Hivi vitu ndivyo vinavyotofautisha uwekezaji kwenye hisa na uwekezaji kwenye maeneo mengine kama nyumba, kilimo cha miti na vito vya thamani


Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

Leo rafiki yangu nataka nikwambie vitu vinavyoafanya uwekezaji kwenye hisa kuwa ni uwekezaji wa kipekee kuliko uwekezaji wa maeneo mengine kama nyumba, kilimo Cha miti na vito vya thamani. Kinachotofautisha uwekezaji huu Ni:

Moja, unaweza kuanza kuwekeza kwenye HISA kwa kiwango kidogo tu Cha fedha .
Ili unielewe vizuri unapaswa kujua kuwa kiwango cha chini kabisa Cha uwekezaji kwenye hisa ni hisa 10.

Hivyo, ukiwa na fedha ya kununua hisa kumi tu, unaweza kuanza uwekezaji wako kwenye hisa. Sasa swali la kujiuliza hapa ni kuwa Ni fedha kiasi gani inahitajika ili kumwezesha mtu kununua hisa kumi?
Ukweli ni kuwa hakuna kiwango rasmi cha kukuwezesha kununua hisa kumi, ila kiasi Cha fedha kinategemea na bei ya hisa kwenye soko kwa wakati husika.
Mfano, sasa hivi ninapoandika hapa.
Bei ya chini kabisa ya hisa ya kampuni mojawapo kwenye soko la hisa ni shilingi 120. Hii ndio kusema kuwa kama unanunua hisa kumi za kampuni utatakiwa kuwa na shilingi 1200/- ukiongeza na gharama za madalali hii unaweza kufikia 2200/- hivi.

Hivyo, kwa kiasi kidogo Cha 2200/- unaweza kuanza kumiliki hisa za kampuni hiyo.

Na hisa zinazouzwa bei ya juu kwa sasa ninapoandika hapa zinauzwa kwa shilingi  16,200/-. Hii ndio kusema kuwa thamani ya hisa kumi itakuwa Ni sawa na 162,000/-. Tukiongeza gharama za madalali unaweza kutoa kiasi Cha 163,300/-.

Kwa hiyo, kwa kiasi Cha 163,000/- unaweza kuanza kuimiliki hisa za kampuni hii.

Ila jambo Kama hili haliwezekani kwenye uwekezaji mwingine. Hivi kweli rafiki yangu unaweza kumiliki nyumba kwa kuanza na shilingi 2200/- au 163,000/-.

HAIWEZEKANI.

Pili, hisa zinatoa mwanya wa kununua kidogokidogo. Unaweza kununua hisa kumi leo. Kesho hisa hamsini. Siku nyingine hisa kumi na tano na kuendelea. Ila huwezi kuwekeza kwenye NYUMBA kwa kuanza kununua chumba leo, baada ya wiki ukanunua sebule, halafu siku nyingine ukanunua choo😂😂.
Ni au ununue kitu chote kizima au la umekikosa…

Nakushauri rafiki yangu uchangamkie uwekezaji kwenye hisa kwa kupata elimu sahihi ambayo utaanza kuitumia kuanzia Leo hii. Pata kitabu changu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kwenye hiki kitabu utajifunza mengi kuhusu uwekezaji huu wa kipekee kwenye maeneo haya ya hisa, hatifungani na vipande.

Fanya uwekezaji wa shilingi 5,000/-tu siku ya leo. Ili uweze kupata kitabu hiki. Lipia kitabu hiki kwa 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Kumbuka kitabu hiki kinapatikana kwa njia ya mtandao (Kama ebook au softcopy). Na gharama yake ni 5,000/- tu. Ukilipia elfu tano, utatumiwa kitabu hiki kwa baruapepe au WhatsApp. Lipia Sasa. Namba ya malipo ni 0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA..

Umekuwa nami
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X