Sababu Tano (05) kwa nini unapaswa kuukataa umasikini


Limekuwa ni  kama jambo la kawaida kusikia watu wanajiita masikini, wanyonge. Kuna watu wanajisifia kuwa masikini kama vile kuwa maskini jambo la kheri au jambo la sifa. Kwa kulifahamu hili, siku ya leo ningependa kukupa sababu 15 kwa nini unapaswa kuukataa umasikini. Kweli kabisa, unapaswa kuukataa umasikini kwa nguvu zako zote.

Kwanza kwa sababu umasikini dhambi.

Ndio, umasikini ndio chanzo cha maovu. Kama hauna hela, utafikiria kwenda kuiba, kama hauna hela hela utafikiria kufanya maou ili upate chochote kile cha kuingiza mkono kinywani.

Hakuna sifa yoyote ile kwenye umasikini ukatae kwa nguvu zako zote.

Ukiwa hauna hela hata huduma nzuri hupati. Ukiumwa hospitali unapaona kama magereza wakati ni sehemu ya kwenda kupata tiba, unaogopa kwenda hospitali kwa sababu hauna hela.ila ukiwa na hela huduma zote nzuri zinakuwa kwa ajili yako. Watoto wako wanasoma shule yoyote unayotaka wewe, siyo shule ya mtaani kwako ambapo walimu wanafundisha kwa kuamua.

Pili, umasikini hauwezi kukufanya usaidie jambo lolote lile

Huwa kuna shughuli mbalimbali za kijamii ambazo watu huwa tunachangia, lakini huwezi kuchangia kwenye hizi shgughuli kama wewe ni masikini, sanasana utakuwa unazengea kwenye hiyo sherehe tu ili uone watu wanavyochanga ili na wewe uwanyanye hiyo pesa.

Tatu, Umasikini unakunyima sauti

Kinachotokea kwenye ngazi ya familia ndicho pia kinatokea kwenye ngazi za kimataifa. Nadhani umewahi kuona kwenye vikao, masikini anakosa sauti ya kuchangia hoja. Na hata akichangia hoja yake inaonekana ni ya kimasiikini na hivyo inatupiliwa mbali. Hivyo hivyo, kitu hiki ndicho kinatokea kwenye ngazi ya kimataifa. Nchi zetu zinashindwa kujihami na kuchangia hoja. Na hata zikichangia hoja, hoja zao zinakuwa hazina mashiko. Unajua kwa nini? kwa sababu, ni nchi masikini. Ili tuondoe umasikini wan chi, tunapaswa kuanza na mtu mmoja mmoja. Wewe ukiondoka kwenye umasikini, basi utakuwa umesaidia sana kuuondoa nchi hii kwenye umasikini. Anza leo hii mchakato wa kuondoka wewe mwenyewe kwenye umasikini

Nne, Unatumia nguvu ileile kuwa tajiri kama ilivyo kuwa masikini

Nguvu ileile unayoitumia kwenye kuwa masikini na kubaki masikini ndiyo nguvu ile ile inayohitajika ili kuwa tajiri. Sasa kwa nini usichague kuwa tajiri.

Tano, Utajiri unakupa machaguo mengi

Ukiw atajiri unakuwa na machaguo mengi sana ya kufanya kwenye maisha. Unaweza kununua kitu chochote kile unachotaka, unaweza kwenda popote pale unapotaka.

Unaweza kuamua mtoto wako wasome shule yoyote. Unaweza kuamua kula chakula chochote, siyo kila siku ugali mlenda, halafu unadanngaya watu eti ooh, ugali mlenda ni mtamu sana. wakati hauna pesa ya kununua chakula kingine.

Tafuta hela ili uwe na mchaguo mengi bila ya kuwa na ukomo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X