Kuna kitu kimoja nakijua kuhusu wewe rafiki yangu. Na kitu hiki ni kwamba mwaka 2023, ungependa kupata matokeo ya tofauti. Matokeo ya tofauti kwenye kila eneo ambalo utakuwa ukilifanyia kazi.
Kama unataka kupata matokeo ya tofauti mwaka 2023, basi hakikisha kwamba unakuwa tayari kufanya vitu vya tofauti. Yaani, vitu ambavyo hujawahi kufanya siku za nyuma.
Huwezi kutegemea kupata matokeo ya tofauti mwaka 2023, huku ukiwa unaendelea kufanya vitu vile vile bila ya kubadilika.
Ni lazima uwe tayari kufanya hivi vitu vya tofauti, labda swali la kujiuliza ni vitu gani vya tofauti ambavyo naweza kufanya mwaka 2023 vikanipa matokeo ya tofauti.
VIfuatavyo ni vitu vitatu vya tofauti ambavyo unaweza kufanya mwaka 2023, vikakupa matokeo ya tofauti kwenye kipato chako, kwenye uwekezaji, kwenye afya yako, kwenye watu unaokutana nao na kwenye kila kitu unachofanya. Kiufupi kama unataka kuufanya mwaka 2023, uwe mwaka wa baraka na kila kitu utakachogusa basi kibadilike kuwa dhahabu, basi hakikisha kwamba unafanyia kazi yafutayo.
Kwanza hakikisha kwamba una malengo ambayo unayafanyia kazi. rafiki yangu, bila malengo makubwa mwaka 2023, hutaweza kutoboa. Kwa hiyo, kama kuna kitu ambacho unapaswa kuanza nacho mwaka 2023, basi ni kuhakikisha kwamba unaanza kwa kuweka malengo. Weka malengo na yafanyie kazi.
Pili, kuwa tayari kuchukua hatua. Rafiki yangu, bila ya kuchukua hatua, malengo uliyojiwekea hayataweza kutimia. Ni lazima uwe tayari kuchukua hatua hata kama ni kidogo.
Wengi hufikiri kwamba ili wafanikishe malengo yao, basi wanapaswa kusuburi siku moja ya mwisho wa mwaka ambapo malengo yao yatatimia, ukweli ni kwamba malengo makubwa huwa hayatimii kwa siku moja ya mwisho wa mwaka. Badala yake yale unayokuwa unayafanya kila siku, kila kukicha ndiyo yanakupelekea wewe kwenye kufanikisha malengo yako au kufeli kwenye kufanyia kazi malengo yako. Ndio maana nimekuandalia kitabu murua kabisa cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Ukipata kitabu hiki, utajifunza na kuona ni kwa namna gani unaweza kufanyia kazi malengo makubwa kwa kuanza kidogo kidogo.
Mambo madogo madogo unayoyafanyia kazi leo hii, yana uwezo wa kukuletea matokeo makubwa. Hakikisha kwamba unapata nakala ya kitabu hiki cha kipekee leo hii. Nakala yako ni 20,000/- tu. na utatumiwa popote pale utakapokuwa nchini.
Tatu ni kukaa na watu sahihi. Watu sahihi rafiki yangu watakufanya uweze kupiga hatua na kufika mbali. Hivyo basi, kama unataka kuufanya mwaka 2023, uwe mwaka wa kipekee hakikisha kwamba unaungana na timu ya watu sahihi. Kuna timu ya watu sahihi ambayo unahitaji kujiunga nayo mwaka 2023, na timu hii ni ya watu ambao wamejiunga na semina ya kufungua mwaka 2023. Ukijiunga na timu hii utakutana na watu sahihi ambao wana mtazamo chanya kama wewe.
hawa wote utakutana nao, endapo tu utajiunga na semina ya kufungua mwaka 2023.
Karibu kwenye semina hii ya kipekee sana.
Kila mwanzo mwa mwaka na katikati mwa mwaka huwa Kuna semina ambayo huwa naiendesha.
Mwakani wakati wa kufungua mwaka mpya tunatarajia kuwa na semina ya kufungua mwaka ambayo itafanyika kuanzia tarehe 15.
Na itadumu kwa siku 15 mfululizo. Semina hii ya kipekee ambayo itafanyika kwa njia ya mtandao, inalenga kukupa maelezo ya kina yatakayokusaidia kuuanza mwaka mpya kwa mtazamo sahihi na kuuweza kuufanikisha kwa viwango vikubwa sana. Semina hii inaitwa JINSI YA KUONGEZA THAMANI YAKO 2023.
Kwenye Semina hii utajifunza Mambo
1. Namna ya kuongeza thamani yako
2. Namna ya kuongeza kipato chako mara mbili mpaka mara kumi zaidi
3. Njia za kuweka malengo na kuyafanyia kazi kwa usahihi ndani ya mwaka 2023.
3. Nguvu ya vitu vidogo kwenye kuongeza thamani yako binafsi na mengine mengi
Hii Ni semina ya siku 15 mfululizo ambayo imeshiba mambo ya msingi sana yanayokufaa wewe na yatakayokusaidia wewe kuuanza mwaka kwa usahihi na kupiga hatua na kufika mbali.
Katika siku hizi 15 utapata masomo 15 yaliyoandaliwa kwa kina na ambayo yatakusaidia wewe kuanza KUONGEZA THAMANI YAKO ndani ya mwaka 2022.
Ni matarajio yangu kuwa baadaa ya semina hii, utakuwa na mbinu za kukusaidia wewe kuongeza thamani yako binafsi na kipato chako walau Mara mbili zaidi
Hakikisha kwamba haukosi Semina hii, ya kipekee sana
Semina itafanyika lini?
Itaanza tarehe 15 Januari na itadumu kwa siku 15
Semina itafanyika wapi?
Semina itafanyika mtandaoni (WhatsApp) kwenye kundi maalumu la WhatsApp.
Je, Kuna ada ya kujiunga na Semina.
Ndiyo ada ipo. Ada ya semina ni 15,000/- tu. Kwa kila mshiriki kwa siku zote za semina.
Mwisho wa kulipia ni tarehe 10 Januari.
Njoo uuanze mwaka wako kwa kiusahihi na kwa kupata mwongozo utakaokusaidia kuufanyia kazi mwaka mpya kutokea kwenye nafasi nzuri.
Kuthibitisha ushiriki wako. Tuma malipo yako kwenye Namba ya simu 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Karibu sana
Whatsap group la semina: https://chat.whatsapp.com/FbzmwEVkObKIuqeR4pIZmu
Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza
Unaweza kusoma makala na mafunzo yake zaidi kwenye blog yake ya SONGAMBELE (www.songambele.co.tz)