Siri itakayokuwezesha wewe kufanya makubwa


Rafiki yangu wa ukweli, sina shaka wiki yako umeianza vizui sana. Hongera sana kwa kazi.

Siku ya leo ningependa tu kukwambia kuwa kama unataka kufanya makubwa kuna vitu muhimu sana ambavyo unapaswa kuzingatia nakuhakikisha kwamba umevifuata. Vitu hivi ni pamoja na na wewe kufanya majukumu makubwa kwanza asubuhi kabla hujafanya kitu kingine.

Kama una majukumu mawili, basi nguvu yako kubwa unapaswa kuilekeza kwenye jukumu ambalo ni kubwa kwa upande wako.. Yaani, lile jukumu ambalo usipolifanya, litakuwa na madhara makubwa aidha ya muda mfupi au ya muda mrefu kwa upande wako. Ni jukumu ambaloendapo likifanyika kwa ukamilifu, litaleta matokeo mazuri. Haya majukmu mengine yanaweza kusubiri lakini hili halipaswi kusubiri.

Mara nyingi watu wengi huwa wanaliogopa na kulikwepa hili jukumu. Kitu ambacho huwa kinawafanya wakimbilie kufanya majukumu madogo madogo ambayo hayana nguvu huku wakiacha majukumu ambayo yana nguvu. Ninachotaka kukwambia siku ya leo ni kwamba, kama uanataka kufanya makubwa. kuwa tayari kufanyia kazi majukumu ambayo muda mwingine yanaonekana ni magumu.

Ni kwa sababu haya majukumu ndiyo ambayo yanaweza kukusogeza wewe kule unapotaka kufika.

Haya majukumu japo yanaogopesha lakini ndiyo ambayo yatachangia kwenye kulipwa kwako kwa asilimia 80, ukilinganisha na majukumu ambayo ni asilimia 20 ambayo siyo ya muhimu sana ambayo unakuwa unafanya.

Kazi yako siku ya leo ni kujua ni kuhakikisha kwamba unayajua majukumu yako ambayo ni ya muhimu sana, kisha kuyafanya hayo kwanza kbla hujafanya majukumu mengine.

Kwenye mambo 10 ambayo unapaswa kufanya leo, siyo yote yana umuhimu na nguvu sawa. Ni baadhi tu, au machache kabisa ambayo yana nguvu kubwa. wekeza kwenye haya machache.

Kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X