Mambo Muhimu ya KUZINGATIA kabla hujawekeza fedha Yako


Kitabu hiki kinapatikana kwa 5,000/-. No softcopy

Rafiki yangu mpendwa. Bila shaka unaendelea vizuri. Kila kunapokucha watu wanabuni njia mpya za kutaka kuondoka na kukaa na fedha zako. Watakuja kwako na maelezo mengimengi wakikushawishi uweze kuwapa fedha zako ambazo wewe mwenyewe umezitafuta kwa jasho na damu kubwa sana. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unashawishika kutoa fedha zako kwa kila mtu anayekuja kwako kukwambia ana fursa nzuri ambayo ukiweka fedha utatajirika.

Sasa ili kuepukana na Hilo, ningependa kwanza tujue vigezo muhimu vya kuzingatia kabla hujawekeza fedha zako. Chukulia tu mfano una milioni moja sasa hivi mkononi na unataka kuiwekeza. Utaiweka wapi? Je, utaiweka kweye hisa, hatifungani, vipande vya UTT, utanunua shamba au utanunua Kiwanja pembezoni mwa mji? Utawekeza kwenye kilimo,au utaenda Geita ununue gramu kadhaa za dhahabu? Utafanyaje ili fedha yako uiwekeze sehemu salama na ambayo itakupa mrejesho mzuri Bila kuharibu uwekezaji wako.

Na kwa nini utawekeza huko?

Vifuatavyo Ni vigezo muhimu unavyopaswa kuzingatia kabla ya kuwekeza fedha zako.

(i) Mrejesho wa uwekezaji

Kitu cha kwanza unachotakiwa kuangalia ni mrejesho gani utaupata kutokana na uwekezaji wako.  Hiki kigezo ambacho unapaswa kuangalia..

Asilimia kubwa ya watu wanapowekeza huwa wanaangalia hiki kigezo peke yake. MTU anaambiwa weka laki moja tukupe laki tatu kesho kutwa, anakubali.

Mrejesho wa uwekezaji Ni kigezo unachopaswa kuangalia,Ila kigezo hiki siyo mwanzo na mwisho. Kuna vigezo vingine vya kuangalia.

Ni muhimu kama mwekezaji kupima iwapo uwekezaji anaouchagua utakuwa na matokeo yanayoridhisha na iwapo uwekezaji huo ni bora kuliko uwekezaji mwingine ambao unaweza kuufanya. Lakini hiki kisiwe kigezo peke yake Cha kuangalia.

Kumbuka sehemu ambayo ina  mrejesho mkubwa na imekidhi vigezo vingine hapo chini  ni bora  kuliko sehemu yenye mrejesho  mdogo.

(ii) Hatari za uwekezaji .

Kama muwekezaji hauwezi kuangalia mrejesho wa uwekezaji tu bila kuangalia hatari za uwekezaji ambazo unazibeba pale ambapo unakuwa unawekeza katika uwekezaji wa aina fulani,

Mfano kama kuna msitu ambao umeambiwa una dhahabu ambazo ukifika unaokota tu kama mawe ila ukaambiwa huo msitu ni hatari una kila aina ya wanyama ambao ukiingia tu wanakugawana ndani ya sekunde, kama mtu mwenye hekima utapima, ni kweli huu msitu una dhahabu tele ila uwezekano wa kutoka na dhahabu ni asilimia 0.0001%,uwezekano wa mimi kupoteza maisha katika huo msitu ni mkubwa kama bado unajali maisha yako  basi utaachana na  hiyo dili maana  ni dili la  moto !

Katika uwekezaji vivyo hivyo hatuangalii tu mrejesho wa uwekezaji tunaangalia pia hatari za uwekezaji kama zinatufaa, nikuongezee kitu hapa kwa kadri unavyobeba hatari kubwa za uwekezaji basi na mrejesho wako uwe mkubwa ili kufidia hatari ambazo umezibeba, kwa hiyo kitu cha pili huwa tunagawanya uwekezaji kuendana na hatari za uwekezaji,

kama unaona hatari za uwekezaji ni kubwa Sana kiasi kwamba utapoteza uwekezaji wako basi achana  na  huo uwekezaji. Hatari za uwekezaji ni ule uwezekano wa kuwa unachokitegemea kukipata kinaweza  kisitokee

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy) 0755848391

(iii) Ukwasi  wa uwekezaji (liquidity)

Sehemu hii nayo ni muhimu kwa muwekezaji makini. Ili kutengeneza fedha ni lazima uwe na uwezo wa kuuza uwekezaji wako pale unapohitaji kufanya hivyo.

Ukwasi maana yake ni uwezo wa kubadilisha uwekezaji wako kuwa katika mfumo wa pesa . Uwekezaji unaoelezwa kuwa na ukwasi maana  yake ni uwekezaji ambao ni rahisi kuubadilisha kuwa fedha na uwekezaji unaoelezwa kuwa hauna ukwasi maana yake ni uwekezaji usio rahisi kubadilishwa kuwa fedha hasa pale inapotakiwa na mwekezaji.

Kama ukwasi una shida maana yake siku ukitaka fedha zako kwa haraka unaweza kutoa macho kama mjusi kwani hutapata wa kumuuzia uwekezaji wako. Katika uwekezaji ambao nimetaja hapo juu kila uwekezaji una sifa yake katika sifa hizi nne je ni uwekezaji gani unaona unakufaa?

Mfano uwekezaji kwenye ardhi ni mzuri ila ukwasi wake ni mdogo. Unaweza kuwa na kiwanja au nyumba, lakini mpaka uiuze upate fedha keshi, inakuwa na mlolongo mrefu na haupati fedha pale unapoihitaji.

