Mwaka juzi nilikuwa naongea na ndugu mmoja kuhusiana na hali yake ya kiuchumi. Alikuwa katika hali mbaya kiuchumi.
Nilimwuliza kama huwa ana tabia ya kuweka akiba. Akaniambia huwa anaweka akiba Ila huwa anaitumia siku chache mbeleni. Nikamwambia kuwa kwa Hali hiyo utapaswa kufungua akaunti benki ili uwe unaweka fedha zako huko. Lakini kikubwa zaidi nikamwambia anza kuwekeza pia kwenye soko la hisa kwa kununua hisa.
Nikaanza kumweleza kuhusiana na hisa na namna zinavyofanya kazi.
Nakwambia rafiki yangu, yule ndugu alinisikiliza kwa sababu Moja tu, kwa sababu muda ule tulikuwa tunatembea kwenda sehemu ili nimlipe kiasi fulani Cha fedha kwa kazi alivyokuwa amefanya.
Ingekuwa siyo hiyo fedha, Nina uhakika siku hiyo asingenisikiliza….
Baada ya kulazimika kunisikiliza katika mazingira Kama hayo, aliuliza swali kwa kusema. Hisa zenyewe zinauzwa bei kubwa…utakufa hisa moja inauzwa elfu sabini!
Nilishangaa kuona anasema hivyo, lakini nikawa nimeendelea kumweleza kuwa kwa sasa kwenye soko la hisa la Dar Es Salaam hakuna hisa inayouzwa kwa bei kubwa hivyo.
Sasa ambacho nimegundua watanzania wengi hawana elimu ya kutosha juu ya uwekezaji huu wa kwenye hisa. Kama huamini toka nje sasa hivi uliza watu kumi tu kuwa wanajua Nini kuhusu uwekezaji kwenye hisa.
Unaweza usipate hata mmoja wa kukupa jibu sahihi.
Uwekezaji kwenye HISA ni uwekezaji ambao mtanzania yeyote anaruhusiwa kufanya. Ninaposema mtanzania yeyote namaanisha bila kujali Ni mtoto, kijana au mzee. Bila kujali Ni mrefu, mfupi, mwembamba au mnene. Bila kujali ni mhitimu wa darasa la saba, msomi wa chuo kikuu, dada wa nyumbani au ofisa anayefanya kazi ikulu.
Wote tunayo haki ya kuwekeza kwenye soko la hisa kwa kununua hisa za kampuni yoyote tutakayoipenda
Kwenye soko letu la hisa hata wageni wanaruhusiwa kuwekeza. Ila serikali yetu imetupendelea zaidi. Wageni (watu kutoka nje ya nchi) hawaruhusiwi kumiliki zaidi ya asilimia 60 ya hisa zote za kampuni iliyo kwenye soko la hisa.
Serikali inafanya hivi ili kuwawezesha watanzania kuimiliki hisa, kumiliki uchumi na vitegauchumi.
Rafiki yangu, changamka. Nenda kanunue hisa ili uanze kuimiliki kampuni na uchumi.
Lakini kabla hujaenda kichwa kichwa kwenye kununua hisa, fanya hivi. Hakikisha umepata mwongozo wa kukusaidia kwenye uwekezaji kwenye HISA. Na mwongozo huu nimeandika kwenye kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki ni kitabu ambacho unapaswa kutembea nacho popote pale utakapokuwa. Kitakusaidia sana kwenye uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Gharama ya kitabu hiki ni 5,000/-. Softcopy. Lipia kwa 0684308755 jina Ni GODIUS RWEYONGEZA.
Karibu sana
Karibu ukipate