Maisha Yako Ni wajibu wako


Maisha Yako Ni wajibu wako, usisubiri MTU aje akusaidie wewe kufanya vitu ambavyo wewe mwenyewe unapaswa kufanya.

Ebu chukulia vitu vya kawaida tu Kama KUTUNZA muda
Kuweka akiba
Kuamka mapema
Kufanya Kazi kwa bidii
Kusoma vitabu na kufanyia kazi Yale unayojifunza.

Je, hivi unahitaji mtu akusaidie kuvifanya? Na hivi unalalamika kwamba serikali haijavifanya kwa niaba yako? Hivi kweli uko siriazi na maisha yako?

Chukua hatamu ya maisha yako kuanzia leo hii, maana maisha ni wajibu wako. Ukishinda ni juu yako. Ukishindwa ni juu yako pia.

Kazi ya kufanya siku ya leo.
Angalia vitu ambayo umekuwa unalalamikia Sana.
Jiulize je, vipo ndani ya uwezo wangu?

Kama. Vipo ndani ya uwezo wako, vifanye. Kama vipo nje ya uwezo wako, achana navyo.

Kila la kheri.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X