(iv) Usalama wa uwekezaji wako

Hapa kuna watu wengi wamepoteza pesa kwa kuwekeza sehemu ambazo hazina usalama ila zinatoa ahadi ya mrejesho mkubwa.

  Kuna watu ambao hawana uelewa wa masuala ya kifedha au wanataka kupata utajiri wa haraka basi wanaingia kuwekeza kwenye biashara za upatu au biashara zisizo na uhakika wa mrejesho wa fedha na mwisho wa siku wanapoteza pesa.

Usalama wa uwekezaji wako ni moja ya kigezo muhimu sana kama unataka kuwekeza, ni lazima sehemu ambayo unataka kuwekeza iwe na usalama wa pesa yako.  Waswahili wanasema ndege aliye mkononi ni bora kuliko ndege wawili walio porini, katika uwekezaji sheria namba moja ni kuwa usipoteze pesa yako kwa kuwekeza sehemu ambayo si salama.

Na sheria ya pili Ni kuwa usisahau sheria ya kwanza.

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Wekeza 5,000 tu ujifunze maarifa muhimu kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. 0755848391

(v) Malengo yako 
Kuwa na malengo katika kutimiza mipango yako ni muhimu. Katika uwekezaji ni muhimu kuwa na malengo. Malengo yanakupa mwongozo wa eneo gani uwekeze na wapi usiwekeze.

Mfano mtu anayewekeza kwa akilenga kupata gawio la ambalo atatumia. Hawezi kuwekeza sawasawa na MTU ambaye anawekeza ili kuimiliki kampuni.

Vi) Nani yupo nyuma ya uwekezaji huo?
Ni muhimu sana kabla ya kuwekeza kujua nani Atakuwa nyuma ya fedha utakazoweka. Uongozi mzuri unaleta fedha zaidi kwa wawekezaji. Uongozi mbaya unaleta hasara.

Vii) Mahali fedha itakapowekwa
Unapaswa kujua kwa uhakika kuwa nikiweka fedha yangu hapa, hii fedha itawekezwa kwenye maeneo gani. Kama watu wanakushawishi uwekeze fedha kuwa utapata faida kubwa. Jiulize Ni biashara gani watakuwa wanafanya.

Ni jukumu lako mwekezaji kujihakikishia kuwa eneo unapowekeza Ni eneo zuri na linalokufaa.

Usihadaike tu kwa sababu uneambiwa utapata faida kubwa.

Vii) Idadi watu wanaokimbilia kuwekeza
Mara nyingi watu wa kawaida huwa wanaokimbilia kuwekeza kwenye miradi feki. Hii Ni kwa sababu huwa hawafuatilii na kujifunza kwa kina kuhusu uwekezaji.

Wanawekeza na walizwa. Ukiona watu wengi wanaokimbilia kwenye uwekezaji husika, ufuatilie kwa ukaribu zaidi kabla hujawekeza. Mara nyingi utakufa huo uwekezaji Ni feki.

Ni Mara nyingi sana utasikia watu wakiwekeza kwenye Aina mbali mbali za uwekezaji na kulizwa. Lakini Ni Mara ngapi umesikia watu wanaongelea uwekezaji kwenye hisa zinazouzwa kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam? Au vipande vya UTT?

Soko la hisa la Dar limekuwepo kwa zaidi ya miaka 20 Sasa na mifuko ya uwekezaji wa pamoja ya UTT, imekuwepo kwa zaidi ya miaka 15. Watu wanawekeza huko kila mwaka, Ila Ni Mara ngapi umesikia watu wakiuongelea huu uwekezaji?

Kaylinda je?

Vii). Umri
Hiki Ni kigezo kingine Cha kuangalia wakati unawekeza. Umri siyo namba tu, Bali una kitu Cha kutwamvia kuhusu uwekezaji.

MTU anayestaafu au anayekarivia kustaafu, hawezi kuwekeza sawasawa na mwanafunzi wa kidato Cha nne.

Ndio maana nataka nashauri kila mmoja ahakikishe amepata mwongozo wa kitabu cha uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande. Kinaitwa MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE.

MWISHO: Haya masuala ya kuambiwa wekeza laki tukupe laki mbili baada ya siku mbili yaepuke sana. Hakuna biashara inayoweza kukupa uhakika wa kupata tu kwa asilimia 100. Kila biashara ina kiwango chake hatari.

Unapokuwa unawekeza fuatilia, kila kitu unachohitaji kujua kuhusu biashara husika. Usiwekeze tu kwa mkumbo.

Hakikisha una nakala ya kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kinauzwa 5,000/-. Softcopy. Nitakutumia kwa whatsap au baruapepe.

Karibu sana.


One response to “Mambo Muhimu ya KUZINGATIA kabla hujawekeza fedha Yako

  1. Ahsante sana bwana kwa mafunzo haya juu ya uwekezaji. Si siku nyingi zilizopita mtu fulani aliponiibia pesa. Akajifanya kuwa yeye ni mkereketwa na atanisaidia kwa kunipelekea pesa ili nijiendeleze baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO 19. Baada akaniambia nifungue akaunti na kampuni fulani aweze kunipelekea fedha hizo. Akanipa nambari ya simu ili nimpigie fulani aniongoze katika shughuli hiyo. Katikati yule jamaa akaanza kuomba pesa za kubadilisha pesa kutoka hii currency kwa nyingine. Nikapeleka eflu hamsini kwanza. Baada ya muda akaniambia nipeleke nyingine hapo nikasitasita na kugundua kuwa huu ni wizi. Nikamfokea na akaniambia nimenusurika nende nikale kuku yangu!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X