Hili ndilo kosa moja kubwa wanalofanya watu kuhusu kuwekeza
Rafiki yangu jamii yetu imejuwa haiewi vizuri uwekezaji. Kitu hiki kimewafanya watu wajihusishe na miradi feki na ambayo haieleweki na hata wakati mwingine kutapeliwa.
Moja ya kosa ambalo watu wamekuwa wanafanya kuhusu uwekezaji Ni kusubiri mpaka watakapokuwa na fedha ili waanze kuwekeza.
Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu. Usisubiri mpaka uwe na pesa ili uanze kuwekeza. Anza na kile ulichonacho
Kwenye makala yangu ya jana, nilikueleza ni kwa namna gani unaweza kuanza kuwekeza kwenye hisa kwa kununua walau hisa kumi tu. Hisa kumi zinagharimu fedha ya kawaida ambayo ukichagua vizuri unaweza kuimudu.
Ubora wa wewe kuanza kuwekeza sasa hivi Ni kuwa kadiri uwekezaji wako utakavyokuwa unakua, wewe pia utakuwa unaongeza maarifa yako zaidi na zaidi. Na hivyo, kuendelea kubobea na kufanya maamuzi sahihi zaidi.
Nikwambie kitu rafiki yangu, usisubiri mpaka uwe na kila kitu ili uanze kuwekeza. Anza kuwekeza hata kwa kutumia kiasi hicho kidogo ulichonacho sasa.
Nakushauri, upate kitabu changu Cha Maajabu ya kuwekeza kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kitabu hiki kitakufaa sana na KItakupa mwongozo unaouhitaji ili uanze kuwekeza.
Usisubiri mpaka uwe na kila kitu ili uanze kuwekeza.
Imeandikwa nami rafiki yako
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz