Jinsi ya kunufaika na muda wako wa safarini


Kwa namna moja au nyingine KATIKA maisha yetu ya kila siku Kuna kusafiri.
Unaweza kuwa unasafiri umbali mrefu sana kama kutoka mkoa mmoja KWENDA mwingine.

Lakini muda mwingine Unaweza kuwa unasafiri eneo fupi tu. Dakika kumi, kumi na tano au SAA moja.

Bila kujali, umbali unakwenda, Bado safari Ni safari na muda huu unapokuwa unatoka eneo moja kwenda jingine Unaweza kuutumia kwa manufaa.

Huu muda wa Kutoka eneo moja kwenda jingine ukiuunganisha kwa siku, kwa wiki na kwa mwaka utajikuta kwamba unapata muda mwingi sana. Brian Tracy anasema kwa mwaka mmoja muda ambao MTU anakuwa safarini ni sawa na mhura mmoja wa chuo.

Kumbe huu muda huu ukiutumia vizuri ni wazi kuwa utajifunza mengi, na pengine hata kitu ambacho umekuwa unatamani kujifunza kwa siku nyingi utakielewa.

Ebu chukulia umekuwa unatamani kujifunza uandishi kwa siku nyingi. Ukaamua tu kuhakikisha unautumia muda ule wa safari kusikiliza vitabu na kozi za uandishi, na Kisha ukawa unatenga dakika chache tu za kuandika kila siku. Ni wazi kuwa baada ya muda utabobea.

Au kama umekuwa unapenda kujifunza mauzo. Unaweza kuutumia muda huu wa ziada kusikiliza mafunzo ya sauti ya mauzo ambayo yatakufanya uweze kubobea kwenye mauzo.

Kumbe basi, wito wangu kwako Ni mmoja TU rafiki yangu, kuanzia Leo hii, hakikisha kwamba unautumia vizuri Sana muda wako wa safari.
Utumie kujifunza na hasa kujifunza kwa kusikiliza mafunzo ya sauti. Yaani, Audiobooks

Hizi zitakupa maarifa yenye manufaa makubwa.

Rafiki yangu, tunahitaji kuleta mapinduzi kwenye jamii zetu. Na hatuwezi kuleta mapinduzi kwa kuendelea kufanya Mambo Yale Yale ambayo tumekuwa tunafanya kila siku. Badala yake fanya mambo ya TOFAUTI kidogo kabisa. Kama kusikiliza mafunzo ya maana wakati wengine wanapoteza muda huo kwa kuchati, kusikiliza miziki na vinginevyo.

Kila la kheri

Kisha andika AUDIOBOOKS


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X