Hii ndiyo sababu kuu kwa nini unapaswa kutoa thamani kubwa kuliko mteja anavyokulipa


Ni miaka kama mitano hivi imepita tangu nimegundua kanuni moja muhimu sana ambayo nimekuwa naitumia kwenye kila kitu ninachofanya. Na kanuni hii siyo nyingine bali ni kutoa thamani kubwa zaidi kwa mteja kuliko mteja anavyolipia.

Tangu nimegundua kanuni hii nimekuwa naitumia kwenye vitabu vyangu vyangu vyote. Ambacho nimekuwa nafanya ni kuwa, kwa kitabu ambacho mteja analipia elfu ishirini, nahakikisha kwamba kinakuwa na thamani ya laki mbli na zaidi. hivyo, namwuzia mteja kitabu chenye thamani ya laki mbili na zaidi kwa elfu ishirini tu.

Nafanya hivi siyo kwamba ninakuwa sijui, bali kwa sababu nataka mtu yeyote yule anayenunua kitabu au kupata huduma yoyote kwangu, apate thamani mara kumi zaidi na vile ambavyo analipia.

Hii ni kanuni muhimu sana ambayo na wewe unapaswa kuizingatia na kuanza kuitumia kuanzia leo hii kwenye biashara yako. Hakikisha kwamba bidhaa au huduma unayoitoa kwa mteja inakuwa na na thamani mara kumi zaidi ya vile ambavyo anavyolipia.

Tumia hii kanuni hata kwenye kazi. hakikisha kwamba unafanya kazi kwa viwango vikubwa mara kumi zaidi kuliko watu wengine wanavyofanya. Jitume mara kumi zaidi ya wengine. Soma vitabu mara kumi zaidi yaw engine. Jibrand mara kumi zaidi ya wengine. Hiki kitu kitakusaidia wewe kuweza kujenga jina lako na hata kujitofautisha.

Unapaswa kufanya hivi, kwa sababu katika ulimwengu wa leo ni watu wachache sana ambao wanafanya hivi.  Wengi wanapenda njia za mkato za kupata mafanikio ila hawapendi kuweka kazi. kufanya kazi zaidi ya vile wanavyolipwa kujituma na kuwapa wateja thamani.

Ukiweza kufanya hivi, maana yake utawateka wateja wako na kuwafanya waendelee kupata huduma kwako na hivyo kujenga jina katika namna ya kipekee ambayo hakuna mtu mwingine anaweza kujenga jina kama wewe.

Kazi yako ya kufanya kuanzia leo hii ni kuanza kutoa thamani mara kumi zaidi ya vile unavyolipwa. Jiulize ni bidhaa ipi haitoi thamani mara kumi zaidi ya vile ninavyolipwa? Kama kuna bidhaa ya aina hiyo, basi anza kuiboresha ili iweze kutoa thamani kubwa zaidi kwa mteja kuliko vile anavyokulipa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X