Siku ya leo nina ujumbe mfupi kwako rafiki yangu. Na ujumbe wangu Ni kwamba kama wewe unapambamia lengo au ndoto yako na unalifanyia kazi mara kwa mara, basi Kaa ukijua kuwa watu hawatakupuuza siku zote.
Ndio wanaweza kukupuuza mara moja au mara mbili, Ila hawatakupuuza siku zote. Kuna siku watanyoosha mikono juu na kusema ngoja tufuatilie kwa kina kile anachofanya huyu mtu. Na kwa jinsi hii utakuwa umewapata.
Kitu kimoja ninachotaka kukusihi Ni kuwa Mara zote hakikisha kwamba unaandaa kazi bora.
Kazi yako yoyote iwe ni bora maana mara zote kuna mtu mpya ambaye hajawaji kufuatilia kazi zako na siku hiyo ndio ndio anafuatilia hiyo kazi.
Kumbe kama leo kuna MTU anafuatilia kazi yako Mara ya kwanza, hakikisha kwamba hakutani na kazi ya viwango vya chini, badala yake, hakikisha kazi yako inakuwa bora, Mara zote na sehemu zote.