FANYA MAZOEZI


Siku moja nilikuwa nasoma makala mtandaoni, kwenye makala hiyo mwandishi akawa amesema kwamba Michael Jackson ambaye ni gwiji kwenye muziki wa hiphop alikuwa ni mmoja watu waliokuwa wanafanya mazoezi kwa muda mrefu sana kabla ya kuonekana mbele ya watu. Kwa baadhi ya watu kitu hiki kilionekana cha ajabu sana, Ukilingananisha na kuwa Michael Jackson alikuwa akiimba na kucheza kwa namna ambayo ilikuwa inaonenekana ni njia ya asili. Inawezekanaje gwiji kama Michael Jackson awe anafanya mazoezi kwa muda mrefu hivyo?

Na hiki ni siri ambayo nimegundua vijana wengi hawaielewi. Wapo wanaodhani kuwa ukishakuwa na kipaji peke yake basi anaweza kulala na kila kitu kikajipanga.

Kama kuna kitu unapaswa kufahamu kwenye maisha yako ni kujua kwamba mazoezi ni jambo moja muhimu sana ambalo utapaswa kulifanyia kazi kwenye maisha yako. Tena utahitaji kuhakikisha kuwa unafanya mazoezi ya mara kwa mara kwenye kitu ambacho unafanya, kiasi cha kuweza kufikia ubobezi kwenye hicho kitu.

Kila eneo lina vitu vyake vya kufanyia mazoezi. Kwa mwanasheria kuna vitu vyake ambavyo anapaswa kufanyia kazi maeozi.

Mazoezi yanakujenga, mazoezi yanakuimarisha na njia ya wewe kupanda kutoka hapo ulipo kwenda unapotaka kwenda ni kufanya mazoezi.

Tujifunze kwa wachezaji wa mpira wa miguu

Wachezaji wa mpira wa miguu ni miongoni mwa watu ambao wanafanya mazoezi bila kuchoka. Kipindi ambacho ligi inakuwa imepumzishwa wenyewe wanaenda mpaka kambini. Na kambi hii inakuwa ni maalumu kwa ajili ya kufanya mazoezi ili waweze kufanya vizuri kwenye mashidano yanayofuata. Na siyo hilo tu, hata baada ya kuwa wamaenda kwenye mashidano huwa hawaachi kuanya mazoezi. Hiki kitu ndicho na wewe unapaswa kuwa nacho pia kwenye kazi na vile unavyofanya. Jijengee utaratibu wa kufanya mazoezi kwenye kazi au kitu unachofanya. Hakikisha kwamba unafanya mazoezi bila ya kuchoka.

Mazoezi yanakuimarisha. Kadiri unavyokuwa unazidi kufanya mazoezi ndivyo unazidi kuimarika na kubobea zaidi.

Mazoezi yanakuondolea hofur woga na wasiwasi. KILA MARA ukifanya mazoezi unairmarika na kukielewa kitu husika.

Ebu fikiria unataka kuwa muongeaji mzuri mbele ya watu. (by the way, kuongea mbele ya watu ni kitu ambacho kinawashinda watu wengi sana na ni kituambacho unahitaji ukifahamu kwa uzuri sana).

Sasa kitu hiki unaweza kukifanyia mazoezi kwa kuhakikisha kwamba kila siku unatenga nusu saa tu ya kufanya hivi. Kwenye hii nusu saa unaamua kuwa unaongea mbele ya watu na kuwasilisha mada yako ambayo umeandaa. Au hata kama hakuna mtu ambaye yuko mbele yako.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X