Habari ya leo rafiki yangu, bila shaka unaendelea vyema kabisa.
Leo ningependa nikwambie kitu ambacho kimekuwa kinawakwamisha watu wengi na kuwafanya washindwe kufanikisha makubwa . Kitu Hiki siyo kingine bali ni kukosa malengo makubwa ambayo wanayafanyia kazi kwenye maisha yao.
Ili uweze kunielewa vizuri hapa naomba nianze kwa kukupa mfano wa kawaida tu, unaweza kukuta MTU anadaiwa hela.
Anapambana kwa nguvu zake zote kutafuta pesa ili alipe deni lake.
Na kweli pesa anapata na deni analilipa, Ila akishamaliza kulipa deni anakosa msukumo wa kuendelea kupambana na kutafuta pesa zaidi ili kununua Uhuru wake wa Kifedha.
Au unaweza kukuta mtu anatembea kinyonge. Lakini inapotokea hatari ya ghafla, MTU huyo anaruka na kukimbia Kama vile siyo yeye.
Huu uwezo tulionao siyo TU tuitumie wakati wa hatari peke yake, bali tuitumie pia muda mwingine ambao siyo wa hatari pia. Kwa ajili ya kufanya makubwa
Kinachowafanya wengi washindwe kuutumia huu uwezo mkubwa Ni kwa sababu hawana malengo. Unapokuwa hauna malengo, maana yake unashindwa kujisukuma maana hauna kitu chochote cha kukusukuma.
Rafiki yangu Mara zote kuwa na melengo ambayo unayafanyia kazi. Malengo yawe makubwa na yakusukume muda wote kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Kama hauna malengo basi kaa chini Uweke malengo sasa.
Malengo ni Moto wa kukusukuma wewe kufanya Yale ambayo wengine wanaona kama hayawezekani.
Tenga muda leo hii ukae chini Uweke malengo. Muda huu ni uwekezaji ambao unaufanya. Kwa ajili ya kesho yako.
Nataka tu ufahamu kuwa bila ya kuwa na malengo, hutajisukuma kufanya kitu Cha maana.
One response to “Kitu Hiki Ndicho Kinawafanya wengi washindwe kufanya makubwa”
Ni habari njema sana