Hiki kitu kimoja hakiwezi kukupa mafanikio unayotaka


Watu wengi wanapenda kupata mafanikio kiasi kwamba ukiingia kwenye chumba Chenye watu kumi na Kuuliza wangapi wanapenda kufanikiwa? Utashangaaa kuona mikono zaidi ya kumi ikiwa imenyooshwa juu. Kwa Nini? Kwa sababu baadhi ya watu wanapenda Sana mafanikio kiasi kwamba wanakuwa tayari kunyoosha mikono miwili juu.

Japo watu wengi wanapenda mafanikio, Ni wachache Sana ambao wanakuwa tayari kuchukua hatua na kuweka juhudi kupata mafanikio wanayotaka. Unakuta MTU anaendelea kufanya vitu kwa namna ileile waliyokuwa wanafanya babu zake Huku akitegemea kupata matokeo ya TOFAUTI.

Hiki kitu Albert Einstein alikiita ujinga aliposema; ujinga ni kufanya vitu vilevile huku ukitegemea kupata matokeo ya TOFAUTI.

Kumbe kwa mantiki hiyo ili upate matokeo ya TOFAUTI. Ni sharti. Na ninasema sharti uwe tayari kuchukua hatua za TOFAUTI.
Hatua za kuanzisha biashara Kama ulikuwa hauna biashara.
Hatua za kuongeza mauzo Kama tayari uneanzisha biashara
Hatua za kujenga timu na kuwa na wasaidizi kwenye biashara. Huwezi kuendelea kufanya majukumu yooote kwenye biashara huku ukitegemea kupata matokeo ya makubwa.
Hatua za KUTANGAZA biashara yako na nyingine nyingi.

Ni kweli hatua hizi muda mwingine zinaogopesha.
Ni kweli hatua hizi muda mwingine zinatufanya tusijisikie sawa. Ila zinapaswa kuchukuliwa Mara zote.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X