Rafiki yangu ili uweze kuishi vizuri kwenye dunia ya sasa. Ni vizuri sana ukihakikisha kwamba una ujuzi wa kufanya jambo au kitu fulani.
Hiki ni kitu ambacho wewe mwenyewe unaweza kujenga. Ujuzi wako unaweza kukutambulisha popote na kwa yeyote. Ujuzi wako unaweza kukulipa.
Kama hauna ujuzi ni muda wako sasa wa kuhakikisha kwamba unaanza kujenga ujuzi. Badala ya wewe kupoteza muda kwenye mitandao ya kijamii ukiangakia vitu ambavyo havina manufaa, utumie muda huohuo kuhakikisha kwamba unajenga ujuzi wako.
Utakuwa hujitendei haki kama unalalamika Kuwa maisha Ni magumu. Vyuma vimekaza halafu baada ya hapo unapoteza muda kwenye mitandao ya kijamii au kwenye vijiwe ukipiga stori. Badala ya kujenga ujuzi ambao utakulipa zaidi.
Ubora wa ujuzi ni kwamba ukishakuwa nao unakuwa nao. Hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuuiba kwako.
Hivyo basi rafiki yangu, kuanzia sasa chagua aina ya ujuzi ambao unaweza kujenga. Kwenye kitabu changu cha NGUVU YA KUCHUKUA HATUA YA KWANZA nimeeleza Aina 21 za ujuzi ambazo unaweza Kuwa nazo. Simaanishi kwaamba unapaswa Kuwa na Aina zote. Hapana.
Badala yake unapaswa kuchagua Aina moja tu ya ujuzi na kukomaa na huo kwanza.
Baadhi ya ujuzi unaoweza Kuwa nao ni Kama
1. Kuchora
2. Kuandika
3. Kuongea na kuwasilisha mada watu wakakusikiliza (uneni)
4. Graphics
5. Kuuza
Zipo Aina nyingi za ujuzi, Ila ujumbe wangu kwa leo ni kwamba chagua Aina moja tu ya ujuzi na hakikisha kwamba unakomaa na hiyo Aina ya ujuzi bila ya kurudi nyuma.
Kila la kheri.