Jana nilikuwa naangalia mahojiano kati ya mtengenezaji wa maudhui kutoka Ghana maarufu sana kama Wode Maya na msanii wa Zimbabwe Jah Prayzah.
Kuna mengi waliyongea ila mimi binafsi niliondoka na mawili ambayo yamenigusa na ambayo nimeona nikushirikishe na wewe.
Kitu cha kwanza kabisa Jah Prayzah alisema hivi, mimi sikuchagua kuwa msanii ila nilichaguliwa kuwa msanii. Hii maana yake nini, maana yake ni kwamba kuimba kupo ndani yake. Hiki ni kipaji chake cha kuzaliwa nacho kabisa.
Nimekuwa nakushauri mara kwa mara rafiki yangu kuwa na wewe uhakikishe unajifanyia tathimini ili uweze kugundua na kutumia kipaji chako. Ukigundua kipaji chako rafiki yangu na ukakitumia, mara zote utakuwa ukifanya kazi yako na majukumu yako kwa furaha. Kwa sababu unafurahia kazi au kile unachofanya.
Kuna siku Arnorld Schwarzenegeer aliwahi kuulizwa, kwa nini, unakuwa na furaha sana muda wote mbali na kuwa unakuwa unanyanyua vyuma kwa muda wa saa tano kila siku. Watu walimuuuliza hivi kwa sababu waliona wengine waliokuwa wananyanyua vyuma hawakuwa na furaha hata kidogo kwenye maisha yao. Kwa kujibu hili Arnorld Swacherzenegger alisema kwamba, ninapenda ninachofanya. Rafiki yangu, kipaji chako ni kitu ambacho kinapaswa kitu kinachotoka moyoni. Kitu ambacho huoni kama umelzimishwa au umesukumwa kukifanya, badala yake unahisi kama kuna msukumo wa ndani kabisa ambao unakusukuma wewe kukifanyia kazi kipaji chako na kukifanikisha kwa viwango vikubwa
Kitu cha pili Jah Prayzah alisema kwamba, mimi mpaka leo bado nafanya kazi kwa bidii kama msanii mchanga. Yaani, bado najituma kwa nguvu zangu zote kama msanii ambaye hajatoboa, na sasa ndio anatafuta namna ya kuweza kutoboa na kwenda hatua ya ziada kwenye maisha.
Hiki kitu rafiki yangu na wewe kitumie kwenye kazi zako na kwenye kitu chochote kile ambacho unafanya. mara zote fanya kazi kama vile wewe bado ni mchanga kwenye sekta ambayo unafanyia kazi, hata pale unapokuwa umekua na umeweza kufika viwango vya juu. Kwa nini?
Ili niweze kujibu kwa nini yako kwa undani zaidi, naomba nikutolee mfano mzuri kwenye biashara, mwanzoni mtu anapoanzisha biashara anakuwa anajituma na kuweka nguvu kubwa sana kuhakikisha kwamba biashara yake inakua. Anatafuta wateja, anawapigia simu na mambo mengine mengi. Yote haya anayafanya kwa lengo moja tu, la kuhakikisha kwamba anafanya mauzo zaidi kwenye biasahra yake. Lakini kadiri biashara hiyo inavyokuwa inazidi kukua, inafikia hatua ambapo yule mtu anasahua ile misingi iliyomwinua na hivyo, kujikuta kwamba anaanza kufanya kazi kwa mazoea.
Na hapo ndipo anguko la biashara nyingi huwa linatokea.
Hiki kitu huwa hakitokei tu kwenye biashara peke yake, bali pia kwenye kwa watu wenye vipaji vyao. Unakuta mtu ana kipaji kizuri, anakifanyia kazi, anakua na kufikia viwango vya juu, ila sasa baada ya muda anasajisahau, anarelax na kuanza kuishi maisha ya kawaida sana. kitu ambacho huwa kinamepekea kwenye anguko. Hapa ndipo huwa unasikia habari za kwamba
Msanii fulani ameshuka kiwango
Au mchezaji ameshuka kiwango
Kinachomfanya ashuke kiwango siyo kitu kingine bali ni kwamba zile juhudi alizokuwa anaweka mwanzoni kwenye kazi, sasa haweki juhudi hizohizo, kitu hiki kinamfanya aanze kushuka kidogo kidogo na baadaye anashuka kabisa.
Kwa hiyo rafiki, mara zote fanya kazi kama vile ndio kwanza unatafuta maisha.
Rafiki yangu, ili kukurahisishia safari yako ya kukifanyia kazi kipaji chako. Nimekuandalia kitabu maalumu kabisa, kinaitwa Kipaji ni Dhahabu. Nashauri sana uweze kusoma kitabu hiki cha kipekee kwa shilingi elfu kumi tu.
Kupata nakala yako, wasiliana nami kwa 0755848391