Jinsi Ya Kubobea Kwenye Kitu Chochote


Rafiki yangu habari ya leo. Bila shaka unaendelea vyama, siku ya leo ningependa kukwambia njia ambayo itakusidia wewe kuweza kubobea kwenye kitu chochote ambacho unafanya, na njia hii siyo nyingine bali ni kufanya kitu husika kwa marudio na mara kwa mara.

Yaani, kama unataka kubobea kwenye kitu chochote kile usikifanye kitu  hicho mara moja kisha ukaacha, badala yake weka nguvu na muda wako mwingi kwenye hicho kitu kwa muda mrefu mpaka kieleweke.

Watu wengi huwa wanapenda kubobea kwenye vitu ila sasa tatizo ni kwamba huwa wanajikuta kwamba wanafanya vitu vingi sana kwa wakati mmoja. Yaani, unakuta kwamba mtu anafanya kitu fulani siku ya leo. Halafu kesho yake hicho kitu anakisahau, kesho anapambana na kitu kingine, hivyo hivyo.

Wewe unayesoma hapa nakupa mbinu ya kubobea kwenye kitu chochote kile. Na mbinu hii ya kubobea ni wewe kufanya kitu hicho kila mara bila kuacha.

Tatizo la watu wengi wanafanya vitu vizuri kwa mazoea

Ninaposema kwamba ufanye kitu kila mara, simaanishi kwamba ufanye kitu hicho kwa mazoea. Kuna tofauti kati ya kufanya hicho kitu kila siku na kwa moyo na kufanya kitu hicho kila siku kwa mazoea. Kuna stori ya mfanyakazi mmoja ambaye alienda kuomba kuongezea mshahara kwa bosi wake. Baada ya kupitia maombi yake, bosi alimwambia kwamba, hawezi kuwmongezea mshahara kwa sababu  huwa anafanya kazi siku moja kwa mazoea au kwa marudio. Yaaani, kwamba huyo mfanyakazi, alikuwa kila siku anaenda kazini kweli, ila hakukuwa na kitu cha tofauti ambacho alikuwa anafanya.

Alikuwa anaenda kazini ili kupoteza muda. Nadhani umewahi kuwasikia wale watu ambao huwa wanasema kwamba ninapoteza muda tu. Kwako haipaswi kuwa hivi, yaani, usifanye kazi au kitu chochote kile kwa ajili ya kupoteza muda tu. Mara zote na siku zote hakikisha kwamba kila siku yako inakuwa ni bora zaidi ya jana. Yaani, usiweke mazoea kwenye kazi.

Kila dakika ambayo unafanya kazi, weka nguvu, akili yako na kila kitu humo.

Ebu tuchukulie mfano unataka kubobea kwenye uandishi.

Unahitaji kuhakikisha kwamba unafanya mazoezi kila siku. Yaani, unapaswa kuandika kila siku. Huwezi kukaa tu kwenye kochi huku ukiw aunategemea kwamba siku moja utakuwaj akuwa mwandishi mbobevu bila ya kuchukua hatu aya ziada. Unataka kubobea kwenye uandishi kuanzia siku ya leo? Anza kuandika.

Au labda tuseme kwamba unataka kubobea kwenye uwekezaji, unapaswa kuhakikisha kwamba unawekeza nguvu na muda wako kwenye kujifunza uwekezaji na kufanyia kazi yale unayojifunza kwa uhalisia.

Unataka kubobea kwenye mchezo wowote. Unapatakiwa kila siku kufanya mazoezi ya kutosha kuhusiana na mchezo husika.

Kwa jinsi hiyo rafiki yangu, utakuwa umejiweka kwenye nafasi ya kufanya makubwa na kwenda mbali zaidi kuliko pale ambapo utakuwa hufanyii kazi haya utakayojifunza.

Kuna siku nilikuwa nasoma wasifu wa Kobe Bryant, kitu kikubwa nilichokuja kugundua kutoka kwake ni kwamba alikuwa mtu wa mazoezi na mazoezi ndiyo yalimfanya kuweza kufikia alipofikia. Nahakufanya hicho mara moja. bali alikifanya mara kwa mara mpaka akaweza kupata matokeo makubwa.

Hivyo basi, nipende kusisitiza ujumbe muhimu kwako rafiki yangu ambaye unapenda kufika mbali. Kitu hiki kwamba kama unataka kubobea kwenye kitu chochote kile basi kuwa tayari kufanya kitu hicho mara kwa mara na marudio bila ya kuacha mpaka pale utakapopata matokeo unayotaka.

Asante sana na nikutakie wakati mwema.


One response to “Jinsi Ya Kubobea Kwenye Kitu Chochote”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X