Jinsi Ya Kufungua akaunti ya mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND)


Juzi niliandika makala kuhusu mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND). Swali ambalo nilipokea kutoka kwa wengi waliosoma makala hii lilikuwa ni kwa namna gani naweza KUFUNGUA akaunti kweye mfuko huu wa FAIDA.

KITU hiki kimenisukuma nikuandalie Makala nyingine kukuonesha ni kwa namna gani unaweza KUFUNGUA akaunti kwenye mfuko huu wa FAIDA. Unajua unawezaje kufungua akaunti.

Fanya yafuatayo.

BONYEZA *152*00# kwenye simu yako.

Kisha chagua namba 1 kama inavyoonekana hapo chini

Baada ya hapo chagua namba 6 Kama inavyoonekana hapo chini

kisha chagua namba 1 tengeneza akaunti ya binafsi.

Baada ya hapo utaweka majina yako kamili

Kisha utaweka tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa

Ukibonyeza hapa, kuna hatua zaidi, utapata. Zifuate Mpaka mwisho ili ukamilishe kusajili akaunti yako.

Ukishasajiri akaunti yako, endelea mbele kwa kuhakikisha unaweka kiasi kisichopungua elfu kumi kwenye akaunti. Kwa kufanya hivyo, utakuwa umefungua akaunti.

kila la kheri

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.

Mtandaoni, vitabu vyake unaweza kuvipata kupitia mtandao wa GETVALUE kwa KUBONYEZA HAPA


2 responses to “Jinsi Ya Kufungua akaunti ya mfuko wa FAIDA (FAIDA FUND)”

 1. habari kaka Godfrey?
  kama unavyojua watanzania wengi wametapiliwa kila wakijaribu kuwekeza mtandaoni. vipi kuhusu mfuko huu unawezaje kuhakikisha usalama wa pesa zako?
  Pia napenda kuomba utupe mchanganuo wa faida ya mfuko huu?

  • Mfuko huu ndio kwanza unaanza. Hivyo, mchanganuo wa faida kwa sasa haupo, maana bado haujaanza kufanya. Ila nina michanganuo ya faida ya mifuko mingine hasa mifuko iliyo chini ya UTT.

   Kama ndio kwanza unaanza, nashauri zaidi ungewekeza kwenye mifuko ya UTT.
   UTT wana mifuko mitano na mifuko yote imekuwa inafanya vizuri.
   mchnganuo wa faida wa mifuko yote ya UTT nimeuleza kwenye kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki ni kitabu ambacho nashauri na wewe upate, maana utajifunza na kujua mengi kabla hujachukua uamumuzi wa kuwekeza.
   Gharama ya kitabu hiki kwa sasa ni 20,000/- kwa nakala ngumu. Nakala laini pia ipo, ni 10,000/- tu. karibu sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X