ulivyomkuta. Unaweza kufikiri kwamba ili ufanye hili basi utahitaji kuwa na fedha, hapana.

Moja unaweza kuongeza juhudi ambazo watu wanaweka kwenye kazi wanazofanya. Kuna watu wanafanya kazi au vitu ila hawajawahi kupata mtu wa kuwapongeza na kukubali kile wanachofanya. Sasa kwa nini wewe usiwape moyo na kuwaambia kwamba kile wanachofanya ni kitu kizuri na chenye manufaa kwa jamii. Nakwambia rafiki yangu, hiki ni kitu kidogo, ila chenye nguvu kubwa sana ambacho unapaswa kuzingatia.

Je, na hilo rafiki yangu, linaweza kukushinda?

5.  KUWA NA FEDHA ZAKO MWENYEWE

Nadhani hili halina ubishi, kwenye hii blogu nimekuw anikiandika mara kwa mara kuhusu fedha. Lakini kwa lleo ningependa kusema kitu kimoja tu kuhusu fedha.

Na kitu hiki ni kuwa, fedha inakufanya uheshimike hata kama ni mdogo, na kama hauna fedha unadharaulika hata kama ni mtu mzima.

Mfano rahisi tu ni kwenye vikao vya familia. Mwenye fedha kwenye kikao anasikilizwa kuliko ambaye hana fedha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X