Kuna MTU kaniuliza swali hili, Nani anapaswa kusoma vitabu na kwa nini
Jana kwa upande wangu imekuwa Ni moja ya siku moja bize Sana. niliamka saa nane usiku, nililala saa sita usiku. Na hapa nipo ikiwa Ni saa kumi alfajiri nimeahaamka.
Ninachotaka kukwambia siku ya leo siyo kuamka mapema, Bali kusoma vitabu.
Ninaamka mapema hivi kila siku, ikiwa Ni lengo la mimi kupata muda wa ziada wa kujifunza na kusoma vitabu.
Ikumbukwe sisomi kwa ajili ya mitihani, wala sisomi ili kupata cheti chochote.
Labda kujibu swali lako vizuri zaidi nipende tu kusema kwamba MTU yeyote ambaye anajua kusoma na kuandika anapaswa Kuwa msomaji wa vitabu.
Bila kujali wewe unafanya kazi ya kupiga debe
Ni machinga
Ni mfanya usafi kwenye kampuni au mkurugenzi
Unapaswa kujijengea utaratibu wa kusoma vitabu. Vitabu vitakujenga na vitabu vitakuwa na uwezo wa kukutoa hapo ulipo Mpaka uweze kufika unapotaka.

Kuna sababu nyingi kwa nini unapaswa kusoma vitabu, lakini sababu kuu ni kwamba unapaswa kusoma vitabu kwa sababu vitakufumbua macho na kukuonesha yale ambayo huwezi kuyaona kama ingekuwa husomi vitabu.