Hii ni tabia muhimu unayopaswa kuanza kuishi nayo kuanzia leo hii. (usishike simu kama kitu cha kwanza unapoamka asubuhi, na wala usishike simu kama kitu cha mwisho kabla ya kwenda kulala).


Siku zinazidi kusogea kwelikweli. Mwaka uliokuwa mpya sasa hivi, tumeshaanza kuuaga taratibu. Siku siyo nyingi utaingia mtaani na kuanza kuzisikia nyimbo za krismasi zikipigwa. Ukiona hivyo, ujue kwamba mwaka unazidi kusogea na na siku siyo nyingi tutakuwa tunauaga. Lakini kabla mwaka huu haujaisha, kuna tabia ambayo ningependa uanze kuifanyia na kuachana nayo

TABIA YA KUTOSHIKA SIMU YAKO KAMA KITU CHA KWANZA UNAPOAMKA ASUBUHI

Kuna siku kulikuwa na kichekesho fulani hivi, kuwa mtu anaamka asubuhi kabla hata hajajua kama kichwa chake kimeshikana kiwiliwili chake anakuwa tayari ameshashika simu yake. Japo ni kichekesho ila kina ukweli mkubwa sana ndani yake. Asilimia kubwa ya watu, asubuhi kabla hata hajatoka kitandani, anakuwa tayari ameshika simu yake.

Na ukifuatilia ni kitu gani cha msingi ambacho huyu mtu anakuwa anafanya na simu yake, huwezi kukiona, zaidi zaidi utakuta kwamba anajibu SMS hata zisizokuwa na maana. Au anaingia kwenye mitandao ya kijamii kuangalia watu wamekoment nini kwenye kitu alichopost jana yake. Sasa rafiki yangu, kuna kitu kimoja ambacho ningependa uweze kufahamu. Na kitu hiki syo kingine bali ni wewe kuepukana na kushika simu kama kitu cha kwanza unapoamka asubuhi.

Ukiamka asubuhi, anza kwa kushukuru kwa kuiona siku nyingine mpya. Baada ya hapo anza kutahajudi.

Kisha jiambie kauli chanya, kauli kama

  • Mimi ni bilionea.
  • Mimi ni sumaku ya fedha na fedha zinanifuata
  • Mimi ni mshindi na nimezaliwa kushinda.
  • Mimi nastahili kupata vitu vizuri na vizuri vimetengeezwa kw ajili yangu. Na nyinginezo nyingi.

 Katika huu muda hakikisha kwamba unapata maji ya uvuguvugu, kisha toka nje uvute pumzi kwa nguvu na ikiwezekana kukanyaga chini kwenye udongo il kuungana na asili na kufanya mazoezi. Baada ya hapo soma walau kwa dakika 20 tu.

Itapendeza sana kama saa moja la kwanza baada ya wewe kuamka kama hutashika simu kabisa.

Hii ndio kusema kwmaba ndani ya saa lako moja hili utakuwa umeweza kufanya makubwa, ikiwa ni pamoja na kupangilia asubuhi yako kwa kuweka to do list. Ukitoka hapo sasa unaweza kuendelea na mambo mengine.

Hivyo hivyo wakati wa kulala. Usishike simu kama kitu cha mwisho kabisa kabla ya kulala. Tafiti nyingi zinaonesha kuwa unapaswa kushika simu walau saa mbili kabla ya kulala. Hii ni kwa sababu simu, ina mwanga ambao unaingiliana na usingizi. Hivyo, unaweza kujikuta kwamba unakosa usingizi muda mwingine, kumbe kinachokukosesha usingizi siyo kingine bali ni simu yako.

Rafiki yangu, najua wazi kuwa simu ina manufaa mengi ila ninachokuomba ni kitu kimoja tu. Usishike simu kama kitu cha kwanza unapoamka asubuhi, na wala usishike simu kama kitu cha mwisho kabla ya kwenda kulala. Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X