Kila kitu huwa kinafanyika kwa sababu…
Kuna mtu unayeweza kuwa unawona anafanya jambo fulani, ukafikri labda yeye ana kipaji na uwezo mkubwa kukliko wewe, ila baadaye ukija kufuatilia ukagundua kwamba suala kubwa siyo kwamba ana uwezo mkubwa kulliko wewe. Siyo kwamba ana konekisheni nyingi kuliko wewe, siyo kwamba amebarikiwa kuliko wewe, labda tu ni kwamba ana SABABU KUBWA KULIKO WEWE. Yaani, ile kwa nini yake ni kuwa
Sababu ndizo huwa zinatusukuma sisi kufanya jambo fulani au kutofahanya jambo fulani. Sababu ndizo huwa zinatusukuma sisi kujituma kwenye kufanyia kazi jambo fulani au kutofanya na kuacha jambo fulani.
Ukiwa na sababu kubwa ndiyo inakusukuma wewe kuamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kwenda kufanyia kazi malengo na ndoto zako, huku wengine wakiwa wamelala. Sababu haihitaji visingizio. Sababu haihitaji urudi nyuma, sababu haihitaji urembe mwandiko.
Sababu inahitaji kitu kimoja tu uzalishe matokeo.
Wewe sababu kubwa inayokusuma wewe kufanyia kazi malengo yako ni ipi. Au visingizio ndivyo vimekutawala?
2 responses to “Sababu yako ni ipi”
Napenda sana mafundisho yako. Lakini nilikua naomba utengeneze makala ambayo itahusu jinsi ya kuacha vilevi(pombe, sigara, bangi, madawa ya kulevya, n.k) maana hii ni changamoto kubwa sana katika jamii yetu. Na ni chanzo cha umasikini pia. Ila kila ukimuuliza mtu anaetumia vilevi atakwambia amejaribu kuacha lakini ameshindwa. Naamini kama utaweza kuwasaidia utaokoa jamii kubwa sana.
Asante kwa mrejesho, nitalifanyia kazi